mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,310
- 6,546
KUNA tajiri alihitaji kununua nyumba ya urithi ya watu ambao walifiwa na wazazi wao. Alichokifanya aliamua kuwagombanisha kwa kutumia rimoti. Watoto wa marehemu wakawa wanavutana na kupigana.
Kuna wakati wale watoto wakawa wanataka kuelewana, tajiri akatumia tena rimoti yake kuzidi kuwagombanisha. Alipohakikisha hawaelewani, akapenyeza habari kuwa nyumba inataka kuuzwa ili wazungukane.
Wenye nyumba ya urithi walipokutana nyumbani wakanyoosheana kidole, mmoja akasema “ninazo taarifa zote kuwa unataka kuuza nyumba ili unizunguke, kwa taarifa yako mtandao wangu ni mkali huwezi kunizunguka hata siku moja.”
Mwenzake naye akajibu “mimi pia najua kila kitu kuhusu madalali wako ambao unawaleta hapa kutaka kuuza nyumba. Huna ujanja wa kunizunguka mimi, na ukithubutu kuuza hii nyumba tunauana.”
Waliendelea kugombana mwisho wakaamua bora nyumba iuzwe kila mtu abaki na chake. Uamuzi huo ulipofikiwa, yule tajiri aliwaita na kuwaweka chini, akawaambia yeye yupo tayari kununua nyumba yao ili wagawane fedha sawa na kubaki na amani.
Kwa vile maelewano yao yalikuwa madogo, walijikuta wanauza nyumba yao kwa bei chee. Mwisho tajiri akawa amefanikiwa azma yake, maana shida yake yeye ilikuwa ile nyumba tu.
Watoto wa marehemu baada ya kuwa hawana nyumba na kuchezea fedha, wakajikuta wanapata akili na kuzungumza, wakagundua kuwa kumbe tajiri ndiye alikuwa anawagombanisha. Wakati huo tayari walishachelewa.
Walikuwa na nyumba eneo zuri na walikuwa na nafasi ya kutengeneza fedha lakini baada ya kukubali kuchezewa akili na tajiri aliyetamani nyumba yao, nao walikubali kugombana, hawakutaka hata kujipa nafasi ya kuzungumza.
Rimoti inafanya kazi pia kwenye Chama cha Wananchi (Cuf), ukifuatilia mgogoro wao unaona kabisa hawagombani wenyewe, isipokuwa kuna nguvu ya nje ambayo inawachonganisha. Badala ya kutafuta nafasi wazungumze ili wapate suluhu, kila upande unadai unazungukwa.
Kinachotokea sasa hivi Cuf hakina tofauti na kile kichowapasua watoto wa marehemu kwenye nyumba yao ya urithi. Cuf hawagombani wenyewe, isipokuwa ipo nguvu ya nje inayowafanya washindwe kukaa pamoja. Kila upande umeaminishwa hasi, kwa hiyo vita ni kubwa.
Kichekesho tu ni kwamba Cuf viongozi wake ni wakubwa. Watu wazima, wazoefu wa siasa, wasomi na sifa nyingi kemkemu. Ajabu wanashindwa kuelewana. Ukiwatazama wao kwa wao hawana suala linalowagombanisha, isipokuwa lipo la nje.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na timu yake, wameaminishwa kuwa aliyekuwa mwenyekiti wao, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na wanaomuunga mkono wanatumiwa na Chama Cha Mapunduzi (CCM) ili kuibomoa Cuf.
Upande wa Lipumba, wanaamini kuwa Seif na watu wake wamerubuniwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyepewa pia baraka za muungano wa vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Ngoyai Lowassa.
Hoja za watu wa Seif ni kwamba Lipumba anatumika kudhoofisha upinzani, kwamba anataka akirejea kwenye chama kama mwenyekiti, asitishe hatua ambazo Ukawa wameshapiga na ikiwezekana kuiondoa Cuf kwenye Ukawa.
Kinachojengewa hoja upande wa Lipumba ni kuwa hivi sasa Cuf siyo chama chenye kujitegemea bali kimekuwa rimoti ya Lowassa na Chadema. Kwamba sauti za Lowassa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, zina nguvu kuliko za viongozi wa chama.
Sasa je, watu ambao wanagombanishwa na sauti za nje, kwamba wao wenyewe hawana hasa kitu cha msingi kinachowachonganisha isipokuwa vichwa vyao vinagonganishwa na rimoti ambazo walionishika wapo, na wao wenyewe wanajua, hicho siyo kichekesho?
Ucheshi wa Cuf ni kuwa wanagombanishwa na uchaguzi. Wao wenyewe ni kichekesho kwa maana wanakubali kugombana kwa maslahi ya wengine. Kinachotesa mbavu kwa kucheka ni jinsi ambavyo wenyewe wasivyotaka kitu kinaichoitwa mazungumzo.
Ikachekesha kusikia kuwa baadhi ya vijana wa Chadema ndiyo waliokwenda Ubungo Plaza kulinda mkutano. Kwamba Chadema kimetoka kuwa chama shirika na Cuf kwenye Ukawa, hadi kuwa chama kinachokilinda Cuf.
Lipumba anasema kuwa akishafanikiwa kurejea kwenye kiti chake, mwaka 2020 Cuf kitasimamisha mgombea urais na kwamba chama chake hakitamuunga mkono Lowassa kutokana na makandokando yake.
Mgogoro wa Cuf ni uchaguzi tu, kama ambavyo mwaka 2015 suala lilikuwa kumuunga mkono Lowassa au kutokumuunga kisha wenye kumuunga wakashinda mpaka kusababisha Lipumba ajiuzulu, ndivyo na sasa jicho la 2020 linatengeneza mgogoro.
Lipumba anashutumiwa kuwa amekula fedha za CCM ndiyo maana anataka kukivuruga Cuf, wakati shutuma zinazoelekezwa kwa Seif ni kuwa wamehongwa fedha na Lowassa ili kumuunga mkono kuanzia Uchaguzi Mkuu 2015 mpaka 2020. Nani ana ushahidi? Ni kwamba kinachotokea hakina tofauti na kilichowagombanisha watoto wa marehemu kwenye nyumba ya urithi.
Ucheshi mkubwa zaidi ni kuwa mgogoro wa Cuf umesababisha chuki kubwa ya upinzani iibuke, wakati kabla ya vuguvugu la Lipumba kutaka kurejea kwenye kiti alichokiacha Agosti mwaka jana, tayari kulikuwa na asilimia kubwa ya maelewano kwa wapinzani, sasa hakuna.
Tayari Ukawa walishakiona Chama cha ACT-Wazalendo kama chama rafiki ambacho wanaweza kushirikiana nacho. Mbowe ambaye pia ndiye Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alishatamka wazi kuwa katika mapambano ya kuupinga udikteta nchini (Ukuta), watashirikiana na ACT-Wazalendo.
Baada ya mgogoro kuibuka, hali ya kutoaminiana kati ya Ukawa na ACT-Wazalendo imeibuka tena. Upande wa Seif wanatoa shutuma kuwa ACT-Wazalendo pia kipo kwenye sehemu ya harakati za Lipumba.
Wakati huohuo, ACT-Wazalendo, wameonekana kuwashambulia akina Seif kuwa si watu wa demokrasia na kwamba walichokifanya kufukuza baadhi ya watu uanachama na kuwasimamisha akina Lipumba ni usiginwaji wa demokrasia.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo ambaye pia ni mshauri wa chama hicho, Prof Kitila Mkumbo, alisema waziwazi, akikosoa jinsi ambavyo mgogoro wa Cuf unaendeshwa kwa kile alichokiita ni cha kimabavu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Cuf, Julius Mtatiro alimjibu Prof Kitila kuwa anajua kila kitu kuhusu mazungumzo ya Lipumba na ACT-Wazalendo. Hata hivyo, Mtatiro hakusema ni nini hasa ambacho kinahusu mazungumzo hayo.
Kinachoonekana ni kuwa ACT-Wazalendo kinaweza kunufaika na mgogoro wa Cuf kama utaendelea kama ulivyo, kwani inadhaniwa kuwa Lipumba na timu yake wakikosa kabisa jinsi ya kupenya watakwenda kujiunga na chama hicho.
Kinachooonekana pia ni kuwa Chadema wananufaika vizuri mno na mgogoro wa Cuf, maana kinazidi kuwaimarisha na kukibakisha kuwa chama kilicho juu, kikiongoza vyama vingine vya upinzani, pamoja na Cuf pia kipo NCCR-Mageuzi na NLD.
Lowassa ananufaika mno na mgogoro huo kwa sababu mafanikio ya kumuondoa Lipumba Cuf, yatakuwa na maana kubwa kwamba mwaka 2020 atakuwa na uungwaji mkono usiotetereka Zanzibar, maana Cuf ni chama chenye nguvu karibu sawa na CCM.
Hata hivyo, jicho la kweli la kichambuzi, linaona kuwa mnufaika wa kweli wa mgogoro wa Cuf ni CCM na upinzani kwa umoja wao, nguvu inapungua na imani ya wananchi kwao inapungua.
Utulivu wa Cuf ulikuwa na msukosuko mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na CCM yake. Jinsi ambavyo Cuf wenyewe wanaparurana, sasa inampa Shein ahueni. Sasa hivi anamfikiria Seif kama mpinzani wake asiye na nguvu, anatetereshwa ndani ya chama chake.
Tumia darubini za kila aina, hutaona chanzo cha Cuf wao kwa wao kutofautiana, kinachowagombanisha ni nguvu ya nje, na kwa sababu wanashindwa kukaa wazungumze wayamalize ni kuwaacha waendelee kutuchekesha kama wale watoto wa marehemu na nyumba yao ya urithi.
Unamfukuza Magdalena Sakaya, Habib Mnyaa! Hiki ni kichekesho kikubwa sana, siku Cuf wenyewe wakijishtukia wanavyochekesha, hata wao wenyewe watajicheka.
Chanzo: Luqman Maloto