Mfumo huu wa uchaguzi unabinya Demokrasia


Alexism

Alexism

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Messages
2,502
Likes
1,061
Points
280
Alexism

Alexism

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2011
2,502 1,061 280
Hili Demokrasia iwepo na kukua ni lazima uwepo uchaguzi huru,wenye usawa na uwazi.Hii ni misingi muhimu katika Demokrasia ingawa waweza kuwa na uchaguzi bila Demokrasia.
Kuna chaguzi nyingi zinafanyika hapa Tanganyika pamoja na nchi ya Zanzibar lakini zinanipa mashaka makubwa.
Mfano maye(mayor) au mwenyekiti wa wilaya au halmashauri tuseme.Viongozi hawa wa kisiasa wanaongonza watu wengi na sehemu kubwa lakini wanachaguliwa na watu wa chache ambao ni madiwani.
Hapa tunakuwa tumebinya ushiriki wa watu kwenye decision making kitu kinachowafanya hawa viongozi wasiwajibike ipasavyo.
Madhara yake mayor anakuwa kama premier au symbol tu,uwajibikaji hamna kwani wananchi hawajamchagua wenyewe na yeye pia anajisahau kwani hakuna pressure kutoka kwa wananchi.
Nadhani tungeiga mfumo kama huu wa Uganda ambapo maye,katibu tarafa,mwenyekiti wa halmashauri wote wanachaguliwa na wananchi.
Je mfumo unafaa kuukumbatia?tujadiri na tuje na tiba mbadara.
 

Forum statistics

Threads 1,236,267
Members 475,050
Posts 29,252,161