Mfanyakazi wa Startv Cyprian Musiba ameamua kuacha kazi baada ya kutukanwa kwenye mitandao ya kijami

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
tmp_479-Screenshot_2017-05-25-17-47-24102889343.png

My take :Hongera sana rafiki yangu Cyprian Musiba umechukua uamuzi wa busara siku zote lazima usimamie unachokiamini.
 
Uamuzi kuntu. Hongera Sana , huyu jamaa ni mjita kina "musiba" ni watu wa musoma Mwanza Hasa wajita (naweza kusahihishwa).

Sasa sijui jamaa alisoma Uzi Flani hapa ulikuwa una zungumzia makabila ambayo watu wake wana msimamo mkali esp wakitakiwa kutenda kinyume na msimamo yao, nadhani wajita walikuwepo. Ingawa hawa Ndugu zetu nao kwa ubishi nawakubali sana.

Ingawa mjita mwenzio "prof. muhongo" kachemka. Wan musoma wamesikitishwa Sana.
 
Kama sababu ni kutukanwa mitandaoni naona kama huyu ni mtu DHAIFU SANA, mtu strong husimamia anachokiamini hata kama ni kwa gharama ya kutukanwa,na kama aliamini kumhoji RC huyo si jambo sahihi alitakiwa ajiuzulu hata kabla ya kumhoji na sio kusubiri atokanwe kwanza ndipo ajiuzulu.
Lakini kama amejiuzulu kwa kukataa kuburutwa nampa big up,kwa taaluma aliyo nayo na kwa kuwa bado kijana bado kuna fursa mbele yake.
 
Uamuzi kuntu. Hongera Sana , huyu jamaa ni mjita kina "musiba" ni watu wa musoma Mwanza Hasa wajita (naweza kusahihishwa).

Sasa sijui jamaa alisoma Uzi Flani hapa ulikuwa una zungumzia makabika ambayo watu wake wana msimamo, nadhani wajira walikuwepo. Ingawa mjita mwenzio "prof. muhongo" kachemka. Wan musoma wamesikitishwa Sana.

Muongo safari hii wamemuonea kwa kweli. Issue za miaka 20 iliyopita duh!Mnyonge mngongeni haki yake mpeni kwenye hili hahusiki
 
Muongo safari hii wamemuonea kwa kweli. Issue za miaka 20 iliyopita duh!Mnyonge mngongeni haki yake mpeni kwenye hili hahusiki
Ndo hivyo tena bulldozer lishapita na kufanya yake
Chamsingi kaangalie michongo mingine maisha yasonge mbele kama kawa kama dawa
 
Soma ujumbe wa mwisho. Nimekataa kuwa mtumwa Mungu anisaidie. Huyo mwandishi wa habari ambaye anaheshimu taaluma yake hana njaa kama wewe unategemea buku 7 kuishi.

Kwanini hakuachia ngazi alipoona matangazo yameanza na mmiliki habadili mawazo kama anavyodai kutafuta tu pakutokea!!!! kweli alimwambia kuwa hatasimia na akaendelea kusubiri nini kuangalia... na bado alisimamia yote na yakajiri baada anakuja kuleta porojo...

Bahasha alipokea kuzuia isirushwe akashindwa, anakimbia kabla hawajamuumbua na sio maneno ya mitandaoni....angeona sentensi mbili tatu na kuignore social networks etc kwani angeyajua yanayojiri...atafute sababu ingine hii katumia kuondokea ya kijingaaaaa hadi nacheka.. hafai tena kuwa kiongozi...kapokea bahasha tangu akashindwa kusimamisha kipindi.

Na bora kaondoka labda hata amejulikana ufitna wake ikabidi kabla ya kufukuzwa.

JPM kasema vita hii ni kubwa na tunamuelewa...

Makonda oyeeeeee
 
Kwani mzee mwinyi alijiuzuru baada ya yale maafa ama kabla ..
 
Issue za mishahara zina sura nyingi ndugu, hapa walau huenda akawa amepata kasababu ka 'kuchomokea'!
 
Back
Top Bottom