Mgaya ang'ara mbele ya Kikwete. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgaya ang'ara mbele ya Kikwete.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by minda, Oct 6, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Send to a friend Wednesday, 06 October 2010 07:45 0diggsdigg

  [​IMG] Walimu wa mkoani Ruvuma wakipita kwa maandamano na mabango mbele ya Rais Jakaya kikwete jana wakati wa maadhimisho ya siku ya walimu Duniani.  Joyce Joliga, Songea

  NAIBU katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Nicolaus Mgaya jana alikuwa kivutio kikubwa mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati aliposhangiliwa kwa muda wa zaidi ya dakika kumi baada ya kutambulishwa ili asalimie walimu.

  Mgaya alikuwa akitambulishwa katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambayo yalifanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na kuhudhuriwa na walimu wengi na wananchi wengine.

  Mgaya alitambulishwa na katibu mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Yahya Msulwa ambaye alimtaka asimame na kuwasalimia wananchi pamoja na walimu.

  Baada ya Mgaya kuitwa, alisimama na kushangiliwa kwa zaidi ya dakika kumi na maelfu ya walimu waliokuwepo uwanjani hapo, huku wakimuita mkombozi na mtetezi wao mkubwa.

  Pamoja na kuwa naibu katibu mkuu, Mgaya ndiye aliyeonekana kuwa mstari wa mbele kufanikisha mgomo wa wafanyakazi wote uliopangwa kufanyika Mei 5, lakini haukufanyika baada ya Rais Kikwete kutoa onyo dhidi ya mfanyakazi ambaye angeshiriki.

  Wakati akihutubia wazee wa Dar es salaam kuhusu mgomo huo ambao ungefanyika katika kipindi ambacho nchi ilikuwa ikiandaa mkutano mkubwa wa kimataifa wa kiuchumi, Kikwete alikuwa akitaja jina la Mgaya mara kwa mara kwenye hotuba yake

  Tucta iliitisha mgomo huo kuishinikiza serikali kushughulikia madai yao ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kuongeza kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa sekta ya umma, kuboresha kiwango cha pensheni na ufanisi wa mabaraza ya wafanyakazi.

  Akizungumza baada ya utambulisho huo, Msulwa alisema ukombozi wowote unaanzia kwa walimu hivyo ni vema serikali ikaona umuhimu wa kuboreshewa maslahi yao na kuusifu utawala wa Rais Kikwete kuwa umejitahidi kuboresha maslahi ya walimu na kutenga Sh73 bilioni kulipa madeni yao katika kipindi cha 2008 -2010.

  CWT iliitisha mgomo mwaka 2008 ikiishinikiza serikali kulipa malimbikizo yao ya muda mrefu, kupandishwa daraja, kulipwa posho za nauli na fedha za uhamisho, lakini siku moja kabla, serikali ilikwenda Mahakama ya Kazi ambayo ilitoa uamuzi wa kuzuia mgomo huo usiku.

  Msulwa alisema bado kuna matatizo mengi ambayo yanawakabili walimu, ukiwemo upungufu wa nyumba za walimu 181,440 na kuwa hali ni mbaya zaidi vijijini ambapo hakuna nyumba za kupanga hivyo kuwasababishia walimu kuishi katika mazingira magumu.

  Aliyataja matatizo mengine ya walimu kuwa ni pamoja na kutolipwa malimbikizo yao ya mshahara, fedha za uhamisho, matibabu pamoja na posho za kufundishia na kuiomba serikali iwaharakishie.

  Akihutubia mkutano huo, Rais Kikwete alisema amesikia matatizo yanayowakabili walimu na ameahidi kuwa atayafanyia kazi yote, ikiwa ni pamoja na na kuboresha zaidi maslahi ya walimu na kuwataka wafanye kazi kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu nchini.

  Source: Mwananchi
  my take:

  nukuu ya kunukulika:

  Rais Kikwete alisema amesikia matatizo yanayowakabili walimu na ameahidi kuwa atayafanyia kazi yote, ikiwa ni pamoja na na kuboresha zaidi maslahi ya walimu na kuwataka wafanye kazi kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu nchini.


  kwa hiyo tuseme walimu pamoja na wafanyakazi wengine wategemee utatuzi wa matatizo yao bila kuathiri kauli ya kwamba hata miaka 8 ijayo walimu wasitegemee kuboreshewa mishahara? au ndio siasa?
   
 2. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aah hizi ahadi nyingine ni za kuwekewa kumbukumbu tu kwamba zilitamkwa. Kimsingi JK hawezi kutekeleza chochote cha maana kwa miaka 5 ijayo HATA KAMA atakuwa rais. Kazi yake kubwa itakuwa kuanzisha kampeni za nani awe mgombea urais wa CCM 2015 ili kulinda maslahi yake, ya familia yake na washirika wake. Jk hakuwa, hana na wala hatakuwa na maslahi kwa taifa
   
Loading...