Mfumo wa elimu mbovu - hukomoa watahiniwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa elimu mbovu - hukomoa watahiniwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Candid Scope, Feb 27, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mfumo wa wa elimu nchini tofauti na ule tulioridhi toka kwa wakoloni, na wanasiasa wanachezea elimu kama siasa badala ya kujenga mfumo wa elimu usiobadilika badilika.

  1. Mabadiliko ya mara kwa mara katika mfumo wa elimu na mitaala huyumbisha wanafunzi na walimu na hivyo kuto kuwa na mwafaka wa mtiririko wa mfumo wa elimu kwa miaka mingi.

  2. Mfumo wa kutahini wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne ni ukandamizaji zaidi kwa vile walishafanya mitihani ya kidato cha pili, iweje watahiniwe kwa mfumo wa miaka minne? Wanafunzi wa kidato cha nne wanatakiwa watahiniwe kutoka mwaka wa tatu na wa nne na hivyo kutawapa wanafunzi uwezo wa kujizatiti katika miaka miwili ya mwisho.

  3. Utaratibu wa ufundishaji wa kuwafanya wanafunzi kukariri badala ya kuelewa ni tatizo kubwa. Wanafunzi wengi hawana uwezo wa kukariri yote wanayofundishwa kwa miaka minne, badala yake mitihani ingetungwa kupima uelewa wao kwa masomo wanayofundishwa.

  4. Record za majaribio na mitihani ya mihula kama ingekuwa inafanyiwa tathmini ya kutosha wanafunzi wengi wasingeshindwa mitihani kiasi hicho. Inaonyesha kwamba matokeo hutegemea tu final exam. Vinginevyo walao wengi wangeangukia kwenye dalaja la nne ambalo ni kifuta jasho.

  5. Shule nyingi za kata zimeanzishwa kisiasa bila kujali ubora wa elimu, kwani shule hizo hazina vifaa na madarasa ya kukidhi matakwa kielimu na hivyo kuwa wahudhuriaji zaidi shuleni. Ni mtindo wa kimaskini kuzaa watoto wengi kwa mpigo bila kujali ubora wa maisha na malezi.

  6.Kukosekana kwa upimaji wa kiwango cha walimu kama ilivyozoeleka mfumo wa elimu ya kikoloni, hivyo wengi wa walimu wana kiwango cha chini mno na hawafai kufundisha.

  7. Mfumo wa uliozoeleka kutoka ngazi za juu kisiasa wa kuweka mbele kufahamiana kwanza ndio ulioongeza kudondosha kiwango cha elimu.

  Kuna mengi, naomba wanajamii forums kuchangia kwani anayeathirika na mfumo mbovu huu wa elimu ni sisi watanzania wote na kizazi kipya ndio zaidi.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Elimu ni siasa au siasa sehemu ya elimu?
   
 3. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Elimu ni sekta nyeti inayotakiwa kutiliwa mkazo kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake siasa zibaki kama siasa na elimu isiingiliwe na wanasiasa kubadili mitaala kama ovyo kama walivyofanya JK na Lowasa
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa miaka kadhaa tangu tupate uhuru elimu imepitia mabadiliko ya mara kwa mara na mengi ya mabadiliko yasiyoleta matunda bali kuyumbisha wanafunzi, walimu na wazazi. Mabadiliko ya mara kwa mara hayawezi kujenga msingi mzuri wa elimu
   
Loading...