Mgodi wa Buhemba Wawafunika wachimbaji. Majeruhi 11 mpaka sasa

srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,148
3,861
Habari wadau. Kwa habari za hivi punde ni kwamba mgodi mwingine huko wafukia watu na mpaka sasa kuna majeruhi kumi na moja na wamefikishwa hospital ya Butiama.

Habari hii nimeinyaka kutoka kwa Mr Informer wa clouds FM..

Watu wahofiwa kufa kwani mgodi huo huingiza watu kama 200..

Mwenye taarifa zaidi tafadhali na picha.

Nawasilisha

====



HABARI zilizotufikia hivi punde zimeelza kuwa wachimbaji sita wa madini wanadaiwa kufukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba madini kwenye mgodi wa Buhemba ulioko mkoani Mara.

Imeelezwa pia kuwa watu 11 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo wamekimbizwa katika Hospitali ya Butiama kwa ajili ya matibabu.

Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi ambaye amekiri kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo, na hivi sasa nipo eneo la tukio. Kuhusu takwimu sahihi za watu waliofukiwa kwa sasa sina, mpaka uchunguzi wa jeshi la polisi utakapofanyika ndipo nitatoa ripoti kamili.” Alisema Kamanda Ng’anzi.

Tukio hilo ni la pili ndani ya kipindi kifupi ambapo siku za hivi karibuni, wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa baada ya siku kadhaa katika Mgodi wa RZ, Nyarugusu uliopo Nyarugusu mkoani Geita.
 
Habari wadau. Kwa habari za hivi punde ni kwamba mgodi mwingine huko wafukia watu na mpaka sasa kuna majeruhi kumi na moja na wamefikishwa hospital ya Butiama.

Habari hii nimeinyaka kutoka kwa Mr Informer wa clouds FM..

Watu wahofiwa kufa kwani mgodi huo huingiza watu kama 200..

Mwenye taarifa zaidi tafadhali na picha.

Nawasilisha
Mbona mgodi wa Buhemba ulishafungwa? taarifa zaidi mkuu.
 
Back
Top Bottom