SoC03 Mfumo dhibiti wa maafa yatokanayo na vyombo vya moto pamoja na uhalifu unaohusisha matumizi ya vyombo vya moto

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
996
1,512
UTANGULIZI
“POSATRAS”
ni mfumo dhibiti wa majanga na uhalifu yanayosababishwa na vyombo vya moto kama vile pikipiki, na magari ya aina zote.

Lengo la mfumo ni kudhibiti majanga yanayotokana na vyombo vya moto, pia kudhibiti uhalifu unahusisha vyombo vya moto.

MUUNDO WA MFUMO.

VIFAA CHUNGUZI.
GPS, Kidhibiti mwendo, CPU, kizima/kiwasha injini, kipokea na kituma taarifa, kitoa tahadhari,
hivi vyote vitaunda (Safer) ambayo haitaweza kufunguliwa, itafanya kazi ya kusoma mahali kifaa kilipo, kudhibiti mwendo kasi, kupokea na kutuma taarifa za mienendo ya kifaa cha moto kwenda kwenye mfumo wa compyuta, kutafsiri alama na sheria za barabarani, na kutoa taadhari.

Kamera;
ni ndogo sana ambazo si rahisi kuziona, hazitaunganishwa na waya, taarifa kutoka kwenye kamera hizi zitapokelewa na “Safer” kwa kupitia kipokea taarifa, zitakuwa na uwezo mkubwa wakuchukua matukio katika ubora.

Pikipiki itakuwa na kamera mbili, moja kwenye kioo (maalumu) cha upande wa kulia na nyingine maeneo ya taa kubwa ya mbele na gari itakuwa na kamera tatu, mbili mbele, na moja nyuma.

Skana ya alama ya vidole; itamtambua dereva anayeenda kukitumia kifaa hicho kwa wakati huo kwa kutumia alama za vidole hivyo inapelekea kuwa na leseni ya udereva ya kielektroniki, hatua ya awali ya dereva itakuwa ni kuweke kidole chake kwenye skana ili atambuliwe,bila ku-skani dereva hataweza kufanya chochote.

Satelaiti; itawezesha mawasiliano kati ya (Safer) na mfumo wa kompyuta ambao utakuwa unatumika kuchambua matukio yote na kufanya maamuzi “Automatically”

“Server” kuhifadhi matukio yote muhimu yanayotumwa na (SAFER).

Mfumo hakiki na chambuzi wa kompyuta; kazi yake itakuwa ni kupokea, kuhakiki, kuchambua na kufanyia maamuzi taarifa zote muhimu zinazotumwa na “Safer”, utawawezesha maofisa wa jeshi la polisi kufuatilia mienendo ya vyombo vya moto barabarani, na uhalifu mwingine uliohusisha chombo cha moto, kupitia mfumo huu wataweza kujua wapi tukio limetokea, nani kasababisha pia wanaweza kuona mwenendo mzima wa chombo cha moto kinapokuwa kinatumika.

App ya simu itatumiwa na wamiliki wa vyombo vya moto kujua makosa waliyotenda na kupelekea kifaa kuzima, na kufanya malipo ya kosa.

Mfumo utafanya kazi kwa kujiongoza wenyewe kwa kanuni kwamba ikitokea kanuni yeyote ama sheria ya barabarani moja wapo ikavunjwa ama alama ya barabarani haikuzingatiwa Basi mfumo utatambua “SIO”, na baada ya dakika 10 za taadhari kifaa cha mtumiaji kitazima chenyewe kwa kusimamisha mtiririko wa umeme katika kifaa na kuzuia injini na hakitaweza kuwaka mpaka pale mfumo utakapo soma “NDIO” kwa kulipa faini, pia chombo hakitaweza kuwaka kama dereva hajafuata miongozo ya usalama kabla ya kuanza kukitumia.

Vyombo vyote vya moto vitasajiliwa makao makuu ya jeshi la polisi katika kila wilaya na kufungiwa vifaa tambuzi, usajili utafanywa kupitia mfumo wa kompyuta, baada ya kukamilika kwa usajili watapewa muongozo wa namna ya kutumia.

UUNGANISHWAJI WA VIFAA TAMBUZI.
Vifaa vitatambuliwa na mfumo wa kompyuta kwa kupitia namba tambuzi iliyopo katika boksi husika na vifa ambatanishi.

“Safer” ndio kifaa ambacho kinakamilisha muunganiko kati ya mfumo washi na mfumo endeshi wa kifa chamoto, Kamera, skana ya alama za vidole na mfumo wa kompyuta kwa kupitia satelaiti

Itaunganiswa na mfumo washi (IS) wa kifaa chamoto, kwenye sakiti sekondari na itapata umeme kupitia mfumo huu pia na kwa upande wa vifaa vinavyotumia umeme itaunganishwa kwenye kifaa ongozi nguvu za kielektroniki (PEC).

Kamera na skana ya alama za vidole zitawasiliana na “safer” kupitia kipokea taarifa (Receiver).

UTENDAJI KAZI.
Utendaji kazi unafanana kwa kiasi kikubwa kwa vyombo vyote, utofauti upo katika hatua za awali wakati wakuwasha kifaa, katika pikipiki baada ya dereva kuwasha swichi ya pikipiki “Safer” itaamka na kuna sauti itasikika ikiashikika kama kila kitu kipo sawa ama havipo sawa (sauti tofauti), pia “LED” zitaonesha, dereva ataweka kidole chake kilichotumika kusajili leseni, mfumo utamtambua na ataona jina lake na namba yake ya leseni.

Dereva atatakiwa kuvaa kofia ngumu, kikinga kifua, na kama anambeba abiria ni lazima nae avae kofia ngumu, haya yote yatakuwa yanahakikiwa na “Safer” kwa msaada wa kamera ambayo itakuwepo katika kioo cha upande wa kulia, kioo hiki kitakuwa kimetengenezwa maalumu na kitakuwa kimefungwa kamera kwa ndani, baada ya kukamilisha yote, ASS itajiwasha na kuruhusu sehemu za mfumo washi kuwa katika muunganiko na hapo dereva anaweza kuwasha injini na kuondoka.

Katika gari dereva akisha skani alama zake za vidole, atatakiwa kufuata kanuni zote kwa ufasha ndio ataweza kuiwasha gari.

Matukio yatarekodiwa na kamera ambazo moja itakuwa ikichukua matukiio ya mbele na nyingine ya nyuma kwa upande wa pikipiki na kamera mbili zitachukua matukio upande wa mbele na moja nyuma katika gari, na kuyatuma kwenye CPU” ambayo itakuwa na uwezo wakuzitambua alama zote za barabarani kwa kuhusisha sheria zote za barabarani, “Sender” itatuma taarifa iliyochambuliwa kwenda mfumo wa compyuta kwa msaada wa satelaiti na kuhifaziwa katika “Server” na uchambuzi zaidi na kurudisha majibu kwenye “CPU” na itatafsiri mrejesho na kupeleka maamuzi sehemu husika kama ni kidhibiti mwendo, kitoa taadhari au ASS.

Taarifa zinazohusu mwendo kasi zitaambatana na taadhari hivyo kidhibiti mwendo na kitoa taadhari vitapata taarifa kwa pamoja, taarifa zote za onyo ama ya kujiandaa zitaenda kwenye kitoa taadhari ambacho chenyewe kitatoa taarifa kwa mfumo wa sauti.

Mfumo utafanya maamuzi kwa kupima uzito wa kosa, ama si kosa, kutakuwa na makosa ambayo yatahitaji onyo kwa mara tatu ndipo litambuliwe kama kosa linalostahili adhabu, na kuna yale ambayo yatatambulika kuwa ni hatari moja kwa moja, kisha utasikika mlio mwingine ambao utahitaji kuweka kifaa pembeni, ambao utafuatiwa na mlio mwingine kwa kuhesabu na dereva atalazimika kuweka kifaa pembeni haraka, ikifika hatua ya kumi kifaa kitazima wakati huo taarifa ya makosa itakuwa imerekodiwa na hakitaweza kuwaka tena mpaka kosa lifutwe.

ASS” ndio itakayozimisha na kuwasha injini, itafanya kazi kwa kutumia kanuni ya “BOOLEN” ambapo majibu yakifika “NDIO” itawaka ama itaendelea kuwaka na yakiwa “SIO” itazima

Kidhibiti mwendo (SG) kitadhibiti mwendo kulingana na maeneo ambayo mfumo utakuwa unahakiki kwa msaada wa kamera kwa kuzingatia alama za barabarani, mfano ikitokea ni eneo ambalo haliruhusiwi kutembea zaidi ya 50km/hr basi chenyewe kitapunguza spidi mpaka 50km/hr ama kitazuia isiongezeke kama ulikuwa chini ya hapo au sawa na hapo, haitaweza kuruhusu uongeze spidi ili ukipite kifaa cha mbele sehemu ambayo alama haziruhusu kufanya hivyo.

Ikitokea mawasiliano kati ya Safer na mfumo wa kompyuta yame feli, taarifa zote zitatunzwa na ubongo wa “Safer” mpaka pale mawasiliano yatakapo rejea, itayatuma kwenye “Server”, hitilafu ya mawasiliano itafahamishwa na mfumo wa kompyuta.

“Safer” itafanya kazi masaa 24 hata kama chombo kimezima na mfumo wa kompyuta utaonesha kama kimezima au kimekatishwa muunganiko na chombo na itaweza kutafutwa ilipo, itakuwa ni kosa kisheri kwa mtu yeyote kukatisha mawasiliano kati ya chombo na “Safer”.
 
Back
Top Bottom