Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,088
Waziri wa Mambo za nchi za nje wa Zambia Harry Kalaba amejiuzulu rasmi nafasi yake ya uwaziri kupitia Facebook katika hatua ya kupinga mpango wa Rais wa Zambia Edgar Lungu kugombea urais kwa Mara ya tatu. Katiba ya Zambia inamruhusu kiongozi kuwa Rais kwa kipindi viwili. Ofisi ya Rais wa Zambia imedai mpaka sasa haijapokea rasmi barua ya kujiuzulu Waziri Harry Kalaba.
Mr Kalaba mbunge kutoka chama cha Patriotic Front alionekana kama mrithi wa Rais Lungu pindi kipindi chake kitakapoisha mwaka 2021.
Je huu ndio mwedelezo wa viongozi wa kiafrika waliopo madarakani kukataa kuondoka madarakani pindi kipindi chao kinapoisha kwa mujibu wa katiba. Rais Museveni wa Uganda ameshasaini mabadiliko ya katiba ili agombee nafasi ya urais kwa mara nyingine pindi muhala wa urais wake kwisha. Rais Museveni ametawala Uganda kwa muda wa miaka 31.
source: BBC