Asalam Aleykum wana JF.
Ama baada ya salamu hizo, niende kwenye hoja moja kwa moja.
Ndugu zangu, upo usemi usemao "Duniani, kitu pekee ambacho hakibadiliki, ni mabadiliko!".
Mabadiliko hayakwepeki kwa hali na mali.
Hivyo ni vizuri mara zote kujiandaa kukabiliana na mabadiliko katika maisha yetu. Ni sawa tu na binadamu anaanza kama mimba, mtoto, kijana (wa kike au wa kiume), mtu mzima, Mzee na hatimaye kufa.
Kuna wakati unakuwa na Afya Njema, na kuna wakati unaumwa. Hayo yote ni mabadiliko na hatuwezi kuyakwepa.
Kwa hali hiyo basi, binadamu kwa asili ni kiumbe ambaye anapenda mabadiliko. Ndiyo maana hata chakula huwa tunabadilisha badilisha.
Hatuwezi kula makande kila siku, usiku na mchana kama ambavyo pia hatuwezi kula pizza kila siku mchana na usiku.
Kwa hali hiyo pia, hata linapokuja suala la serikali ni lazima kujua kwamba ni vigumu kwa chama kimoja kuongoza serikali milele. Hakipo na hakitakuwapo.
Hivyo ninashauri mfumo wetu (wengine kitaalamu wanauita "Deep State"), kuwa na chama mbadala na ikiwezekana watu mbadala ambao "wameandaliwa" kushika jahazi la kuongoza nchi yetu endapo ikatokea wananchi walio wengi wameamua hivyo.
Mfumo wetu usitumie nguvu nyingi kuyapinga mabadiliko, kwani kufanya hivyo ni sawa na kujaribu kuzuia mafuriko kwa mikono! Haiwezekani kabisa.
Najua kwa dhati kwamba idara yetu nyeti ni moja kati ya idara bora Afrika na hata duniani kwa ujumla.
Ubora huo wa mfumo, utumike kwa weledi kutuandalia mbadala kuliko kung'ang'ania chama au mtu ambaye hakubaliki kwa wale anaowaongoza.
Idara mnapaswa kuwa wazalendo kwa nchi na wala siyo chama au mtu. Idara haipaswi kuwa na uzalendo uchwara kama alivyosema Baba Askofu fulani wakati wa maazimisho ya Misa ya sikukuu ya Pasaka.
Kwenye Biblia, kitabu cha 1 Samweli 16:1, yupo nabii mmoja aliyekuwa anaitwa Samweli ambaye alikuwa ni mhafidhina (hakuwa mpenda mabadiliko). Yeye alitamani Mfalme Sauli aendelee kuongoza licha ya madhila aliyokuwa anawafanyia watu wake na uovu wake mbele za Mungu. Lakini tunaona Mungu anamwambia Nabii Samweli kama ifuatavyo,
*1 Samweli 16:1
[1]BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.*
Ni matumaini yangu, ujumbe wangu utaeleweka vyema zaidi na wahusika kwa ubora zaidi kuliko hata nilivyouwasilisha. Maana najua wao ni watu "smart" ambao huweza kutoa kilicho bora toka kwenye kibovu.
Ahsanteni sana.