Mfumo wa elimu na ukosefu wa ajira na madudu ya TAMISEMI

Emmanuel180

JF-Expert Member
Dec 17, 2019
342
626
Mfumo mbaya wa elimu ukosefu mkubwa wa AJIRA kuendelea na yale yale ambayo yalianzishwa na wakoloni ukosefu wa katiba mpya yenye kulenga mahitaji muhimu na ya msingi ya kupunguza madaraka ya rais na kuvipa nguvu baadhi ya vyombo Muhimu ya kusimamia na kupambana na rushwa ndio sababu kubwa ya umasikini na ukosefu wa ajira kubwa kwa vijana na kushindwa kuenjoy nchi yao.

Kuna tatizo kubwa sana la ajira tatizo kubwa mno tatizo ambalo kama halitatafutiwa ufumbuzi wa haraka ni bomu kubwa ambalo serikali inalitengeneza na sijui kwa kulitatua.

Serikali inaweza ikafanya mengi mazuri lakin nataka niseme serikali hii utaonekana haijafanya la maana kama haitawatendea haki na kuwapa ajira wasomi iliowatengeneza ukosoaji mkubwa unafanyika kutoka kwa wasomi hawa hawa waliokosa cha kufanya ndio maana kuna muda unakuta baadhi ya mitandao inafungwa kwasababu wasema kweli wamekua ni wengi.

Serikali inaendelea kuamini watanzania wa leo ni sawa na wa miaka 10 au 20 iliopita hapana unapo mpa mtu elimu yenye utegemezi wa kuajiriwa na usimuajiri unampa room ya kuhoji ku reason mambo mengi ambayo hasira yake inatokana tu na mambo machache ulioshindwa kumtimizia.

Mfumo huu huu wa elimu ambao serikali inatengeneza utaendelea kuikosoa serikali kwa makelele mengi mtandaoni na badae kilio cha wengi kitakua kikio cha Mungu.

Rai yangu kwa mamlaka inayosimamia elimu kubadili mfumo huu hasi huu ambao unaendelea kuzalisha product ambazo ni useless mtaani.

Nashangaa kila siku serikali inajisifia ufaulu unaongezeka tena juzi wamefikia muda wameongeza na combination so what? Unaongeza mpk na combination then mtu aje kua jobless au kusoma kumekua kama desturi tu kwamba lazima tusome na hii ndio inayonipa mashaka na wateule wanaoaminiwa na rais kusimamia mambo kama haya wanashindwa hata kumshauri raisi kubadili mfumo huu ambao haumsaidii mtu kupata uwezo wa kujiajiri.

Mtoto wa kitanzania anasomeshwa na HELSB anakopeshwa baada ya miezi 24 kama hajaanza kurejesha mkopo riba inaanza kuongezeka huoni kama huu ni unyonyaji ni mtu gan ambaye kama angepata kazi within ashindwe kulipa hio pesa?

Waziri wa TAMISEMI na ELIMU waliangalie hilo.

Kama tumeamua kufata mitaala ya wazungu isiyokua na manufaa it's better tukae mtaani wanetu wasisome ili hali kama kuna we watu wanasoma then wanaambiwa wajiajiri ni kama kupotezeana muda mtu anafikisha 24 yrs hajui hata kulima.

By the way kusoma ni investment kama walioamua kufanya biashara tu sasa kuna umuhimu gani wa ku-invest kwenye biashara ambayo haiwezi kukulipa?

Serikali iliangalie hili suala upya.

Nchi zilioendelea kama marekan Vyombo vyao kama FBI na CIA vimepewa nguvu kubwa nje ya serikali kuhakikisha taifa liko salama katiba ya marekani haimpi nguvu raisi kwenye kila kitu kuna maamuzi ambayo lazima bunge likae kuridhia nchi yetu raisi anakua kama Mungu akiamka asubuhi akasema wote mfagie woote mnaingia mzigoni kesho akisema mnywe ulanzi woote vilabuni kiufupi president anapewa mamlaka makubwa kiasi kwamba akija kichwa maji maji tutauta mma.

Katiba lazima tubadilishe haiwezekan katiba yetu inasema raisi akifanya madudu asishtakiwe we uliskia waapi?
 
Hii leo kazi ya ulinzi wanataka cheti cha form4 udereva wanataka cheti cha form4 unaposema tuondoe huu mfumo unatuweka mashakani mkuu
 
Hii leo kazi ya ulinzi wanataka cheti cha form4 udereva wanataka cheti cha form4 unaposema tuondoe huu mfumo unatuweka mashakani mkuu.
Sijakataa mfumo huu ubadilishwe uwe na tija kama elimu haimuandai mtu kajiriwa basi kutengenezwe mtaala utakao muandaa mtu kujiajiri toka udogoni somo la entrepreneurship tunasoma chuo tu na ni option sio lazima huon unatesa watu.
 
Kama mzee aliyeenda zake , ni rais ambaye hakuwa muelewa kuliko marais wote ambao wamewahi kutokea Tanzania.

Totally elimu yetu inatuandaa wahitimu kuajiriwa, na ndio maana utawaona wabunge wanapambana kugombea miaka 20 mpaka wengine wafie bungeni, pamoja na kupata hela nyingi na mishara mikubwa ndani ya miaka mitano hutokuja kusikia mbunge akisema hii mitano inanitosha sasa nikajiajiri kwa kufanya shughuli nyingine.

Wengi wanaonga ili wapate vyeo na kusema watu tujiajiri lakini watoto wao wanatengenezea chaneli za kuajiriwa.

Ngozi nyeusi sijui inamapungufu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno meeeengi,unapoongelea katiba hata katiba ikibadirishwa uchungu wa hiyo katiba mpya utauona tu, kama si wewe basi hata mtu mwingine atauona, katiba ni sheria na usidhani inakuja kumfurahisha kila mtu nchini,msiwe wajinga sana...ukiona kumekuja katiba mpya usijidanganye kwamba matatizo yaimeisha.
 
Sijakataa mfumo huu ubadilishwe uwe na tija kama elimu haimuandai mtu kajiriwa basi kutengenezwe mtaala utakao muandaa mtu kujiajiri toka udogoni somo la entrepreneurship tunasoma chuo tu na ni option sio lazima huon unatesa watu.
Unajua Nyerere alikua ni Great thinker huenda angekuwepo tungeona mabadiliko kwenye hii secter ila mimi nawewe tukitoa mawazo yetu hayamati sana.
 
Maneno meeeengi,unapoongelea katiba hata katiba ikibadirishwa uchungu wa hiyo katiba mpya utauona tu,kama si wewe basi hata mtu mwingine atauona,katiba ni sheria na usidhani inakuja kumfurahisha kila mtu nchini,msiwe wajinga sana...ukiona kumekuja katiba mpya usijidanganye kwamba matatizo yaimeisha
Hatutajutia kwa sababu mioyo itatusuta kila aliyeitaka moyoni mwake,Hivyo ije tuu📕📕📕Katiba mpya.
 
Kama mzee aliyeenda zake , ni rais ambaye hakuwa muelewa kuliko marais wote ambao wamewahi kutokea Tanzania.

Totally elimu yetu inatuandaa wahitimu kuajiriwa, na ndio maana utawaona wabunge wanapambana kugombea miaka 20 mpaka wengine wafie bungeni, pamoja na kupata hela nyingi na mishara mikubwa ndani ya miaka mitano hutokuja kusikia mbunge akisema hii mitano inanitosha sasa nikajiajiri kwa kufanya shughuli nyingine.

Wengi wanaonga ili wapate vyeo na kusema watu tujiajiri lakini watoto wao wanatengenezea chaneli za kuajiriwa.

Ngozi nyeusi sijui inamapungufu gani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Bora wakoloni wangekuja tu tuwakabidhi nchi tuishi kama wa sauzi tupambane na rascism kuliko kusikiliza mambo haya ya CAG
 
Tanzania tanzania! Ewekwako waziri mwenye dhamana na Tamisemi kwa sasa nakuomba acha kufanya kazi kwa mihemuko yakutaka kumfuraisha aliye kuteua pasipo kusoma nyakati ya utawala. Mh. Rais wa sasa hataki mijisifa kama aliyekufundisha kusema ukweli usoni na sio moyoni. Nimekufuatilia hotuba zako mbili na nimegundua bado unakaelement ka legacy ya hayati ktk kutoa maamuzi. Naomba fata sheria za utumishi na sio kufanya kazi kwa mihemuko.
 
Tuwape muda.. Change is a Gradual process..
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom