Mgogoro mkubwa wazuka CCM Arusha mjini kisa ni Lowassa............................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro mkubwa wazuka CCM Arusha mjini kisa ni Lowassa.............................

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 18, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,617
  Likes Received: 38,934
  Trophy Points: 280
  Katika hali inayoonyesha "La kuvunda halikosi ubani" wana-CCM Arusha wameparanganyika katika makundi matatu makubwa kutokana na kuchukizwa na asiyekuwa mwanajimbo la Arusha mjini, Mheshimiwa Lowassa kuwachagulia mbunge wao.

  Wanaokereketwa na sakata hili na ambao ni wengi wanalia Dr. Batilda ni mradi wa "Saidia Lowassa ashinde URAISI 2015" na kwa hiyo hauna tija na mahitaji ya uongozi wa jimbo hili kwa sasa.

  Kundi dogo na la pili ambalo ndilo linalomuunga mkono Dr. Batilda ladai tofauti zizikwe kwa minajili ya kuliokoa jimbo lisinyakuliwe na Chadema.

  Kundi la tatu lataka Chadema wachukue ubunge kama suluhisho la kuvunja makundi ili wana-CCM angalau waweze kuokoa kura za JK ambazo zinazidi kuyeyuka siku hata siku. Kundi hili linadai bila ya kuliachia jimbo la Arusha na kuwa na tamaa ya mzee fisi basi watapoteza yote ubunge na kura za JK kutokana na mgawanyiko mkubwa ndani ya Chama jimboni ambao waweza kukisambaratisha chama hapa Arusha.

  Mgawanyiko huu ambao siyo wa ki-itikadi bali ni taswira ya mgombea ubunge tu unaashiria CCM itaangukia pua safari hii hapa Arusha mjini kwenye nafasi zote za ubunge na uraisi lakini wataponea kwenye udiwani hivi...
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,057
  Likes Received: 883
  Trophy Points: 280
  na waparanganyike tu ..hili dubwana CCM life
   
 3. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mie masai bana sitaki mcheso mwaka hii. Kura kwa ile Dr. Saa maana ina maneno masuli sana iko hapana penda fisadi. Hayo si maneno yangu bali ya mmasai mmoja niliyeongea naye hapa arusha.

  Wanamtaka Dr. Slaa basi. Sishangai CCM kupoteza kiti cha ubunge na dalili zote zipo hilo halina ubishi kwa mtu yoyote aliyeko hapa Arusha
   
 4. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 5,579
  Likes Received: 2,154
  Trophy Points: 280
  Ila cha ajabu mtakuja sikia huyo wa CCM kashinda kwa kishindo..
  Maana jamaa wanajua kucheza rafu ka De Jong.
   
Loading...