Mfumo ni Muhimu kuwa Imara kuliko Watu!

nkulikwa

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
721
813
Maisha ni mifumo bila mifumo hakuna maisha. Mfumo wa hewa,wa chakula, wa damu na mfumo wa kutoa uchafu! Hata uoge namna gani au uwe na akili kiasi gani bila mfumo umekwisha na uhai wako lazima utoweke; kwa kifupi basi uhai ni mfumo thabiti na wenye kufanya kazi!

Vilevile katika nchi, uhai wake na ustawi wake unategemea mno mfumo thabiti; mfumo wa kupata viongozi; mfumo wa kuwajibisha wakikosea; mfumo wa kutoa haki na mfumo wa kustawisha jamii!!
Mahali popote pale ambapo kuna maendeleo na ustawi ujue kwamba mifumo inafanya kazi kama ilivyojengwa na ukikuta mahali mambo yako ovyo jua mfumo ni mbovu! Mfano mfumo WA akili ukienda nje kidogo lazima uwe mwehu maana mfumo hauko sahihi!

Bahati mbaya kwa Tanzania ni kwamba huwa tunahangaika na Watu badala ya mfumo. Tunaweza kusema Raisi huyu bwana hafai kumbe siyo yeye ni mfumo ndiyo wenye kuleta matatizo kwa wananchi. Mkiwa na Raisi mzuri sana lakini anafanya kazi kwenye mfumo wa ovyo lazima awe wa ovyo Maana siyo yeye ni mfumo wa ovyo.

Kwa nchi mifumo ya nchi iko kwenye katiba. Maana yake mkiwa na katiba mbaya lazima muwe na watawala wa ovyo kabisa; wanasheria wanajua hili kwa uwazi kabisa: mwalimu Nyerere pia alijua na alionya juu ya hili.

Mkiwa na mfumo ambao viongozi wana uhakika wa kufanya lolote na wanajua hakuna hatua zozote zinaweza kuchukuliwa zidi Yao hawana sababu ya kuogopa hata kidogo Maana wanaamini kuwa kama watawala wanavyotaka watatenda hivyo hivyo na hamuwezi kuwafanya kitu chechote wanajua hivyo. Mkiwa na bunge ambalo waziri ana uhakika wa kusema lolote na akapigiwa makofi ;hawezi kujiandaa sana Maana ana uhakika hakuna wa kumfanya lolote; mkiwa na Mbunge anaweza kutukana na akapigiwa makofi na wenzake hawezi kujifunza kujenga hoja Maana ana uhakika na makofi kwa wingi. Mwisho siyo makosa Yao ni mfumo.

Mkiwa na wapinzani wanaodhani shida na taabu ni Watu hawezi kutawala hata siku moja Maana shida siyo hao Watu pamoja na madhaifu Yao shida ni mfumo dhaifu au mbovu au usioeleweka kabisa! Lazima kuanza kutumia akili kwa weredi mpana na wa hoja. Tunahitaji maendeleo, tunahitaji ustawi hivi vyote haviwezi kuja kwa sababu ya Watu hata kama ni muhimu kiasi gani unahitaji mfumo wa kitaasisi Maana Watu hutoweka!! Lazima uwe na mfumo wenye kuchuja Watu!

JK alijua hili akataka kuja na mfumo wa katiba mpya;bahati mbaya wanaojua Maana ya mfumo walikuwa wachache na wenye dhamira ya Kweli na Tanzania walikuwa wachache pia. Wengine walikuwa wanawaza madaraka, utawala na uongozi bila kuwaza ustawi wa taifa la Tanzania kwa vizazi vijavyo. Hata wanaotetea kitu kibovu ni kwa sababu wana matumaini ya uongozi kwamba ipo siku na wao zamu Yao itafika; kumbe kungekuwa na mfumo bora kabisa wanaweza kufaidi Leo na wala siyo kesho.

Ukisema ngoja niwanyoshe unaweza kuwa na dhamira njema kabisa na kusudi bora kabisa la kuwanyosha lakini bila mfumo unawakomoa tu na matokeo yake ni kuleta utepetevu na unajisi na kani ya kushindana. Matokeo yake hayatakuwa kama dhamira inavyotamani. Bunge likiwa mbovu hakuna kinachoweza kunyoka; lazima kuwa na mfumo bora kama tuna dhamira ya Kweli ya kunyoshana ili hata anayenyosha akikosea naye ananyoshwa:

Ni wakati muhimu kuanza kutafakari upya kwa akili na weredi na kujua kwamba siraha yetu kuu ni haki Maana haki huzaa umoja na mshikamano watoto pacha na nguzo muhimu za ustawi wa Taifa. Umoja wetu leo kama taifa ulitokana na mfumo uliojengwa na kusimamiwa vema nachelea kusema kwamba kwa kuwa hatujali mfumo kwa hakika siyo muda kama taifa tutawanyika!! Tujifunze kuishi pamoja katika tofauti zetu; sisi Tanzania moja na maiti wa siku moja!
 
Back
Top Bottom