Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,135
- 48,821
July 08 2016 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephaim Kwesigabo amezungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi June, 2016 umeongezeka hadi 5.5% kutoka 5.2% mwezi uliopita kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma, Kwesigabo amesema…….
>>>’ Mfumuko wa bei umesababishwa na kuongezeka kwa bei za vyakula kama vile mahindi ambayo yameongezeka kwa 3.2%, unga wa muhogo kwa 2.4%, samaki wabichi kwa 3.8%, maziwa mgando kwa 4.3%, maharage mabichi yaliyomenywa kwa 6.1%, kitunguu swaumu kwa 12.5%, njegere kwa 6.2%, viazi mviringo kwa 2.5%, mihogo mibichi kwa 6.7%, magimbi kwa 4.5%, na ndizi za kupika kwa 2.7% ‘
Aidha amesema bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na huduma ya kinywa na meno ambayo imeongezeka kwa 13.8%, mafuta ya dizeli kwa 2.4% na mafuta ya petroli kwa 4.3%.
Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa mwezi June, 2016 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.5 ongezeko sawa na mwezi uliopita. Aidha amesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula majumbani na migahawani umeongezeka hadi 8.3% mwezi June, 2016 kutoka 7.2% mwezi May, 2016. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.47 mwezi June, 2016 kutoka 103.00 mwezi uliopita.
Kwesigabo amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 96 na senti 65 mwezi June, 2016 kutoka mwezi December, 2015.
Source: Millard Ayo.