MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,184
- 5,435
Wanasema kuishi na kuwa na pesa ni ujanja tu.
Hapa Tanzania wale waliosoma shule wakawa wanashika nafasi za kwanza na za pili darasani hupelekwa kusomea mambo ya engineer wakavumbua na vitu.
Hawa wanaoshika nafasi za tatu wanaenda kusomea sheria na kuja kuwa mameneja wa hawa maelite wanasayansi.
Kuna hawa wanaoshika nafasi za nne wao hujiingiza kwenye siasa na kisha kuja kuwa mabosi na kuwatawala wote wanasheria na wanasayansi.
Kuna hawa waliofeli hawa wengi hujiingiza katika jeshi na kushika nyazifa kubwa na kumiliki njia za ulinzi hawa wote wakizingua jamaa wanapindua nchi na kutawala wote.
Lakini kuna huyu mtoro wa shule aliyekimbia shule yeye hujiingiza ktk jadi na kuwa mganga wa jadi kwa hiyo mwanasayansi, meneja mwanasheria, mwanajeshi humiminika kwake kama msafara wa kikombe cha babu wakapate kinga na watatue matatizo yao kwa njia za jadi na kumwachia mapesa mengi.
Hii ndiyo ecosystem ya elimu Tanzania yetu ndiyo maana unawaona mawaziri wanamwaga vitu vya ajabu ajabu bungeni tena wakiwa wanasheria huulizi wamevitoa wapi gamba laishia kiunoni.
Kutwa kucha mtaala wa elimu haueleweki yaani taifa halijajua linaenda wapi kielimu.
Ndiyo maana ubashite hauishi Tanzania elimu ndogo inaiongoza elimu kubwa.
Tufikie hatua tuishi kisayansi siyo kwa ramli za kitamaduni zisizo na evidential fact or data.
Mbunge anapeleka mswada wa kutaka sayansi ya usafiri wa ungo ihalalishwe aliyajulia wapi yote hayo?
Tusipobadili mtaala wetu wa elimu tutaendelea na matukio zaidi ya ajabu kuliko hata haya.