Mgodi ambao mchimbaji alichomwa moto wafungwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,538
9,355
Mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Mererani, wilayani Simanjiro ambao mchimbaji wake, Joel Ephata(34) alinusurika kufa baada ya kuchomwa moto, umefungwa.

Akizungumza na waandishi wa leo Jumatatu, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma alisema mgodi huo wenye namba 003436 uliopo kitalu D Mererani, unamilikiwa na Fatuma Kikuyu.

Kamishna Juma alisema mgodi huo umefungwa kwa tuhuma za kukiuka haki za binadamu, baada ya meneja wa mgodi huo, Nickson Emmanuel kutuhumiwa kumchoma moto mchimbaji huyo kwa tuhuma za upotevu wa vifaa.

"Tanzania tumeridhia mkataba wa kimataifa wa haki za binaadamu maeneo ya migodini katika ukanda wa maziwa makuu(ICGR) hivyo tukio la kuchomwa moto mchimbaji huyu ni kuvunja sheria," alisema.

Alisema mgodi huo, utafunguliwa pale tu uchunguzi utakapokamilika na hatua kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria. "Tayari tumetoa taarifa kwa wamiliki wa mgodi na pia kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Manyara, lengo ni kuwataka wachimbaji wadogo kuzingatia sheria," alisema.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Fransis Masawe akizungumza na Mwananchi kuhusu tukio hilo alisema bado uchunguzi unaendelea. Tukio hilo, lilitokea Juni 25 mwaka huu, saa tatu usiku.


Chanzo
mwananchi
 
Iwe fundisho kwa wamiliki migodi.Yaani mirerani watu wanvunja sheria utadhani sio Tanzania.
 
Back
Top Bottom