chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,412
- 25,001
Habarini za Jioni waungwana...
Ni katika kupashana tu na kuweza kusaidiana ili mwenzetu asije akauvaa huu mkenge wa matapeli waliojaa pale mgahawani wa Liverpool.
Kwa wale wasafiri wa route hii ya nyanda za Juu kusini bila shaka siyo wageni wa huu mgahawa.
Leo nitawaasa kuhusiana na wale vijana pale nje wanaouza mboga mboga,.
Hawa vijana ni matapeli wa kutupwa na wanajua sana kubembeleza wateja, yaani ukishuka tu kwenye gari basi wanakuganda mwanzo mwisho, na hata kama unaelekea msalani wako tayari kukusubiri mpaka utoke ukanunue bidhaa zao.
Hii imenitokea leo ila niliweza kutegua mtego wao wa kitoto.
Alinifuata kijana mmoja akinisihi sana nimuungishe japo vitunguu nikamwambia tiyari nina stock ya kutosha na vingine vinaaribika havijatumiwa, hakunielewa akaendelea kunisihi nimuungishe.
Kama mtu muelewa na nafahamu hali halisi ya maisha ni ngumu nikasema nimuungishe kijana aliyeamua kujituma siyo sawa na wa vijiweni wanasubiri kuomba tu.
Nikamwambia anipimie sado moja alikuwa akiuza elfu tisa, basi wakati anachagua sado ya kunipatia nikawa na mimi naandaa pesa ya malipo, dogo aliinua sado fasta na kumwagia kwenye fuko kubwa jeusi kwa uharaka sana nikaingiwa na wasiwasi ila nikasema itakuwa ushapu tu wa kazi, sikujali sana nikamkabidhi elfu kumi akate elfu tisa yake akanirejeshea chenji yangu.
Nafsi yangu ikaingia woga na wasiwasi nikajaribu kuangalia ndani mwa lile fuko jeusi, holla lalaaaa... Vitunguu vizima havikuzidi kumi, yaliyobaki yote ni kama mashina ya vitunguu.
Nikamrudia fasta nikamwambia kijana huu UHUNI naujua kabla yako, chukua vitunguu vyako leta pesa yangu, akaanza kuomba msamaha pale nikamwambia rejesha pesa kabla sijakufanya kitu mbaya. Akawa amerejesha nikamwambia umekutana na mtu mstaarabu nikamuacha.
Chondechonde wandugu, route hii ya imejaa matapeli sana, yule unayemuonea huruma kumbe siye.
Tuwe na tabia ya kuhakiki bidhaa tunazozinunua kabla ya malipo.
Wengi wamelizwa.....