Mgao Wa Umeme Hautuhusu: SMZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgao Wa Umeme Hautuhusu: SMZ

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Oct 20, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mgao wa umeme ulionaza huko Tanzania Bara hautovikumba visiwa vya Zanzibar kwa kuwa wao ni walipaji wazuri huduma hiyo.

  Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kasssim Mzee aliwaambia waandishi wa habari nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi jana waliotaka ufafanuzi kuhusiana na mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa katika sehemu mbali mbali za Tanzania bara.

  “Huo mgao sisi hautotukumba kwa sababu sisi ni walipaji wazuri tu wa huduma hiyo na hivyo suala la mgao ni huko Tanzania bara kwetu sisi tumesalimika katika suala hilo” alisema Mzee.

  Alisema Zanzibar inalipa kiasi cha shilingi 1.2 billioni kila mwezi kuilipa shirika la TANESCO hivyo haoni kama kuna sababu ya kupewa mgao huo ambao hutolewa hivi sasa katika maeneo mbali mbali ikiwemo mikoani.

  Mzee alisema Zanzibar kwa wastani wa matumizi ya umeme huwa inatumia karibu megawati 47 kiwango ambacho kinatosha kwa matumizi ya kawaida kinatosha sana.

  “Nadhani mgao wa umeme uliopo Tanzania Bara kwa sasa hautoathiri Zanzibar….sisi matumizi yetu tunayopewa ya umeme yanatosheleza kwa ujumla na hakuna sababu ya kukatiwa umeme kwa sasa”’alisema Tafana.

  “Tulikuwa na tatizo la muda mrefu la kudaiwa bili ya umeme kiasi ya kutishiwa kukatiwa huduma hiyo kwa sasa halipo tena….Zanzibar tumekuwa walipaji wazuri wa matumizi ya umeme wa TANESCO nadhani hivi sasa tatizo kubwa kwetu ni huko Pemba lakini nalo linakariba kumalizika iwapo umeme wa chini ya bahari ukikamilika” alisema Mzee.

  Mwaka mmoja Zanzibar ilikatiwa umeme waka kutokana na kuwa na rimbikozo la deni kubwa na kusababisha shirika la TANESCO kulikatia umeme shirika la umeme la Zanzibar na kusababisha Zanzibar kuwa gizani.

  Suali hilo lilizusha malalamiko makubwa ndani ya baraza la wawakilishi kwa wajumbe kukasirishwa kutokana na kukatiwa umeme huo na seriakli mbili zilianzisha mazungumzo na umeme huo kurejeshwa lakini wajumbe walitoa aliitaka serikali iwe imepata somo kutokana na tukio hilo.

  Kukatwa kwa umeme visiwani Zanzibar kulitokana na kuwa na limbikizo kubwa la deni ambalo lilifikia zaidi ya shilingi billioni 130 jambo ambalo shirika la ygazi wa umeme lilishindwa kuvumilia na kuamua kuikatia Zanzibar na kuwalaza giza.

  Shirika la umeme la Tanzania TANESCO limetangaza kuanza kwa mgao wa umeme nchi nzima kufuatilia kupunguwa kwa kiwango cha maji katika mabwawa yake nchini.


  SOURCE:
  ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwa hiyo giza mwisho Chumbe.
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama mgao hauwahusu kwanini mnaleta choko choko sasa,mkiendelea tutawakatia umeme na huo mgao hamtapata hata kidogo ili mtumie mafuta hewa mliyoyapata huko zenj!!
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sisi tunanunua kwa mkataba maalum. Hivyo lazima tanesco itekeleze mkataba huo.
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi Visiwani kwa nini wasizalishe umeme wao? Ni hadi utoke bara!
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Sababu ni mbili kuu.
  1. Visiwa vyetu vya Unguja na Pemba vimezungukwa na bahari. Hivyo maji ya chumvi.

  2. Umeme wa HEP unazalishwa kutokana na maporomoko ya maji jambo ambalo katika bahari hakuna maporomoko.

  Kwa upeo wangu najua hayo.
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  ZNZ si wanahitaji umeme unaolingana na anaotumia mbara mmoja tu (kwa mfano Shubash kwenye viwanda vyake pale mikocheni). Wangekuwa wanahitaji mwingi wangeingizwa kwenye mgao tu!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Msisahau kuna majenereta ya umeme pale Saateni
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Daniel Yona alipokuwa waziri wa fedha aliiambia SMZ kuwa "...hakuna suala la undugu hapa msipolipa tutawakatia...business is business..." akasepa, na walikata kweli...baada ya 'hasira' na 'matusi' ya SMZ, wakarejesha,hivi sasa,kama umemsoma naibu wazir hapo juu anasema wao ni wateja wazuri wa Tanesco...kwa makubaliano maalumu kati yao ndo maana akasema giza hilo linaishia huko huko...visiwani walaa.
  23rd June 2009,
  The Zanzibar government is negotiating with a power generation firm based in Israel, to produce electricity from sea waves.

  Isles Water, Construction and Lands, Tafana Kassim Mzee said this at the ongoing House of Representatives meeting here yesterday when responding to a question from Ali Abdalla Ali, (Mfenesini, CCM) who demanded clarification on efforts by the government to address the problem of power.

  He said the project would soon be introduced in Pemba.
  He added that experts from Israel had carried out feasibility studies in the area and discovered the huge potential on sea wave power production project.

  “The government is currently working on the report prepared by the power firm for implementation. I led a special delegation to Israel where we learnt about the functioning of a similar project.

  Three sources of power will be installed in Zanzibar. They include wind, sea waves and residue whose experts from Germany are negotiating with the government,” Mzee informed the House.

  Furthermore, the government intended to have in place thermo power generation, explained the deputy minister, saying the aim was to ensure supply incase of failure of the national power grid from the Mainland.

  However, the House was further informed that the intermittent power blackouts were due to various reasons including, wearing out of the supply infrastructure and accidental short-circuiting of power lines.
  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 10. mponjoly

  mponjoly Member

  #10
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 4, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haiwahusu kivipi?kwani hamwezi hata kufeel sorry for ur fellow compatriots tz bara?siku yatawakuta nanyi!!
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  porojo tu za wazenji lakini hakuna lolote
   
 12. D

  Darwin JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Ndio wa kwanza kuwa na umeme hata kabla TZ bara hawajakua na umeme kwahio wanajua wanachozungumzia.

  Na kama ni wanunuzi wazuri wa umeme wanaweza pia kununua kutoka Kenya au Msumbiji.
   
 13. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Huko Visiwani hakuna hata mmoja anaeshughulikia masuala ya maendeleo kama hayo. Kama Karume angelikuwepo mpaka leo I can swear to God kwamba ZNZ leo wangelikuwa na umeme kutokana na Nuclear energy. Karume alinunua ma-generator 3 makubwa ambayo yalitoka Uingereza kwa Hercules kabla ya kidato. Wa-znz wala hawakujua hayo ma-generators ni nini baada ya kupokea umeme wa kidato na yalimalizikia sijui wapi! ZNZ imekufa na CCM inaimaliza kabisa!
  Huyu Waziri nae ni mzulufu na wala hajui huo mgao wa umeme ni kwasababu gani. Kwani huku Bara unakogawiwa ni kwasababu ya kutokulipia? Waacheni walale hivyo hivyo na maji yatakapomalizaika na umeme ukawa haupatikani kabisa, hapo tena wataingia akili na watajua la kufanya!
  Wao ni waswahili zaidi yetu, lakini wamesahau kuwa MTEGEMEA CHA NDUGU HUFA MASIKINI!!!
  Wa-ZNZ amkeni!!! Mtategemea Bara mpaka lini?????????????????
  Hata generator dogo la emergency la kuendesha Mnazi Mmoja Hospital linakushindeni?????
   
Loading...