Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,180
- 149
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mgao wa umeme ulionaza huko Tanzania Bara hautovikumba visiwa vya Zanzibar kwa kuwa wao ni walipaji wazuri huduma hiyo.
Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kasssim Mzee aliwaambia waandishi wa habari nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi jana waliotaka ufafanuzi kuhusiana na mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa katika sehemu mbali mbali za Tanzania bara.
Huo mgao sisi hautotukumba kwa sababu sisi ni walipaji wazuri tu wa huduma hiyo na hivyo suala la mgao ni huko Tanzania bara kwetu sisi tumesalimika katika suala hilo alisema Mzee.
Alisema Zanzibar inalipa kiasi cha shilingi 1.2 billioni kila mwezi kuilipa shirika la TANESCO hivyo haoni kama kuna sababu ya kupewa mgao huo ambao hutolewa hivi sasa katika maeneo mbali mbali ikiwemo mikoani.
Mzee alisema Zanzibar kwa wastani wa matumizi ya umeme huwa inatumia karibu megawati 47 kiwango ambacho kinatosha kwa matumizi ya kawaida kinatosha sana.
Nadhani mgao wa umeme uliopo Tanzania Bara kwa sasa hautoathiri Zanzibar .sisi matumizi yetu tunayopewa ya umeme yanatosheleza kwa ujumla na hakuna sababu ya kukatiwa umeme kwa sasaalisema Tafana.
Tulikuwa na tatizo la muda mrefu la kudaiwa bili ya umeme kiasi ya kutishiwa kukatiwa huduma hiyo kwa sasa halipo tena .Zanzibar tumekuwa walipaji wazuri wa matumizi ya umeme wa TANESCO nadhani hivi sasa tatizo kubwa kwetu ni huko Pemba lakini nalo linakariba kumalizika iwapo umeme wa chini ya bahari ukikamilika alisema Mzee.
Mwaka mmoja Zanzibar ilikatiwa umeme waka kutokana na kuwa na rimbikozo la deni kubwa na kusababisha shirika la TANESCO kulikatia umeme shirika la umeme la Zanzibar na kusababisha Zanzibar kuwa gizani.
Suali hilo lilizusha malalamiko makubwa ndani ya baraza la wawakilishi kwa wajumbe kukasirishwa kutokana na kukatiwa umeme huo na seriakli mbili zilianzisha mazungumzo na umeme huo kurejeshwa lakini wajumbe walitoa aliitaka serikali iwe imepata somo kutokana na tukio hilo.
Kukatwa kwa umeme visiwani Zanzibar kulitokana na kuwa na limbikizo kubwa la deni ambalo lilifikia zaidi ya shilingi billioni 130 jambo ambalo shirika la ygazi wa umeme lilishindwa kuvumilia na kuamua kuikatia Zanzibar na kuwalaza giza.
Shirika la umeme la Tanzania TANESCO limetangaza kuanza kwa mgao wa umeme nchi nzima kufuatilia kupunguwa kwa kiwango cha maji katika mabwawa yake nchini.
SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.