Mfundishe mtoto wako kujitegemea

KatetiMQ

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2022
Posts
299
Reaction score
613
KAMA mzazi au Mlezi moja ya lengo kuu la Malezi ya Mtoto wako linapaswa kuwa: "Kumfundisha kujitegemea"....

MTOTO anapaswa kukulia katika Malezi yanayompa Changamoto ya kukuza Ujuzi, ukakamavu, ustahimilivu, uwajibikaji, juhudi, ili kumwongoza katika maisha yake ....

Mruhusu mtoto wako Kufanya makosa, na anapokosea mfundishe kuwa makosa ni fursa ya kujifunza ili kuwa Bora zaidi wakati UJAO...

Mshirikishe mtoto wako katika shughuli za nyumbani. Hakikisha unampa kazi zinazoendana na umri WAKE...

TOA chaguo na Uhuru Lakini ndani ya Mipaka. Kufanya hivi humjengea mtoto wako ujasiri katika Ufanyaji wa maamuzi na kusaidia kujenga hisia ya KUWAJIBIKA....

MHIMIZE mtoto wako kujitegemea, Epuka kumpatia usimamizi katika kila anachopaswa kukifanya. Jaribu kila siku kuwa mbali na Mtoto wako katika kumpatia kitu Cha kufanya peke yake bila uwepo WAKO karibu...

KWA kadiri iwezekanavyo, epuka kumrekebisha mtoto wako wakati anajaribu kufanya kitu kwa kujitegemea. Kwa mfano; Ikiwa umemwomba mtoto wako atandike kitanda chake na ukaona hajatandika vizuri pingana na tamaa yako ya kutaka kurekebisha Jaribu kukumbuka kuwa ukamilifu si lengo. Lengo ni kuruhusu mtoto wako kuwajibika....

IKIWA utaonekana kumrekebisha katika kila anachokifanya, unaua Uwezo wake wa Kuendelea kufanya kwasababu Ikiwa atafanya atahisi kuwa hafanyi kulingana na viwango VYAKO....

KUKUZA Uhuru wa kujitegemea kwa mtoto wako Ni zawadi pekee...

Epuka Kumsaidia Mtoto wako kazi ambayo unahisi anaweza kuifanya...

UFUNGUO wa kumuandaa mtoto wako kujitegemea ni mkuruhusu Kufanya kile anachopaswa kukifanya nasio kumfanyia.....

VIJANA wengi wakike au wakiume wanaoendelea kukaa majumbani kwa wazazi wao licha ya umri mkubwa walionao. Ni wale waliokulia katika Malezi yasiyotoa fursa ya kujitegemea wao kama wao zaidi ya kutegemea.....

CHAGUA kuwa Mzazi Bora kwa mtoto wako kwa kumuandaa kujitegemea.....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…