Mgogoro wa Uhuru park unatokota

Patachimbika aisei, hii nchi sina uhakika tunakokwenda au kuelekea kisiasa. Itakua mara ya kwanza kwa upinzani kuwa na sherehe yao mbadala kwenye sikukuu ya kitaifa. Yaani, Kenya itakua nchi ya kwanza kuwa na kitu kama hiki. Sina uhakika kama serikali itaruhusu, na wakizuia kwa kujaza polisi, wategemee umati wa warusha mawe kutoka kitaa.

Te te te!! Yaani wanasiasa wameamua liwalo na liwe, wataburuzana hadi kwenye matope hata kama ni kuharibu nchi, yote sawa. Mmoja anamwaga unga, mwenzie anamwaga mboga (msemo wa Kibongo). Tatizo ni pale bomu la machozi likitupwa la kwanza, wanasiasa wote wanaingia kwenye magari yao makubwa na kutoweka, halafu wanakwenda sehemu kutazama kwenye runinga jinsi ngoma inachezwa, yaani jinsi wafuasi wao wanatembezwa kichapo.

Naomba Alshabaab wasije tumia hii fursa kutulambisha vumbi, maana hapa naona hatari.
 
Back
Top Bottom