Mgogoro mkubwa Tanga Cement (Simba Cement)

Second July

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
234
323
Sintofahamika imejitokeza jioni ya leo ndani ya Tanga Cement (Simba Cement) baada ya Katibu wa chama cha wafanyakazi (TUICO) bwana Lawrence Malale kufukuzwa kazi bila sababu za msingi.

Sakata hili limetokana na Bwana Malale kuongea kauli ambayo ilitafsiriwa vibaya na management ya Kikaburu. Kauli hii aliitoa katika kikao cha wafanyakazi na management cha kudai nyongeza ya mshahara kwa asilimia 10 (10%).

Maamuzi haya ya kibabe na kiunevu ni kutaka kuvunja nguvu na kuwanyamazisha wafanyakaz na uongozi wa chama cha wafanyakazi katika kudai mahitaj yao mengi kubwa ikiwa ni nyongeza ya msharaha kwa mwaka huu wa 2016. Ikumbukwe kuwa mpaka sasa ni mwezi wa tatu ss uongozi huu wa kikaburu umegoma kuongeza mshahara kwa 10% ikitaka kuongeza kwa asilimia 6.8% (Inflation Rate for the month of December, 2015). Tayari management ya Tanga Cement imeanzisha tabia ya kufukuza fukuza wafanyakazi kwa vijikosa vidogo visivyo leta tija kwenye kampuni.

Suala hili halikubaliki na linazorotesha kasi ya serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Serikali inaombwa kuingilia kati mgogoro huu nakuifuatilia vizuri miendendo ya kampuni hii, hali sio nzuri kwa sasa. Makaburu sio watu wa kucheka nao.
 
Serikali ingilie kati mgogoro huu kabla haujafika pabaya.

Panapofuka moshi kuna moto.
 
Kampuni ikishakuwa na uongozi wa makaburu inakuwa na shida. Mara nyingi wanataka walete watu wao kutoka SA kufanya kazi za wazawa. Huko kwao migogoro ni
Kitu cha kawaida. Kwa ujinga na kwa kutotumia akili watanzania wana wambia wazawa viongozi watengeneze kesi za kufukuza watu. Kwao ni Capitalism type of economy kwa hiyo waupe wanaamua kila kitu. Na ukiingia kwenye shamba la whites anakushoot kama nyani.
Hivi kweli mtu kuhoji kitu kwenye mkutano uloitishwa na Management ni kosa? Hapo kuna kitu lazima wafanyakazi mjitahidi hilo kosa la kufuta mtu kazi lisitokee. Waziri wa viwanda na kazi wahusishwe kabla ya matatizo hayajawa makubwa.
Mkijindanganya Dangote atachukua masoko yenu nyie mkiendelea na migogoro.
 
Management hii ya kikaburu iliyopo pale ni ya hovyo sana. Nilikaa mda mfupi pale nikaondoka, ile management ya kikaburu itaharibu ile kampuni. Huwez ukamfukuza Katibu wa chama cha wafanyakazi kwa kosa la kuongea tena maneno sio mabaya kiasi hicho katika mkutano wa madai ya wafanyakazi uliotishwa na management yenyewe. Tatizo kubwa pale ss hv ni kuwa wafanyakazi wanataka nyongeza ya 10%, kampuni haitak inataka iwape 6.8%. Kaburu kwny hili la kufukuza katibu wa TUICO kiwandani pale kachemsha.

Serikali ilione hili kwakwel.
 
Mbona kwenye Uzi
umesema 6.8% alafu hapa tena unasema 6.5% ebu sema katibu alihoji nini mpaka kufka hatua hiyo? Je maneno yake yalikuwa Nje ya agenda? Fafanua maana inaonesha we ni sehemu ya wahanga
 
Mbona kwenye Uzi
umesema 6.8% alafu hapa tena unasema 6.5% ebu sema katibu alihoji nini mpaka kufka hatua hiyo? Je maneno yake yalikuwa Nje ya agenda? Fafanua maana inaonesha we ni sehemu ya wahanga.

Ni 6.8% mkuu, hy 6.5% ni typing error. Nimeshabadilisha.
 
Mbona kwenye Uzi
umesema 6.8% alafu hapa tena unasema 6.5% ebu sema katibu alihoji nini mpaka kufka hatua hiyo? Je maneno yake yalikuwa Nje ya agenda? Fafanua maana inaonesha we ni sehemu ya wahanga.

Mm sio mhanga mkuu, I am no longer working there.
Jamaa zangu wa karibu sana bado wanafanya kazi pale.
Katika kuhoji, huyo katibu alimwambia mmoja wa mabosi wa pale "nakushangaa unajisifu kuzalisha kitu kibovu", hapo ni baada ya huyo bosi kusema "mwaka jana tumezalisha vitu vibovu"

{NB: Hii kitu kibovu sio cement lakin mkuu, ni moja ya vitu vinavyozalishwa pale, wataalam wa cement wanajua vzr.}
 
Hatujajua kafukuzwa kwa sababu gani ? hapo ndio tunaweza kutoa rai. Sidhani mtu atafukuzwa kwa kuomba nyongeza tu.
 
Hatujajua kafukuzwa kwa sababu gani ? hapo ndio tunaweza kutoa rai. Sidhani mtu atafukuzwa kwa kuomba nyongeza tu.

Mkuu ni hivi, katika kikao kati ya wafanyakazi na management kujadiliana mambo ya nyongeza ya mishahara, katibu huyo wa chama cha wafanyakazi alimwambia mmoja wa mabosi wa pale "nakushangaa unajisifu kuzalisha kitu kibovu", hapo ni baada ya huyo bosi kusema "mwaka jana tumezalisha vitu vibovu".

Kosa lake hapo wanasema ametumia lugha mbaya kumdhalilisha huyo bosi wao. Kesi hiyo ndio imemfukizisha kazi leo. Maajabu haya.
 
Back
Top Bottom