Mgawo wa UMEME ARUSHA waanza Rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgawo wa UMEME ARUSHA waanza Rasmi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MVUMBUZI, Sep 12, 2012.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,768
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Nisemalo ni kweli kwani jana ilikuwa ni zamu ya maeneo ya Njiro ambapo umeme ulikatika asubuhi na kurudi saa nne usiku. Leo ni Zamu ya maeneo ya Kimandolu na vitongoji vyake ambapo umeme umekatika saa 5 asubuhi hadi jioni haujarudi.
  Kinachosikitisha ni kwamba kampuni ya Symbion iliweka mitambo ya kuzalisha umeme eneo la Njiro TANESCO kwa ajili ya kuzalisha umeme na tayari imeshaanza kazi lakini hii haikuwa ni suluhisho na badala yake tunarudi kule kule. Kwa maelezo ya ndani ya TANESCO mgao huu utaendelea kwa kipindi cha mwenzi huu wa September hadi tarehe 30.

  Uzoefu unaonyesha kuwa mgao ukishaanza Arusha ambayo hutumika kama Quinese pig ya kupima reaction lazima uenee nchi nzima.

  Wakazi wa Arusha tunapata shida kujua tatio nini kwani majenerator yaliyowekwa tangu yaanze uzalishaji hayana hata miezi 3 tunarudi kule kule kwenye mgao wa umeme.
  Hii inatufanya wananchi tuone kuna hujuma nyingi zinafanywa na watu wachache wabinafsi ambao wako tayari kumwua au kumsababishia mwenzake mateso makali ili mradi amepata anachotaka.

  Tunaomba TANESCO mkoa watupe majibu kuna tatizo gani mpaka wataabishe wakazi wa Arusha kwa kiasi hicho kwani kesho itakuwa zamu ya kitongoji au mtaa mwingi.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,926
  Likes Received: 5,080
  Trophy Points: 280
  mmh huku kijijini kwangu hakuna umeme toka saa moja ndo mgao wenyewe nini? Na mie sipo arusha.....

  Au ndo ule mgao wa mezani?
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,114
  Likes Received: 2,213
  Trophy Points: 280
  Huku kwetu umeme umekatika asubuhi mpaka sasa haujarudi dsm nipo maeneo ya mbezi.
   
 4. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,748
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 160
  Zitto Kabwe alisema wakati wa kipindi cha Bajeti kwamba hakuna pesa zimetengwa kununulia mafuta ya kuendesha Majenereta ya kukodi! Akasema baada ya muda mgawo utaanza na wahusika watadai wanahujumiwa na mafisadi. Tuombe mvua zinyeshe,mitambo ya Kihansi na Mtera isisimamishe uzalishaji wa umeme.
   
 5. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 1,308
  Trophy Points: 280
  Wametangaza kuwa ni kutokana na wanafanya mabadiliko ya nyaya na nguzo kwa muda wa wiki mbili. Ni mojawapo ya hatua ya kuepuka usumbufu kipindi cha mvua kali zikianza.
  Source: Kwenye television (lilikuwa ni tangazo kutoka TANESCO).
   
Loading...