Mgeja: Niko tayari kufukuzwa CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1]
[/h]

Na John Maduhu,Mwanza
Akizungumza na MTANZANIA Mjini Mwanza jana, Mgeja alisema ameshangazwa na taarifa zilizochapishwa na gazeti moja (siyo MTANZANIA), kuwa yeye na Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa wako hatarini kutimuliwa kutokana na kuwa karibu na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa.

Alisema kinachowaunganisha wana CCM ni itikadi bila kujali rangi, dini au ukabila na kusisitiza kuwa urafiki wa mtu binafsi siyo suala la chama.

“Suala la urafiki siyo suala la chama hata siku moja, hawa ni wanasiasa ucharwa jamani ambao wamekuwa wakipotosha umma kwa maslahi yao binafsi.

“Kila mwanachama ana haki sawa na mwanachama mwenzake, lakini nashangaa baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM wanapanga mikakati maalumu kwa ajili ya kuwashughurikia wenzao.

“Sina kosa la kimaadili ndani ya chama na sijawahi kuitwa katika kikao chochote kwa kuvunja maadili, siogopi kufukuzwa kama itatokea nimefanya kosa la kimaadili na usaliti ndani ya CCM, lakini sitokubali kuchaguliwa rafiki.

“Nina imani na Sekretarieti ya chama inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama na kamwe haitoweza kupokea ushauri wenye nia ya kukiangamiza chama chetu.

“Kwa hiyo, wana CCM mkoani Shinyanga, wapuuze maneno hayo na waendelee kuchapa kazi za kuimarisha chama chetu.

“Wasisikilize hizi porojo za vibaka wa kisiasa ambazo hazisaidii bali zimelenga kukichafua chama, hoja zao hazina mashiko yoyote, mimi niko imara siku zote na nitaendelea kupigania haki ndani ya chama”,alisema Mgeja kwa kujiamini.

aseee!!!
yeye na wenzake watachaguliwa rafiki, hata wafanye nini...........labda waondoke CCM
 
Hajui kama Lowassa Ni Gamba lililogoma Kuvuka likija kuvuka lenyewe au wakilivua kinguvu naye ataenda na maji... Mgeja umekaa kwenye tawi Bovu
 
Da aisee huyu mzee sijui lowassa alichompa kitu gani,yani anampenda lowassa mpaka watu wanaweza kumuhisi vibaya,maanake sio mapenzi ya kawaida aliyonayo kwa lowassa bali mahaba,nadhani kuna kitu ameahidiwa na lowassa!
 
Mbona wanatishia sana kujiuzuru chama kina watu wengi na wao siyo waanzilishi wake Wakiamua kujiuzuru wengi walijiuzu lakini chama kipo ngangari
 
sisi wataka mapinduzi tuna furahia kutoelewana kwenu kwani kunaturahisishia kazi.
adui ya yako mwombee njaa
 
Hajui kama Lowassa Ni Gamba lililogoma Kuvuka likija kuvuka lenyewe au wakilivua kinguvu naye ataenda na maji... Mgeja umekaa kwenye tawi Bovu

Teh teh teh teh! Kwa upande flani ni kuti bovu, ILA si inasadika kuwa huyo rafiki yake ni MTARAJIWA? Huenda Mgeja anatageti za kua KIRANJA MKUU 2015.. Teh teh teh, urafiki bhana.!
 
Ni mtoa mada (mwanzisha thread) au ni mwandishi wa habari ambaye hajaonyesha Mgeja ana cheo gani ktk CCM au taifa? Kuonyesha cheo cha Mgeja kungesaidia kuonyesha kwanini kuwa kwake tayari kufukuza ni "news" maana sio wote wanamfahamu.
 
Da aisee huyu mzee sijui lowassa alichompa kitu gani,yani anampenda lowassa mpaka watu wanaweza kumuhisi vibaya,maanake sio mapenzi ya kawaida aliyonayo kwa lowassa bali mahaba,nadhani kuna kitu ameahidiwa na lowassa!

Muulizeni Cameron. Anajua siri hii.
 
sisi wataka mapinduzi tuna furahia kutoelewana kwenu kwani kunaturahisishia kazi.
adui ya yako mwombee njaa
Sio njaa tu Mgeja anatajwa sana kufanikisha uchakachuzi wa mbunge wa ccm shinyanga dhidi ya ushindi wa wa cdm mwaka jana kama ni kweli dhambi inamrudia na bado.
 
Lowasa mjanja,anateka kanda ya ziwa,anajua huko ndo kwa kupatia ushindi
 
Hajui kama Lowassa Ni Gamba lililogoma Kuvuka likija kuvuka lenyewe au wakilivua kinguvu naye ataenda na maji... Mgeja umekaa kwenye tawi Bovu

Mkuu mimi nakukatalia. Mngeja (jina sahihi) anajua anachofanya. Sio kuti kavu, wanachofanya hawa magamba ni ile, jahazi lizame tugawane mbao.
Huyu jamaa anajua gravity ya EL kwenye hiyo sisiem yao, so pengine ameona hapo ndipo safe side kwake. Huwezi jua ameahidiwa nini na rafiki yake.

Mimi alichoniacha hoi ni pale alipotenganisha urafiki binafsi na maswala na political interests, how valid could this be.At least mmoja wapo asingekuwa mwanasiasa basi, hivi inawezekanaje huu urafiki kati ya mwizi na mtu asiye mwizi. Nijuavyo mimi siku zote marafiki wanashare common interests. Inawezekana na wao hawajakutana barabarani tu!

Mngeja bwana! Haya, sisi yetu macho tu.
 
Mbona wanatishia sana kujiuzuru chama kina watu wengi na wao siyo waanzilishi wake Wakiamua kujiuzuru wengi walijiuzu lakini chama kipo ngangari

Mnjeja ana impact gani kwenye chama hata wakimtimua(hicho anachoita kujiuzulu). Anatafuta sifa tu isiyokuwa na maana yoyote, hata yeye anajua hilo. Na akifukuzwa hapo, kwa huo urafiki wake na EL hatapata chama kingine kikubwa kitakachompokea, labda na nao waanzishe sisijei yao.
 
Mkuu mimi nakukatalia. Mngeja (jina sahihi) anajua anachofanya. Sio kuti kavu, wanachofanya hawa magamba ni ile, jahazi lizame tugawane mbao.
Huyu jamaa anajua gravity ya EL kwenye hiyo sisiem yao, so pengine ameona hapo ndipo safe side kwake. Huwezi jua ameahidiwa nini na rafiki yake.

Mimi alichoniacha hoi ni pale alipotenganisha urafiki binafsi na maswala na political interests, how valid could this be.At least mmoja wapo asingekuwa mwanasiasa basi, hivi inawezekanaje huu urafiki kati ya mwizi na mtu asiye mwizi. Nijuavyo mimi siku zote marafiki wanashare common interests. Inawezekana na wao hawajakutana barabarani tu!

Mngeja bwana! Haya, sisi yetu macho tu.
jina sahihi ni Mgeja,HAMIS MGEJA.Asije akawa kama Mashishanga kwa Sumaye
 
Lowasa mjanja,anateka kanda ya ziwa,anajua huko ndo kwa kupatia ushindi

Huyu Mgeja anataka nini kwa Mafisadi? Mbona wananchi wa Shinyanga walishachoka na hao watu? Mbona hasomi alama za nyakati? Bila kuchakachua mkoa wake ulikuwa umepoteza majimbo mengi sana likiwemo la Kahama, Msalala, Shinyanga Mjini achilia mbali Bariadi Magharibi. Kwa taarifa yake Wasukuma wakisema wamechoka ujue hakuna wa kuwazuia. This is one of the useless leader CCM is trying to keep.
 
Hajui kama Lowassa Ni Gamba lililogoma Kuvuka likija kuvuka lenyewe au wakilivua kinguvu naye ataenda na maji... Mgeja umekaa kwenye tawi Bovu
Ulichosema kimenikumbusha Mashishanga na "urafiki" wake kwa Sumaye Enzi zileeee...KILICHOMPATA MZEE HUYU kinafanana na unachomtahadharisha nacho Mgeja
 
Sisi ni wanafiki kweli; tunapenda kukuza mambo sana. Lowasa ni Mbunge wa Monduli, Mwneyekiti wa kamati ya Bunge ya Ulinzia na ushirikiano wa kimataifa (sina uhakika), na Mjumbe wa Kamati kuu (au halmashauri kuu) ya CCM. Sasa kwa nini watu hawaoni veyo hivyo ambavyo ni hai na badala yake tunataka kutumia cheo ambacho hakipo cha wazii Mkuu aliyejiuzulu? Sana sana semeni kuwa Munbge wa monduli aliyekuwa waziri mkuu wa zamani. Kumataja kama Waziri Mkuu Aliyejouzulu na kudharau Unduge wake aliopewa na wanachi wa monduli wa kuwadharau wana Monduli.
 
Back
Top Bottom