Mgao wa umeme waisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgao wa umeme waisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 29, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Date::9/29/2008
  Tanesco watangaza mgawo wa umeme kwaheri
  Jackson Odoyo na Aika Mushi
  Mwananchi

  MGAWO wa umeme uliokuwa ukiendelea nchi nzima sasa umekwisha baada ya mafundi kutoka Marekani kuwasili na kutengeneza mtambo mmoja wenye uwezo wa kuzalisha megawati 40.

  Awali Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ilitangaza kuwepo kwa mgao wa umeme nchini nzima baada ya mitambo mitatu ya Kampuni ya Songas inayozalisha umeme wa gesi asilia ya megawati 182 kuharibika.

  Akizungumza na Waandishi wa habari jana ofisini kwake Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masudi alisema mgao huo umesitishwa rasmi kuanzia sasa baada ya mafundi hao kufanikiwa kutengeneza mtambo mmoja.

  "Kuanzia leo hakutakuwa na mgao wa umeme kwa sababu wataalamu kutoka Marekani waliwasili juzi na kuanza kazi ya kutengeneza mitambo iliyokuwa imeharibika,"alisema Masudi.

  Alisema megawati hizo 40 zilizoomgezeka pamoja zile 72 zilizokuwa zinazalishwa awali na kampuni hiyo zitaweza kusaidia na kwamba mbali na megawatt hizo pia wanategemea mitambo yao mingine inayotumia nguvu ya maji na mafuta.

  Badra aliongeza kusema kwamba kutokana na hatua hizo Tanesco ina uhakika suala la mgao wa umeme halitakuwepo tena na kwamba kama kutakuwa na tatizo lolote watatoa taarifa mapema iwezekanavyo.

  Kuhusu suala la Kampuni ya Songas kuharibikiwa mitambo yao wakati wameingia mkataba na Tanesco alisema kwa mujibu wa mkataba wao katika kipindi hiki ambacho Kampuni hiyo ilishindwa kuzalisha umeme katika kiwango kinachotakiwa hawatawalipa.

  Alisema mkataba huo unawaelekeza wawalipe mara baada ya wao kuzalisha umeme tena kwa kiwango walicho kubaliana tu na kwamba kwa mantiki hiyo katika kipindi chote walichoshindwa kuzalisha kutokana na mitambo yao kuwa mibovu hawatalipwa.
   
 2. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huu unaonyesha ni moja ya mikataba iliyosainiwa kwa hila na yenye harufu ya rushwa. Ikiwa Tanesco hawatawalipa Songas kwa kutopatiwa umeme its common sense kuwa Tanesco wamepata hasara na Songas wanatakiwa wawalipe Tanesco kwa damages walizopata. Hiyo condition ingewawezesha hao Songas wawe makini na kuwa na back up nzuri ili inapotokea matatizo Tanzania isiwe gizani. Kwani ukweli wa mambo sio Tanesco tu ndio watakosa kuuza umeme na wauza bidhaa (perishable goods) wanaingia hasara ya mamilioni. Sijui hili mnalionaje au labda mimi I am from mars! maana watu wanachukulia poa tu kwa kila kitu
   
 3. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umeongea point, juzi juzi nilisoma habari kwenye gazeti (thisday ---soma hapa) moja baada ya mgawo kuanza kuwa Tanesco wanaandaa master plan kwa ajili ya umeme wa nchi nzima na wanapendekeza kuwe na buffer ya 15% kwa sababu nchi nyingine ndio wanafanya hivyo. Nikawa najiuliza ina maana miaka yote ili lilikuwa halijulikani? Halafu bado tunashangaa kwanini investors wanakwenda Kenya na sio Tanzania....we are not serious on everything we do.
   
Loading...