Mgao huu wa umeme mjini Moro ni kero

Mgao huu wa umeme mjini Moro ni kero

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,548
Habari za leo wanajamii wenzangu wa jukwaa hili. Kumekuwa na mgao mkali wa umeme katika mji huu wa morogoro hivi karibuni bila mamlaka husika kutoa taarifa kuna hitilafu ama ni mgao ( nipo tayari kukosolewa). Umeme umekuwa ukikatika saa moja asubuhi na kurudi Saa 12 jioni. Kisha kukatwa tena saa nne usiku.

Wakati wa mjadala wa eskrow bungeni zilitoka taarifa kuwa kuna hitilafu zimejitokeza katika baadhi ya mitambo huko kidatu na tayari timu ya mafundi ilishapelekwa huko kushughulikia tatizo hilo. Cha ajabu tangu wakati huo mamlaka husika haijatupa mrejesho wa suala hilo ( I stand to be corrected).

Wakati umefika sasa wakazi wa moro na viunga vyake tuambiwe ukweli wa suala hili kwani kukatika katika huku kwa umeme kumekuwa kero kubwa...hali inayopekekea shughuli nyingi za kimaendeleo kutofanyika.
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sn. I wonder why its not among of the Seven wonders of the world. Wonders shall never cease in Tz.
 
Mgao wa umeme kwa sasa uko katika mikoa mingi tu. Tunachoomba ni taarifa rasmi ya mgao na kwa nini kuna mgao.
 
Yaani hii nchi imekuwa ya ajabu sana, kila mtu ana uwezo wa kuamua kufanya chochote bila taarifa yoyote na haogopi!
 
Na hiv mmewanyima kula uchaguzi mdogo,mtaimba chorus.

Nimewaza tu.
 
Hapa mwanza hata sasa hivi umeme hakuna na jana ilikuwa giza usiku kucha...
_kama kawaida tumekaa kimya kama bubu
 
Habari za leo wanajamii wenzangu wa jukwaa hili. Kumekuwa na mgao mkali wa umeme katika mji huu wa morogoro hivi karibuni bila mamlaka husika kutoa taarifa kuna hitilafu ama ni mgao ( nipo tayari kukosolewa). Umeme umekuwa ukikatika saa moja asubuhi na kurudi Saa 12 jioni. Kisha kukatwa tena saa nne usiku.

Wakati wa mjadala wa eskrow bungeni zilitoka taarifa kuwa kuna hitilafu zimejitokeza katika baadhi ya mitambo huko kidatu na tayari timu ya mafundi ilishapelekwa huko kushughulikia tatizo hilo. Cha ajabu tangu wakati huo mamlaka husika haijatupa mrejesho wa suala hilo ( I stand to be corrected).

Wakati umefika sasa wakazi wa moro na viunga vyake tuambiwe ukweli wa suala hili kwani kukatika katika huku kwa umeme kumekuwa kero kubwa...hali inayopekekea shughuli nyingi za kimaendeleo kutofanyika.

poleni morogoro mkose maji na umeme tena
 
naona IPTL wamezima mitambo yake maana hapa Arusha leo siku ya tano hakuna kazi kwa mafundi wanaotumia umeme!
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sn. I wonder why its not among of the Seven wonders of the world. Wonders shall never cease in Tz.

Kweli hii nchi n ya ajabu sana alafu tunataka tukue kiuchumi tunachekesha sana
 
Back
Top Bottom