Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Tangu Alhamis ya wiki iliyopita watu wa maeneo ya kigogo, majohe na kisarawe tunakabiliana na mgao mkali wa umeme ambao unaanza tangu saa nne za asubuhi hadi saa tatu za usiku au zaidi. Hatujui kama maeneo mengine ya Dar yanshida hii pia, but hali ya huku ni mbaya sana, na inashangaza kwb hadi hivi sasa Tanesco hawajatangaza uwepo wa mgao huu. Na zaidi ya yote, ninapata shida kumuelewa Muhongo aliyetangaza mgao wa umeme kuwa historia halafu mapema hivi tunaanza mgao. Inashangaza pia kwamba mgao huu umeanza mapema kiasi hiki, itakuwaje tukifika December?