Mganda amshitaki Katibu Mkuu wa EAC katika kesi ya aina yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganda amshitaki Katibu Mkuu wa EAC katika kesi ya aina yake

Discussion in 'International Forum' started by Ngongo, Jul 9, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Ni ya kuchelewesha uundwaji wa 'Supreme Court' ya jumuiya
  JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imekumbwa na misukosuko ya kisheria baada ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kushitakiwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki kwa madai ya kuchelewesha suala la kupanua mamlaka (jurisdiction) ya mahakama hiyo kuwa mahakama ya rufaa (supreme court) katika jumuiya hiyo.

  Kesi hiyo ilifunguliwa na mbunge wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki toka nchini Uganda, Sitenda Sebalu na hati mashitaka iliwasilishwa mahakamani hapo Juni 14 mwaka huu.

  Mlalamikaji katika kesi hiyo anawakilishwa na mawakili kutoka kampuni maarufu nchini Uganda ya Bakiza & Co. Advocates, Semuyaba, Iga & Co. Advocates.

  Katika kesi hiyo, kwa mujibu wa hati ya mashitaka ambayo Raia Mwema limefanikiwa kuiona, washitakiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Uganda na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo.

  Mbunge Sebalu, katika kesi hiyo namba moja ya 2010, anadai kuwa mshitakiwa namba moja; yaani Katibu Mkuu wa EAC amevunja mkataba unaounda jumuiya hiyo kwa kuchelewesha kuuitisha mkutano wa Baraza la Mawaziri uweze kuamua juu ya mamalaka ya mahakama hiyo.

  Sebalu anadai kuwa Katibu Mkuu huyo amevunja Ibara ya 7 (2),8 (1), (C) na Ibara ya 6 ya mkataba unaounda Jumuiya ya Afrika Mashariki uliosainiwa na viongozi wakuu wa nchi hizo mwaka 1999. Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, kwa sasa, ni Juma Mwapachu wa Tanzania.

  “Kutoitisha mkutano wa baraza la mawaziri wa EAC na kimya chake kizito juu ya suala hili, ni ukiukwaji wa mkataba (treaty) unaounda jumuiya yenyewe”, inasomeka sehemu ya hati hiyo.

  Anaitaka mahakama hiyo iamuru Jumuiya ya Afrika Mashariki kuharakisha majadiliano ya itifaki inayotaka mamlaka ya mahakama hiyo ipanuliwe ili kutoa fursa kwa wananchi katika jumuiya hiyo wanaonyimwa haki na mahakama za kitaifa kupeleka malalamiko yao katika mahakama hiyo isiyokuwa na mfungamano na upande wowote.

  Kwa mujibu wa maelezo ya mbunge huyo wa zamani, kilichomsukuma kufungua kesi hiyo ni hatua ya yeye kunyimwa haki na mahakama za Uganda baada ya kupeleka malalamiko yake dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa, Sam K. Njuba ambaye ndiye aliyemshinda katika kinyang’anyiro cha ubunge wa jumuiya hiyo.

  “Kama mamlaka ya Mahakama ya Afrika Mashariki ingekuwa imepanuliwa, ningekata rufaa dhidi ya kesi yangu na ningepata haki yangu….naamini wananchi wengi wa jumuiya hii wananyimwa haki na mahakama za kitaifa na hawana pa kwenda zaidi ya hapo” anasema Sebalu katika maelezo yake ya ziada.

  Msajili wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Dk. John Ruhangisa ameithibitishia Raia Mwema kuwa kweli kesi hiyo imeshafunguliwa katika mahakama hiyo.

  “Tumepokea kesi hiyo na tayari tumekwisha watumia notisi washitakiwa wote na wanatakiwa wajibu ndani ya siku 45 tangu walipoandikiwa barua hii”, Dk. Ruhangisa alisema.

  Baada ya washitakiwa wote kujibu kwa maandishi, mahakama itamuarifu mlalamikaji kisha ajibu kabla ya mahakama kupanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

  Duru za kisiasa mjini hapa zinasema kuwa kesi hiyo itakuwa na mvuto wa aina yake kutokana na ukweli kwamba wananchi wengi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatamani mahakama hiyo iwe ya rufaa katika jumuiya ili waweze kukata rufani za kesi zao zilizoamuriwa na mahakama za kitaifa.

  Wengi wanaitazama mahakama hiyo kama chombo kinachojitegemea kisichoegemea upande wowote; jambo ambalo wanaamini litawawezesha kutendewa haki kama mahakama hiyo ingepewa mamlaka ya kuwa mahakama ya rufaa.

  Itifaki ya mahakama hiyo kupewa mamlaka ya kisheria kuwa mahakama ya rufani ilishaandaliwa tangu mwezi wa Mei mwaka 2005, lakini hadi sasa hakuna anayejua kinachoendelea.

  Itifaki hiyo ilitakiwa ijadiliwe na nchi wanachama ili waafikiane namna ya kuipa hadhi mahakama hiyo, lakini Sekretarieti ya jumuiya hiyo, chini ya uongozi wa katibu wake, Balozi Juma Mwapachu, imeshindwa kusukuma mbele ajenda hiyo.

  Hata hivyo, vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya jumuiya hiyo vinaeleza kuwa suala la mahakama hiyo kupandishwa hadhi na kuwa mahakama ya rufaa linakosa msukumo kutokana na viongozi wa nchi wanachama kuwa wagumu katika kupanua demokrasia.

  “Pamoja na kuundwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini ukweli ni kwamba viongozi wa hizi nchi bado ni wazito katika kuachia baadhi ya mamlaka ya nchi zao kwenye vyombo vya jumuiya vya kufanya maamuzi kama vile bunge na mahakama”, alisema mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa jumuiya hiyo aliyeomba asitajwe jina.

  “Unajua viongozi wetu wengi wamezoea kufanya mambo ‘kiimla’ kwa ajili ya maslahi yao binafsi na nchi wanazoziongoza, kwa hiyo inakuwa vigumu kutoa uhuru nje ya mipaka ya nchi zao ili kupanua demokrasia” alisisitiza ofisa huyo.

  Hoja za ofisa huyo zinatiwa nguvu na matokeo ya kesi ya mwaka 2007 iliyowasilishwa mahakamani hapo na wabunge wa chama upinzani cha ODM cha Kenya waliokuwa wakipinga uteuzi wa nafasi za kuwakilisha nchi hiyo katika Bunge la Afrika Mashariki.

  Wabunge hao, wakioongozwa na Profesa Anyang’ Nyong’o, walipinga utaratibu uliotumiwa na Serikali ya Kenya wa kuwateua wabunge hao badala ya kupigiwa kura na wabunge wa bunge la kitaifa kama ilivyoanishwa katika mkataba unaounda jumuiya.

  Profesa Nyong’o na wenzake walifungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki kupinga hatua hiyo ya serikali ya Rais Mwai Kibaki na mahakama ilitengua uamuzi batili wa serikali na kuagiza uchaguzi huo ufanywe upya.

  Katika hukumu yao, jopo la majaji wa mahakama hiyo, wakioongozwa na Jaji Joseph Mulenga (Uganda) aliyekuwa Makamu wa Rais wa mahakama hiyo, aliweka wazi kuwa utaratibu uliotumiwa na Serikali ya Kenya kuwateua wabunge hao ulikuwa “haramu” na ni kinyume na mkataba unaounda jumuiya hiyo..

  Majaji wengine walioshiriki kusikiliza kesi hiyo na kuitolea maamuzi ni pamoja na Augustino Ramadhani (Tanzania), Harold Nsekela (Tanzania) na Kasanga Mulwa (Kenya).

  Alisema katika hukumu yake kuwa uteuzi huo ulikuwa umevunja ibara ya 50 ya mkataba wa jumuiya inayoeleza wazi kuwa kila nchi inapaswa kufanya uchaguzi kupitia mabunge ya mataifa wanachama kuchagua wabunge watakao wakilisha nchi zao katika Bunge la Afrika Mashariki.

  Hata hivyo, katika hatua ambayo haikutarajiwa na wengi, Kenya ilipuuza na kubeza mahakama na hukumu ya majaji hao na kuonya kuwa mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi wanachama.

  Mwanasheria Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wilbert Kaahwa hakupatikana mwishoni mwa wiki kuelezea hatua watakazochukua kukabiliana na kesi hiyo inayowakabili, lakini habari za ndani kutoka EAC zinaeleza kuwa tayari wamepokea notisi ya kesi hiyo na wanasheria wanajipanga kujibu hoja za mlalamikaji.

  Source :Raiamwema.

  My Take.

  Bila shaka raia wa nchi zote za EAC zinahitaji kuona mahakama ya rufaa ya Afrika mashariki inaanza kufanyakazi mara moja.Mahakama za nchi zote wanachama wa EAC zimekumbwa na jinamizi la kukumbati watawala,hukumu ya mgombea binafsi kwa upande wa Tanzania ni uthibitisho dhairi jinsi mahakama zetu zilivyo za hovyo katika maamuzi yake.

  Bwana Sitenda Sebalu atakuwa anawakilisha maoni ya wananchi milioni 126 wa Afrika mashariki kulilia uanzishwaji wa mahakama ya rufaa ya Afrika mashariki.Tuumunge mkono kwa kuonyesha njia,yamkini hata Mchg Mtikila akapata nafasi ya kupeleka malalamiko yake dhidi ya ile hukumu ya kibaradhuli ya mgombea binafsi.

   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  IMO Tz have important things to worry about..kujiingiza kichwakichwa huku gharama yake si ndogo.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Abdulhalim,

  Mkuu wangu tayari Tanzania ni mwanachama wa EAC,yapo mambo mazuri ndani ya hii community pia yapo mambo ya hovyo mabyo kila mtanzania anayapinga akiwemo mimi na wewe.mambo ya ardhi tumeyakataa,mambo ya free labour tumeyakataa lakini serekali yetu imeridhia inagwa wanasema watalinda baadhi ya ajira za wazawa wa nchi yetu,sijui vipi ?.

  Kuna hili suala la kuwa na fedha kwanye EAC mimi hili nimelihafiki kabisa.Pia kama ikiwezekana iwepo tume ya uchaguzi ya EAC ningefurahi kweli kwasababu tume za nchi zote EAC si tume huru lakini tukizipeleka kwenye jumiya zinaweza kuondoa matatizo ya hizi tume zetu kuendelea kukumbatia watawala walioko madarakani.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huwezi kuwa na tume ya uchaguzi ya Jumuiya ya Afrika Mashsriki kabla ya kuharmonize katiba za nchi husika. Leo hii wakenya kuwa na mgombea binafsi sio contentious issue lakini hapo Tanzania serikali yao inapinga; katika hali kama hiyo tume itashindwa kufanya kazi yake stahili!!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mkuu hiyo itakuwa ni white elephant.

  Kumbuka kuwa matatizo yote ktk ukanda huu yanasababishwa na watu wachache kuhodhi madaraka na kurithisha wana na mabinti zao. Kundi hili si la leo, kesho au keshokutwa, linao mtandao wa kuwalinda ndani na nje ya nchi. IMO,sasa ktk mazingira kama haya hizo tume zitakuwa ni mzigo tu kwa walipa kodi na kuuzunguka mti badala ya kuangalia ulipo mzizi mkuu ili tuuchimbue ili tuondokane adha ya mti usiozaa matunda.
   
Loading...