UCL
Member
- Aug 18, 2020
- 8
- 6
Hii si sauti ya kwanza kupazwa juu ya mfumo wa elimu unaoonekana kupwaya katika kukidhi haja na maono ya watanzania. Ni mfumo tulioachiwa na Waingereza 1961 uliolenga kupata vijana wachache watakaohudumu kwenye Serikali yao tena katika ngazi za chini.
Ni mfumo unaomwandaa kijana wa Kitanzania na mwananchi wa kesho kuwa tegemezi kwa Serikali. Hivi sasa tumeanza kuonja machungu ya funika kombe mwanaharamu apite. Vijana wanaofeli Drs la saba, kidato cha nne na kidato cha sita hawana mchango wowote katika ujenzi wa uchumi wa Taifa hili mbali na kusomeshwa kwa gharama kubwa ikiwemo elimu bila malipo ya ada. Wanaomaliza Elimu ya kati na Vyuo vikuu wamekuwa wakitembea barabarani kutwa nzima na bahasha mkononi wakisaka ajira utafikiri ni watumishi wa Tanroad wanakagua barabara. Wasomi wamekuwa wengi mtaani lakini wanaobahatika kupata ajira ni wachache
Mbaya zaidi sasa wanaambiwa eti wajitolee maeneo waliko ili Serikali iwafikirie kuwaajiri. Mfumo huu una tofauti gani na Wajumbe? Mtoto aliyetoka kisiwa cha Ukara na akasomea mambo ya gesi atajitolea kwenye kiwanda gani Ukara kama siyo kushughulika na gesi itokanayo na kinyesi cha ng'ombe (Bio-gas)?. Hii si tu kwamba ni kadhia bali pia utumwa wa kifkra
Watanzania zaidi ya million 55 wanahitaji mfumo mpana wa elimu (Extensive Educational System). Mfumo rafiki utakaokidhi hitaji lao na kukata kiu waliyonayo. Mfumo huru utakaotoa fursa kwa vijana wetu kurithishwa maarifa na stadi juu ya biashara, kilimo, ufugaji uvuvi, madini, utalii n.k shughuli ambazo hufanywa na jamii wanamotoka. Mfumo huu utapunguza umaskini tulionao na utawapa thamani hata wanafunzi wanaofeli kuendelea na ngazi za juu za elimu.
Watu kama Mhe. Kishimba na wengineo, tafadhali wasichukuliwe kama wachekeshaji. Ni hoja inayopaswa kuchukuliwa kwa uzito na umakini wa hali ya juu kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa hili na watu wake. Wanaoumizwa na mfumo huu ni wengi sana ila wapatao fursa ya kuwasilisha machungu wanayoyapitia ni wachache. Tusipochukua hatua sasa yajayo hayafurahishi hata kidogo.