Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 288
- 412
Habari za muda huu waungwana, naomba kutoa kero yangu haswa kwenye Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa, mimi ni mkazi wa Dumila. Kumekuwa na kero ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza ng'ombe kwenye mashamba ya watu yenye mazao bila hofu yoyote ile. Nasema hivi sababu nishalima Kimamba, Miyombo mwishoni nikaamua kurudi kulima Dumila.
Kero hii imekuwa ni ya Miaka mingi sana lakini Serikali imeshindwa kabisa kutatua hii kero Kati ya Wakulima na Wafugaji. Sidhani kama shamba ndilo linamfuata mfugaji bali mfugaji ndio anafuata shamba.
Mfano mdogo ukienda Kimamba, Masai akiingiza ng'ombe shambani ni bora ukimbie uache shamba walishe mpaka wamalize maana ukileta ujuaji na kugombana nao kukuua ni dakika moja tuu.
Masai anatembea na rungu, sime na fimbo sisi Wakulima saa nyingine unakuta hata ukiwa na jembe halikusaidii chochote. Hiyo nguvu ya kupambana na Masai unaitoa wapi na uko porini? Hata ukisema umpigie kiongozi anaweza akakujibu kuwa yuko mbali, hivyo mtafute kiongozi mwingine hapo unakuwa huna msaada wowote au anaweza kusema anakuja akaja muda umeenda na wamasai washatoa ngombe shambani kwako na kuwakimbiza.
Akisha ondoa ng'ombe shambani unakuwa ushapoteza ushahidi. Pengine unaweza na kuwa na simu janja na kuanza kurekodi wakijua tu unarekodi unapigwa na Masai au hata kunyanganywa simu. Hili jambo linaumiza sana sana. Hivi majuzi kati Juni 2025 kuna ndugu yangu alinipigia simu na kunieleza kuna ng'ombe walikamatwa Kijiji cha Changarawe ambapo kule kuna ndugu zangu nao ni Wakulima pia.
Waliharibiwa mazao yao na ng'ombe za wafugaji jamii ya kimasai Lakini mpaka sasa hawajapata haki zao ilhali tathmini zilifanyika, serikali ilikuwepo, nikisema serikali namaanisha maaskari, viongozi wa vijiji na hata afisa mifugo, wakulima pamoja na wananchi wa eneo hilo. Kesi mpaka sasa hivi haijaisha.
Pamoja na kukamatwa na kulipishwa faini Masai waligoma kupeleka ng'ombe mnadani kwa kigezo cha kuwa wanaonewa na viongozi na wananchi. Kilichofuata Mkuu wa Wilaya ya Kilosa aliwafuata wafugaji na kuwaomba wapeleke ng'ombe mnadani sababu Serikali inakosa mapato. Hakukutanisha wafugaji na wakulima bali aliwafuata Wafugaji tu na kuwaomba wapeleke ng'ombe mnadani.
Je, hii ni haki? Kwamba mkulima hathaminiwi kulishiwa mazao yake huku akiwa katumia nguvu nyingi pamoja na kupoteza pesa nyingi huku familia ikiwa inamtegemea, bali Wamasai ndio wana haki ya kuthaminiwa mpaka kwenda kubembelezwa wapeleke ng'ombe mnadani?
Kesi zikipelekwa mahakamani wamasai wanatoa pesa (RUSHWA) ili waonekane hawana hatia hivyo kuwapa kiburi cha kuendelea kuwanyanyasa wakulima sababu wao wana pesa.
Masai akiuza ng'ombe mmoja au wawili haoni tabu wakati kutoa rushwa ili mkulima akandamizwe na hakimu huku mkulima akibaki anaumia kwa kutokuwa na uwezo wa kuendesha kesi sababu ya kutokuwa na uwezo wa kifedha. Na kawaida ya masai yeyote akitoa pesa (rushwa) ili mkulima asipate haki yake huwa wanasema hawafichi kabisa. Wengine wanasema kabisa kuanzia viongozi wa chini mpaka ngazi za juu wamewashika na kuwaweka Mfukoni hawawezi kufanya lolote juu yao.
Mfano sasa hivi Masai anasema atalisha kwenye mashamba ya watu mpaka pale pesa zao walizotoa za kampeni ziishe. Hii ni haki?
Kwanini viongozi wa Kilosa wanakuwa dhaifu hivi? Serikali iko wapi? Ina maana hiki kilio cha wakulima kilosa hakisikiki? Mheshimiwa Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan hajasikia kuhusu hili?
Kwanini serikali ikae kimya? Kuna nini kinacho endelea kati ya mfugaji na Serikali huku serikali ikimuacha mkulima kwenye maumivu makali? Kuna wengine kilimo hicho hicho ndicho kinacho somesha watoto wao, wengine wanategemea kula hapo hapo wengine ndio ajira zetu.
Mimi mwenyewe ni muathirika mmojawapo wa hawa wafugaji wa jamii ya kimasai. Unamkamata yuko kwenye shamba lako, ukiwa mwenyewe anaweza hata kukuuwa. Naomba utupazie sauti. Rushwa imetawala sana Kilosa. Viongozi Wanapokea rushwa kuwakandamiza wakulima na kuwaacha wamasai wakiendelea kuwakandamiza wakulima. Tunaomba hili swala likomeshwe, sio kwa viongozi hata kwenye mahakama zetu wasipokee mifuko yenye pesa kutoka kwa wamasai na kusahau kumpa haki yake mkulima.
Kuna hakimu mmoja wa mahakama ya Masanze nasikia ni mpokeaji 'mpunga' mkubwa, juzi tu kuna kesi imemuharibia sifa alipokea mambo kutoka kwa Masai mmoja bahati nzuri yule aliyekuwa na kesi naye hakukata tamaa akahakikisha anapata haki yake yule Masai mpaka sasa hivi yupo magereza, na ukitaka kuamini fuatilia utaupata ukweli.
Mahakimu wajue mpaka tathmini inafanyika na serikali ni kwamba mifugo ya masai imeshafanya uharibifu. Lakini pia naomba serikali iingilie kati hili swala kuanzia ngazi za wenyeviti wa vitongoji, wenyeviti wa vijiji, Watendaji wa Vijiji, Madiwani, Maaskari, Mkuu wa Wilaya mpaka ngazi za juu kukomesha hii rushwa ili kumkandamiza mkulima.