Mgao wa Umeme wawa kero Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112

3314234.jpg

Monday, October 12, 2009 7:53 PM
MGAO wa umeme wa zaidi ya saa 14 kwa siku katika kila kona ya jiji ya Dar es Salaam, ulioanza wiki iliyopita nchi nzima, umekuwa ni kero na kuwasababishia watu kuingia hasara katika shughuli zao za kila siku. Kufuatia mgao huo wakazi wa jiji hilo wamekuwa na hali ya kuingia na hali ya mashaka kuhusu mgao huo unaokuwa kero katika jiji hilo.

Hali hiyo imedaiwa kuwa ni mchongo uliochongwa na wenye nyadhifa ili kuifanya Serikali, Bunge na Watanzania wote walazimike kukubaliana na uamuzi wa kununuliwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Dowans, ambayo ni mbadala wa kampuni tata ya kuzalisha umeme ya Richmond.

Hayo yanahisiwa kwa kuwa hadi kufika sasa Serikali haijawa na mikakati madhubuti ya kuondoa tatizo hilo la umeme nchini ambalo linapunguza vipato vya baadhi ya watanzania kwa siku.

Baadhi kwa wakazi wa jiji hilo na wanasheria wanasema kuwa endapo serikali ingeamua kuvalia njuga suala hilo basi tatizo hilo lingemalizika mara moja kwa kuwa Serikali yetu ina pesa nyingi sana, na kudaiwa kuwa hivi sasa inakusanya zaidi ya shilingi bilioni 250 kwa mwezi kupitia kodi.

Na isingeshindwa kuwapatia Watanzania umeme wa uhakika kuliko hii hali iliyopo sasa wa kukaa bila umeme zaidi ya masaa 12 na kuendelea nchi nzima.

Hata hivyo uongozi wa juu wa shirika hilo walipohijiwa kuhusiana na tuhuma hizo walikana vikali na kudai kuwa mgao huu hauhusiani hata kidogo na mitambo ya Dowans.

Na kusema kuwa mgao huu unatokana na vyanzo vya umeme kuwa hafifu na kuzalisha umeme ambao hautoshelezi kwa kutumia nchi nzima na ndio chanzo cha mgao huo.

Kufuatia mgao huo wananchi wameulani vikali mgao huo mana unawarudisha nyuma kimaendeleo kwa kuwa bila umeme hawawezi kuongeza kipato cha siku kutokana na shughuli zao zinaenda na umeme.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3314234&&Cat=1
 
kweli mkuu mbona tutajuta kuifahamu serikali ya JK na TANESCO mwaka huu.yaani mgao ni masaa 15 daily.nimeweka kijenereta home majirani wanasema nawapigia kelele yaani ni mateso tupu
 
kweli mkuu mbona tutajuta kuifahamu serikali ya JK na TANESCO mwaka huu.yaani mgao ni masaa 15 daily.nimeweka kijenereta home majirani wanasema nawapigia kelele yaani ni mateso tupu

Hahahahah! majirani wanataka mlambe mateso wote sasa wewe unaleta
ufahari ili uendelee kuangalia TV lazima walalamike. hehehehehe

HAO MAJIRANI HAWAONI KAMA UMEME HAKUNA? NA KAMA UNA MAMBO YAKO
MUHIMU YAKUFANYA NA UWEZO WA JENERETA UNAO KWANINI USIWEKE.

Wabongo kwa lawama....
 
Yaani masaa 15 kwa siku bila umeme du, wacha tu niendelee kupiga box huku ughaibuni.
 
inaboa sana hivi hii ni hujuma au ni kitu gani ..Hawana hata aibu kuongeza mgao
 
Yaani mgao unatuchosha, halafu siku hizi hawana ratiba maalumu wanakata tu ovyo, kuanzia saa tatu asubuh hadi 12 jion, wanakata tena saa tano usiku, wanaleta 12 asubuh saa 3 wanakata tena, yani vululuvululu
 
Poleni, kazi kweli kweli hizi nchi zetu hapa kwetu tulikuwa na mgao until last week, sasa wameleta generators inabidi bills ziende juu!! hapaponi mtu!
 
Inasikitisha sanaa..yaani karibu miaka 50 baada ya kupata uhuru ..bado umeme ni tatizo!!
 
Yaani masaa 15 kwa siku bila umeme du, wacha tu niendelee kupiga box huku ughaibuni.

heri yako una sehemu ya kupiga box huko ughaibuni wananchi wenzio hapa ni kutaabika tu kwa kwenda mbele
 
Yaani wanatufanya tuwa sujudie kwa sababu ni wenye nchi wametufanya wanachi hatuna la kusema bali kukubali yaishe ebu fikiria mtu anakudharau kiasi hicho hakuwekei ratiba anakatakata tuu umeme hujui lini ununue vyakula uweke kwenye fridge wengine taarifa za habari ni ndoto hatujui nini knaaendelea yaani hivi tuseme lugha gani ili utawala wa Kikwete ufahamu kwamba nchi imewashinda,aibu tena aibu tena sana,tu kama Dar es Salaam inatoa changizo kwenye pato la taifa kwa asilimia 70 wanataka nini kitokee sasa ishuke iwe asilimia mbili halafu taifa lifanyeje
Hii serikali uji kabisa hovyo hovyo hakuna mfano
 
yaani mchana wanakata maofisini na generator haiwezi kurun ac ofisi zote computer na vifaaa vingine, ukitoka jion ni zamu ya nyumbani.
 
kweli mkuu mbona tutajuta kuifahamu serikali ya JK na TANESCO mwaka huu.yaani mgao ni masaa 15 daily.nimeweka kijenereta home majirani wanasema nawapigia kelele yaani ni mateso tupu

Weka nani hii kaka... solar power haina kelele hiyo ila utawaumiza roho.....
 
Back
Top Bottom