mfumo wa serikali ya kidikteta tuliyoizoea kuisoma darasani na kwenye vitabu sasa ipo kwa vitendo.

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Kwa watanzania tumekuwa tukijifunza darasani na tukisoma vitabu ili kujua nini dhana nzima ya dikteta, Dalili zake na jinsi serikali yake inavyofanya kazi.

Nikirejea yale tuliyosoma kwenye historia (History) na Uraia (Civics) sina budi kuthibitisha kuwa Tanzania tunaingia katika mfumo huu wa kiudikteta. Darasani nilijifunza, Udikteta ni ile hali ya mtu mmoja au kikundi cha watu fulani kwa matakwa yao ndio wanaoamua nchi iendeshwaje bila kujali sheria na katiba ya nchi hiyo.

Nikirejea katiba ya nchi yetu inatoa uhuru wa kutoa maoni na kusema chochote pasipo kuvunja sheria ya nchi. Lakini kwa sasa Tanzania uhuru huu umetoweka kwa asilimia nyingi sana. Leo nimeona agizo toka ikulu likionesha uwepo wa uwezekano wa kufungia mitandao ya kijamii nchini. Hali hii ni dalili za udikteta tuliyosoma darasani. Vitabu vinatuambia dikteta akiwa ndiye kiongozi wa nchi watu wake hunyimwa uhuru wa kutoa maoni.

Darasani pia tulijifunza dikteta akiwa madarakani, raia wake hawana uhuru wa kukosoa serikali yake, wala hamruhusiwi kupinga nyie kila kitu jibu ndiyo mkuu. Nikihusanisha kile nilichokisoma darasani sina shaka ndicho kinachofanyika sasa nchini kwangu Tanzania. Ukikosoa serikali jiangalie sana maisha yako yapo shakani, unakaa kwa hofu, utashinda jela.

Dikteta akiwa madarakani huteka vituo vya habari, na huwa na mamlaka ya kuzuia habari fulani na kuwapa habari za kutangaza, Hali iliyotokea Clouds ndicho kinachonifanya nihusishe nilichosoma darasani na uhalisia wa uwepo wa udikteta nchini.

Udikteta tulijifinza ni stage unaanza kidogo kidogo mwisho hufikia hatua ya juu zaid. Kweli sasa yale tuliyojifunza kwa nadhalia darasani tunayaona kwa vitendo, Somo linaingia vizuri kichwani lakini madhara yake makubwa siku zijazo.

Vyombo vya habari na watanzania kwa ujumla bila kuogopa tupinge hali hii, dikteta akiwa madarakani ni vigumu sana kumtoa madarakani. Tumejifunza Darasani kuwa madikteta wote waliowahi kutokea dunia wengi wao walikufa wenyewe au la walitolewa kupitia mapinduzi. Tanzania yetu hatutaki tufike huko bora tuanze kupaza sauti kabla hali haijafikia katika kiwango cha kati na mwisho juu kabisa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Hivi kichaa alipataje nafasi ya kutawala nchi.

Natamani nisikie anaumwa,amefariki au kupata ajali mbaya.

Natamani nipate connection na mataifa yenye nguvu ili huyu bundi auawe.

Kwa watumishi Annual Increment na kupanda madaraja hadi lini.

Hizo pesa sio zako Sizonje ni kodi zetu.

Hivi ilikuwaje kichaa akapewa nchi.
 
Sio la kweli hilo tangazo
IMG-20170324-WA0021.jpg
 
Back
Top Bottom