Mgogoro kati ya Armenia na Azerbaijan

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,080
Mgogoro huu inasemekana ni wa muda wa karibu miongo minne.

Lakini ulikuja kuwa mkubwa sana baada ya nchi hizi mbili kupata uhuru wao kamili miaka ya 1990 na kuendelea.
Inasemakana Russia inawaunga mkono Armenia huku Uturuki ikiwaunga mkono Azerbaijan.

Leo kumetokea kurushiana risasi, ndege kuangusha vifaru kulipuliwa mpakani mwa nchi mbili huku kisa cha haya ikiwa ni sehemu ya Nagorno-Karabakh inayogombaniwa na nchi hizi. Eneo hili linakaliwa na Warmenia wengi.

Fuatilia mgogoro huu kwa karibu kupitia vyombo mbali mbali vya ulimwengu.
Mimi nimeanza na chombo hiki hapa chini cha habari.

1601211967661.png



‘Azerbaijan is not alone’: Ankara throws weight behind Baku as fighting rages on over disputed Nagorno-Karabakh region

Hostilities break out between Armenia & Azerbaijan over long disputed Nagorno-Karabakh region, both countries trade blame

----- UPDATE-----

28/09/2020: Mapigano ya Armenia na Azerbaijan yaua 59

Mapigano makali zaidi kutokea katika kipindi kirefu, kati ya Armenia na taifa jirani la Azerbaijan yameendelea ambapo leo hii yameingia siku yake ya pili kwa kufyatuliana makombora.

Mapigano makali zaidi kutokea katika kipindi kirefu, kati ya Armenia na taifa jirani la Azerbaijan yameendelea ambapo leo hii yameingia siku yake ya pili kwa kufyatuliana makombora.

Mapigano hayo ya sasa ambayo yamesababishwa na mzozo wa jimbo la Nagormo-Karabakh kwa leo yanatajwa kugarimu maisha ya wanaotaka kujitenga 28.

Eneo hilo la Nagormo-Karabakh, ambalo kimataifa linatambuliwa kama sehemu ya Waislamu wa Azerbaijan, limekuwa likidhibitiwa na kundi la waliojitenga la Waarmenia kwa miongo kadhaa, huku kukiwa na makuabiliano tete ya amani tangu miaka ya 90.

Jeshi la Azerbaijan limedai kufanikiwa kuyakomboa maeneo kadhaa ya kimkakati ya milima ya Nagorno-Karabakh.

Aidha limeongeza wapiganaji wa wanaotaka kujitenga 28 wameuawa katika mapigano ambayo yametokea leo na kufanya idadi jumla ya waliuwawa kufikia watu 59. Viongozi wa mataifa kadhaa wamezitaka nchi hizo kuacha mapigano, baada ya mengine mabaya zaidi kutokea 2016 ambayo yanaashiria vita vipya kati ya mataifa hayo ambayo yalikuwa sehemu ya uliokuwa Umoja wa Kisovieti.

Mataifa hayo yamekuwa katika mkwamo wa mgogoro wa kimipaka, tangu kipindi hicho cha miaka ya 90, pale ambapo Karabakh ilipojitangazia uhuru wake, baada ya vita ambayo iligharimu maisha ya watu 30,000.

Hata hivyo hakuna hata taifa moja ambalo liliutambua Uhuru wa Karabakh. Lakini hadi sasa Azerbaijan haijatoa taarifa za vifo vilivyotokea kwa upande wa jeshi lake, tangu kuzuka kwa mapigano haya ya sasa.

Ufaransa, Urusi na Marekani zilishiriki jitihada za upatanishi kwa kile kilichofahamika kama "Kundi la Minsk" lakini jitihada kubwa kabisa ya mwisho ilivunjika 2010.

Wakati huo huo Rais Racept Tayyip Erdogan wa Uturuki ameitaka Armenia kuliachia eneo la la Nagorny Karabakh baada ya kuzuka kwa mapigano hayo, katika eneo la mpakani la Azerbaijan.

Amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP akisema "Umewadia muda kuufikisha kikomo mgogoro huo ambao ulitokana na ukaliaji wa Nagorny Karabakh, na kwamba Armenia ikiondoka tu, mgogoro huo utakuwa umekwisha."

Uhispania nayo haijakuwa nyuma katika mzozo huo, ambapo waziri wake wa masuala ya kigeni Arancha Gonzalez alionesha kusikitishwa na hayo yanayotokea na kutoa wito wa kusitishwa mapigano wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
 
Leo nilikuwa nachek video Armenian ilirusha makombora mawili Azabaijan nayo ikajibu mapigo baada ya hapo armenia ikasogeza vifaru karibu na mpaka wa Azarbaijan. Azarbaijan nayo ikarusha ndege mbili mapigano yakaaanza mpaka mapigano yanaisha vifaru vitatu na magari ya jeshi la Armenia yarihaibiwa na helcopter tatu na drone nne za Azarbaijan zilishushwa
 
Nimefatilia huu mtanange twitter comment za watu waliopo battle ground inaonekana Azerbaijan katandikwa haswa na kingine inaonekana Armenia ndio mkorofi
Leo nilikuwa nachek video armenian ilirusha makombora mawili azabaijan nayo ikajibu mapigo baada ya hapo armenia ikasogeza vifaru karibu na mpaka wa azarbaijan .azarbaijan nayo ikarusha ndege mbili mapigano yakaaanza mpaka mapugano yanaisha vifaru vitatu na magari ya jeshi la armenia yarihaibiwa na helcopter tatu na drone nne za azarbaijan zilishushwa
 
Wote wamepata hasara mpaka sasa

#Azerbaijan: Azerbaijan Ministry of Defense: 32 Armenian soldiers were killed in border clashes.
 
kiufupi Azerbaijan kapigwa haswa that why anafanya propaganda za kijinga kuficha aibu
Leo kwenye taarifa ya DW ya 7:00 nimeisikia habari juu ya huu mzozo kwa mujibu wa taarifa hii inaoneka Armenia ndio iliyo poteza zaidi.
 
Leo kwenye taarifa ya DW ya 7:00 nimeisikia habari juu ya huu mzozo kwa mujibu wa taarifa hii inaoneka Armenia ndio iliyo poteza zaidi.
That why nasema Azerbaijan kawekeza nguvu zaidi kwenye propaganda, Fatilia twiti za watu uone jinsi wanavyoandika Azerbaijan kapigwa
 
That why nasema Azerbaijan kawekeza nguvu zaidi kwenye propaganda,Fatilia twiti za watu uone jinsi wanavyoandika Azerbaijan kapigwa
Mm sijasikiliza propaganda mkuu bali nimesikiliza hii habari kutoka kwenye shirika kubwa na lakuaminika la habari ulimwenguni hata sasa hivi nimetoka kusikiliza habari yao ya saa 12:00 Azebaijan imeyateka baadhi ya maeeneo ya kimukakati ya jimbo linalo leta mzozo.
 
Hizi zote zilikuwa makoloni ya russia. (urusi ya zamani). Hao ni ndugu tofauti ni tamaduni labda na lugha. Huu mgogoro wa kuumaliza ni russia peke yake. Maana wakizidi kwa jinsi navyojua siasa za ukanda huo, russia hachelewi kuzikalia na kuanza kuweka vibaraka wake . Wataanza kuongoza nchi kwa maagizo toka moscow
 
Back
Top Bottom