Mfumo mpya wa simu waingiza mabilioni

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
Magu+pic.jpg


KUPITIA Mfumo wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) Serikali imepata zaidi ya Sh bilioni 93.6 fedha ambazo kama sio mfumo huo zingekuwa kwenye mifuko ya watu. Takwimu hizo zilitolewa Dar ea Salaam jana na Rais John Magufuli wakati akikabidhiwa rasmi mfumo huo ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuthibiti mawasiliano pamoja na mapato ya huduma ya Mawasiliano ya simu hapa nchini.

Rais Magufuli alisema: “Bila kuwa na mfumo huu huwezi kuhakiki mapato yatokanayo ya Mawasiliano ya simu, TRA hawakuweza kukusanya kodi iliyostahili, mtambo huu unahakiki mapato.” Mfumo huo ulikabidhiwa na Kampuni ya TMS na GBG kwa TCRA ambapo Rais Magufuli alisema sasa kila kitu kiko wazi katika sekta hiyo kwani hakuna fedha itakayopotea.

Alisema kupitia mfumo huo kampuni za kutoa huduma ya mawasiliano pia zimenufaika kwa kupata Sh Bilioni 173.93 na mkandarasi Sh bilioni 53.52 na Sh bilioni 13.3 wamepata TCRA kupitia simu za kimataifa. Rais Magufuli aliipongeza TCRA kwa kazi wanayoifanya sasa kwani alipoingia madarakani hakupendezwa na utendaji kazi wao palikua na mchezo mbaya.

“Palikua na mchezo mbaya sana, Tanzania tumeibiwa mno, tumechapwa ukweli, tumeliwa kweli, tumedhulumiwa vya kutosha,” alisema. Alisema 2015 alipoingia madarakani aliamua kuutafuta mkataba wa wakandarasi hao ambapo mkataba halisi ulichwa na kuwa kipengele kilichohusu kukusanya fedha kwenye kampuni za mawasiliano kilichwa hivyo ilibidi atumie vyombo vya ulinzi akaupata mkataba huo. “Nilichofanya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Simba nikatengua uteuzi wake nikamtoa kwanza tukapeleka mabadiliko kwenye Bunge na Spika na watu wake wakakiweka kipengele kilichokua kimefutwa kwa ujanja ujanja uliofanywa na baadhi ya viongozi waliokuepo serikali ni,” alisema Rais Magufuli.

Alisema baadaye mkandarasi aliamriwa kurudi kukamilisha kipengele kilichochwa kwenye mkataba na baada ya kutimiza sasa wamekabidhi kazi. Rais Magufuli alisema aliongeza mkataba wa miaka mitano zaidi kwa mkurugenzi Mkuu wa TCRA ili aendelee kufanyia kazi mfumo huo. Alisema takwimu za kidunia zimeonesha kuwa sekta ya Mawasiliano ni nyeti na muhimu na inakua kwa kazi duniani, zaidi ya watu bilioni tano wanatumia simu duniani kote na wanaotumia data ni milioni 3.9 na kwa Tanzania, wanaotumia simu ni zaidi ya watu milioni 42 .

“Biashara nyingi ya rejareja zinaendeshwa kwenye mitandao na kwa mwaka 2017 biashara hiyo iliyofanyika kwenye mitandao zilikua na thamani ya dola za Marekani trilioni 2.3 kupiku biashara za kwenye maduka makubwa na maduka ya kawaida,” alisema rais. Aidha alisema sekta ya mawasiliano imewezesha kupatikana kwa huduma ambazo awali hazikuwepo mathalani afya, elimu, usari wa teksi, kibenki ambapo zaidi ya watu milioni 20 wamejiunga na huduma za kibenki mitandao na pia ndio uliosaidia serikali kungia simu hafu milioni moja na kufahamu vifaa vyote vinavyotumia mtandao. Alisema sekta hiyo imetoa ajira zaidi ya milioni 28 za moja kwa moja na kufanya sekta hiyo kuitwa kisima kipya cha mafuta au mgodi wa madini.

Hata hivyo, alisema sekta hiyo inachangamoto zake ambazo ni pamoja na uhalifu wa mtandao na kuathirika mila na desturi. “Kukabiliana na changamoto hizi serikali imekua ikianzisha mamlaka na mfumo mbali mbali kudhibiti na sisi tumeanzisha mamlaka kutunga sera, sheria na kuweka miundombinu pamoja na mfumo huu wa TTMS kufatilia takwimu za Mawasiliano,” alisema. Rais Magufuli pia alitoa mwito kuujengea uwezo mfumo huo na kuusimamia isitokee yaliyotokea katika mfumo wa kukusanya kodi wa TRA, EFD.

“Wote tunajua yaliyotokea katika mfumo wa EFD, mtambo haukua Tanzania lakini sasa tumebadili uko hapa nchini nchini ya Wizara ya Fedha,” alisema. Rais aliagiza pia taasisi zote za serikali ambazo zinahusika na ukusanyaji mapato ya serikali kutengeneza mfumo wa kukusanya mapato na pia kuunganishwa na mfumo wa taifa. “Kati ya taasisi 667 ni taasisi 339 tu zimeunganishwa, Waziri wa fedha nataka uwaandikie barua nakala apewe Waziri Mkuu na mimi nipewe nakala yangu ili niweze kufuatilia,” alisema. Rais Magufuli pia aliwashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kumuombea na kuongeza kuwa vita ya uchumi inahitaji maombi na kuwa matatizo yaliyopo sasa serikali hii isipoyatatua hayatatatuliwa tena.

Akizungumzia mfumo huo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema kukamilika kwa mfumo kumewezesha kuonesha taarifa mbalimbali zinazopita katika Mawasiliano hapa nchini. Aidha, alisema Mfumo unaiwezesha TCRA kupata takwimu za Mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje, kuhakiki mapato ya watoa huduma, kupata takwimu zinazohusiana na huduma za mawasiliano ya sauti, data na ujumbe mfupi, kubaini Mawasiliano ya ulaghai, kutambua takwimu za fedha za mitandaoni na kusimamia ufanisi na ubora zaidi viwango vya mawasiliano kwenda kwa watoa huduma, kuwasililisha mapato ya Mawasiliano ya kimataifa.

“Toka mwaka 2013 mfumo ulipoanza kufanya kazi mpaka Septemba 2018 serikali imepata chanzo kipya cha Mawasiliano yanayotokana na Mawasiliano ya kimataifa zinazoingia na kuishia hapa nchini na kiasi cha Sh bilioni 93 ziliwasilishwa serikalini,” alisema. Aidha alisema pato la kodi limeongezeka na kwamba simu za kimataifa zilikua zinaingia kiulaghai.

Mfumo umewezesha kubaini watu wenye mfumo mingine ya ulaghai kuingiza simu za nje kukishwa kwenye vyombo vya sheria, sasa simu zinazoingia kwa njia za ulaghai ni asilimia kumi wakati awali zilikua zaidi ya asilimia 60. Malaba alisema sasa TRA na BOT zinapata taarifa ya kiasi cha fedha na kuwa awali zilikua Sh trilioni nane kwa mwezi na kwa mwaka jana kukia Sh trilioni 11.

Mkurugenzi huyo aliahidi wataendelea kuboresha mfumo huo kutanua wigo ili kuendelea kutoa huduma na kuongeza mapato kwa serikali ambapo aliahidi mamlaka hiyo kuutunza mfumo wa TTMS. Alisema chimbuko la kuanzishwa mfumo huo ni Bungeni baada ya malalamiko ya gharama za simu zinazoingia nchini kushuka kila kukicha hali ambayo ilipunguza mapato kwa watoa huduma na pia kodi kwa serikali na mchango katika uchumi.

“Ilionekana hitaji la mfumo huu, TCRA ilisimamia manunuzi ya mfumo huu na Machi 22, 2013 kwa lengo la kutekeleza mradi ikiwa ni kujenga kuendesha na kuhamisha umiliki Octoba mosi 2013 mkataba wa miaka mitano Septemba 2018 mkataba huo umemaliza muda wake,” alisema. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema gharama ya kuunganisha mitandao imepungua kutoka Sh 30.58 iliyokuwepo mwaka 2015 hadi kukoa Sh 10 kwa dakika kwa mwaka huu na itaendelea kupungua ike Sh mbili mwaka 2022. Alisema ilani ya Chama cha Mapinduzi ilielekeza kulinda wananchi dhidi ya wizi wa mtandao ambapo wanaendelea kusajili kwa kutumia alama za vidole kuendelea kuzuia wizi huo.
 
Mh. Sana amekuwa mzungumzaji wa kila jambo kiasi kwamba hatuelewi lipi sahihi na lipi sio sahihi.

Siasa kwenye mambo ya kitaalam zinatosha sasa.
Wakati umefika wazungumze wataalam wa nyanja husika ili waweze kuulizwa maswali. Maana akishazunguza huyu mheshimiwa inakuwa kama amri za muumba, hahojiwi.
 
Hizi billioni 53.52 alizolipwa mkandarasi ni kwa kazi gani? yaani kuweka tu king'amuzi ndo anavuta hesabu ndefu hivyo?
 
Back
Top Bottom