Mgogoro kati wa maisha (midlife crisis)

Mgogoro kati wa maisha (midlife crisis)

moto2012

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
2,309
Reaction score
1,552
Wapendwa wana MMU wenzangua. Ni jioni nyingine tena napenda kuwashiriksha juu hili tatizo la Mgogoro kati wa maisha ambao huwakumba watu wengi walio katika kipindi cha mpito yaani kuhama kutoka ujana na kuingia utu uzima. Aghalabu katika kipindi hiki ndoa/mahusiano mengi huvunjika na pia kuna matumizi mabaya ya rasili mali mfano unuzi wa magari (Verosa, altezza, Benzi, BMW n,k) au mavazi ya thamani ambayo kimsingi hatuwezi kuyaendesha, na pengine baadhi ya watu huacha kazi bila sababu za msingi. Naomba tutafkari mada hii

Midlife crisis (Mgogoro Kati wa Maisha) ni nini?
Ni kipindi katika maisha ambapo mhusika anafanya vitu vya aibu ambavyo wakati mwingine havina sababu za msingi wala uhalisia. Kwa mfano mtu anaweza kuacha kazi pasi na kujipanga, kununua gari zuri la kimichezo(wakati hashiriki) au fahari/gharama kubwa, au kumwacha/kumtupa mwenzi. Aghalabu tatizo hili limekuwa kubwa kwa kizazi hiki.

Matumizi ya msamiati crisis hauendani na maoni ya watalaam wa masuala ya Kisaikolojia kwa sababu ingawaje tatizo hili linaweza kuambatana na matatizo makubwa ya msongo wa mawazo(Depression) lakini kipindi hiki kinaweza kikawa ni alama ya wakati wa ukuaji mkubwa wa akili/maisha ya mhusika aliyepo katika midlife crisis

o-SOMEONE-UPSET-ON-SCALE-570.jpg
Umri wa Midlife Crisis kutokea
Umri wa tatizo/kipindi cha midlife crisis kutokea unatofautiana kutokana na utamaduni na pia umri ambao watu wa jamii hiyo wanatarajia kuish. Ila kwa ujumla ni kati ya miaka 37-50. Lakini zipo tafiti zinaonesha tatizo hili siku hizi kuanza katika umri wa chini Zaidi kati ya miaka 20-30 kutokana na kuenea kwa mfumo wa kimagharibi. (Kumaliza shule/chuo na kuanza kazi katika umri mdogo na kupungua kwa life expectancy)
Na huathiri kati ya 10-15% ya watu walio kati ya umri wa miaka 40-60 (Life begins at 40?)
Mara nyingi Mgogoro kati wa maisha hutokea kuambatana na matukio makubwa/muhimu ya maisha ya mhusika. Mfano kifo/vifo vya wazazi au watu muhimu kwa maisha yetu, kuingia katika muongo mpya, kuzaa watoto, watoto kuanza au kumaliza shule n.ko-HAPPY-FAMILY-WITH-TEENAGERS-570.jpgAthari za Midlife crisis kwa wanaume na wanawake
Wanaume na wanawake wanaweza kutokewa na tatizo hili kwa usawa, ila athari zake hutofautiana kidogo baina ya jinsia hizi mbili. Athari za tatizo hili zinaweza kuwakumba wanawake katika kipindi cha miaka 3-5, ilihali kwa wanaume ni kati ya miaka 3-10.
Kwa wanaume mara nyingi hupendelea kununua magari ya kifahari/kimichezo. Pia tafiti zinaonesha wanaume huwa wanakuwa na lengo la kuthibitisha jambo fulani katika jamii, aidha kwa kupima utendaji wao kikazi au vipato vyao
Lakini wanawake hupenda kujipima kupitia mahusiano yao katika jamii kama vile kuolewa au kuwa na watoto.

Mgogoro kati wa maisha ni hatua muhimu katika maisha

Mwanasaikolojia Daniel Levinson anaichukulia nadharia hii kama ni hatua ya ukuaji/ustawi wa utu uzima, na utu uzima hupitia hatua tofauti tofauti.
Katika wakati huu kwa watu wengi muundo wa maisha unahusisha famila na kazi, lakini pia inaweza kuhusisha masuala ya dini au hali ya kiuchumi.
Tatizo hili linahusianishwa sana na vijana wanaoanza kazi katika umri mdogo, na takwimu zinaonesha wastani wa umri wa wakuu wa idara/maofisa waandamizi umeshuka kutoka miaka 59 hadi miaka 48.
Kadiri watu umri unavyowatupa mkono, wanaingiwa na mashaka juu ya mwonekano wao na wanatamani kurudia ujana wao. Haishangazi wahusika kufanya mabadiliko makubwa juu ya mwonekano wao kadiri umri unavyozidi kuwatupa mkono.
Wanaume haishangazi kuingia gharama kubwa kupandikiza nywele kwenye vipara vyao, wanahofia kupoteza kazi zao wakidhani mwonekano wao wa ujana utawafanya waonekane nadhifu sio tu kwa watu wa jinsia tofauti bali kwa waajiri wao pia.
Dalili za Mgogoro Kati wa Maisha
  1. Kuacha/kuogopa kuwaambia watu umri wako
  2. Kuogopa kijana mdogo kuchukua kazi/nafasi yakoo-JEALOUS-OF-YOUNGER-570.jpg
  3. Kujiunga na mitandao ya kijamii/kununua simu ya kisasa/i-pad ili wakuu/mwajiri wako akufikirie kuwa nawe umekuwa wa kidigitali zaidi.
  4. Kuanza kuwatafuta marafiki/wapenzi wako wa zamani katika mitandao ya kijamii kama facebook na twitter
  5. Kuziogopa simu unazopigiwa na wazazi wako/ndugu zako katika muda usiotarajiwa (Kuogopa taarifa mbaya)
  6. Kuwa na mazoea ya kutumiana/kuchati sms za kimapenzi na watu walio na umri mdogo miaka 20 zaidi yakor-MIDLIFE-CRISIS-large570.jpg
  7. Kufikiria kuifanya dunia kuwa mahali bora kwa vizazi vijavyo-kuanza kufikiria kuwekeza
  8. Kuhudhuria matamasha ya bendi za miziki ya zilipendwa za miaka ya 70 na 80 na Kubadilisha station za redio mara kwa mara kutafuta miziki unayoipenda
  9. Kupenda kulinganisha mwonekano wako na watu wengine wa umri wako
  10. Mara zote kupenda kuchunguza na kujiridhisha kuwa mwanasiasa au mfanyabiashara maarufu anaumri mdogo Zaidi yako
  11. Kufikiria kwenda kanisani/msikitini lakini kamwe huwezi kutekeleza
  12. Mara kwa mara kulinganisha mafanikio ya taaluma/kazi yako na ya rafiki zako.
  13. Kuziogopa nywele zako nyembamba/ Kuanza kupaka piko nywele zako zinazoanza kuwa na mvi
  14. Kusoma Makala za magazeti kwa shauku kubwa ya kutaka kujua watu wanavyokufa
  15. Kukumbuka na kuzungumzia zaidi juu ya maisha yako ya utoto na kuziangalia picha zako zau utoto kwa muda mrefu na pengine kuzipost facebook
  16. Hangover zinazidi na huisha kwa Zaidi ya sikumoja

Matibabuna kuzuia


Inatumia muda na rasilimali nying kutibu tatizo hili. Madililko ya mfumo wa maisha ni jambo muhimu kuzingatia na ulaji unaofaaIMG-20140214-WA0005.jpg

Kufanya mazoezi ya viungo/mwili
Exercise.jpegKuwa na rafiki unayemwamini kumshirikiaha shida/maoni na mitazamo yako.

thumb.pngKujifanyia tathimini yenye uhalisia juu ya malengo yako, kupambana nachangamoto za maisha na sio kuziogopa.

Kufanya madiliko ya maisha/kazi mapema –tafiti zinaonesha kuwawaliobadilisha kazi mapema katika maisha yao wamekuwa na mafanikio makubwa.
youngman 2.jpeg
Chukulia kipindi hiki kama ni cha mpito kuelekea mafanikio. Inafaida kubwakuukubali uzee mapema.

Maandalizi ya kiakili yatasaidia kukabiliana na hali hii

Nawatakieni jioni njema
CC Mtambuzi, Bujibuji, Boflo, lara1, The Boss, AshaDii
 
Kwa kweli sina cha kuongeza
Ahsante kwa useful thread.
Ubarikiwe mkuu
 
Kaunga aliwahi weka thread hapa Zamani...thanks kwa kuleta. Tena
 
Last edited by a moderator:
Wanasema asilimia kubwa ya divorce inatokea kipindi hiki mwanaume anapitia midlife crisis
 
Nimesoma nikachoka mpaka kichwa kikajibu...loading error......
 
Wanasema asilimia kubwa ya divorce inatokea kipindi hiki mwanaume anapitia midlife crisis
Sio wanaume pekee,hata wanawwke hupitia kipindi hiki. Tabia zao huwa hazieleweki na hivyo kuachika kirahisi.
 
Kaunga aliwahi weka thread hapa Zamani...thanks kwa kuleta. Tena
Hata wewe iliweka thread inayomhusu mzee Mengi mwaka 2009 kwa theory ya second midlife crisis
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hizo nyingi( labda kasoro (3,4 na 6). Naona its normal way of life kulingana na umri na its not CRISIS in mid years of life.. naona ni mabadiliko ambayo yanatokea psychologicaly kutokana na umri unavyoenda.. Mid life crisis mara nyingi inatokea kukiwa na mvutano unatokana na umri kwenda na kutokubali matokeo kisaikolojia(mind).. Mfano mtu ana miaka 40 lakini bado anataka kuangaika kuvaa mlegezo mind inakataa umri..3 ,4 na 6
 
Back
Top Bottom