Mfanyakazi wa Kihindi afukuzwa kazi nchini kwa kuwaita wafanyakazi nyani

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,796
Raia wa India, Dennis Smith ameachishwa kazi katika Hoteli ya Ramada kwa madai ya kuwatukana wafanyakazi wa ngazi za chini akiwaita nyani.

Smith, ambaye ni meneja wa chakula na vinywaji wa hoteli hiyo, aliwatukana na kuwadhalilisha wafanyakazi hao siku ya Sikukuu ya Wapendanao akiwatuhumu kushindwa kuandaa meza vizuri.

Kutokana na udhalilishaji huo, wafanyakazi wa hoteli hiyo jana waligoma wakishinikiza meneja huyo asimamishwe kazi au wao waache kazi.

Wakizungumza jana, baadhi ya wafanyakazi ambao waliomba majina yao yahifadhiwe walisema tabia ya meneja huyo imekuwa sugu na tukio la juzi lilikuwa halivumiliki. Walisema raia huyo wa India amekuwa mwenye majivuno na kutoa lugha chafu dhidi yao.

“Tumechoshwa, anatuitaje sisi nyani, hii tabia ni ya muda mrefu na sasa hatuwezi kuivumilia,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Mwakilishi wa wafanyakazi hao, Mathew Misalaba alisema bosi huyo amekuwa akiwarushia maneno ya kuwadhalilisha kila wanapofanya makosa hata kidogo.

Alisema licha ya uongozi wa hoteli kuahidi kumsimamisha kazi Smith, wamelipeleka suala hilo polisi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Meneja Rasilimaliwatu wa hoteli hiyo, Sebastian Nchimbi alisema tayari Smith ameachishwa kazi kutokana na tukio hilo.

“Tulizungumza na wafanyakazi wakatuambia kuwa hawataki Smith awepo kazini na sisi tukafanya uamuzi ili kuwalinda wafanyakazi wetu,” alisema.

Alisema waliamua kumwachisha kazi Smith baada ya kupata malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi hao.

“Si tukio la mara ya kwanza na ndiyo maana tulipoona yamezidi tuliamua kuchukua hatua,” alisema.

Hata hivyo, Nchimbi alimsifu Smith akisema ni mtendaji mzuri na alikuwa na tija kwa hoteli hiyo ya kitalii lakini hakuwa na kauli nzuri kwa wafanyakazi Waafrika.

“Kiutendaji ni mzuri mno… yaani kwetu sisi tunapoteza mtu hasa, tatizo ni mdomo tu,” alisema.
 
Pia Wabongo tuache Uvivu,Watu wametoa pesa zao kwenda kustarehe kwny Valentine halafu wahudumu wanaleta uswahili uswahili wa kushindwa kuwajibika mpaka jioni hata meza ya Vinywaji haijaandaliwa!Haikufaa kuitwa nyani ila ilifaa tusi lingine jepesi kidogo! wakiajiriwa wageni kwny hizo kazi tunalaumu wakiajiriwa vijana wetu uwajibikaji hakuna!
 
Mkuu hao waswahili wana tabu sana katika kazi haswa za mahotelini na viwandani, ila bhai hakupaswa kuwatolea lugha mbovu.
HAPANA WAHINDI NI NAMBA 1 KWA UBAGUZI DUNIANI


HALAFU KWAO WALIVYO NA TAABU SASA WANALALA MAJALALANI KUKULIA MAJALALANI WAKIPATA KAZI HUKU WANAJIDAI UTAKUTA UKOO MZIMA NI MACHOKORAA WAFUKUZWE TUU MAANA WENGINE ASILIIA 90 YA WAHINDI NI WANYAYASAJI HIYO KUMI ILI=YONBAKI NAYO NI 50 KWA 50 IDIAMINI DADA ALIWAFANYIA VYEMA
 
Hawa Wahindi kuna wanacho kitafuta na muda sio mrefu watakipata ,Manyanyaso ya Watanzania na hawa jamaa ni mengi sana ni vile tu watu wananyamaza ,Kuongoza Watanzania baadhi unatakiwa uwe na kichwa cha mwenda wazimu pamoja na hayo unyanyasaji wa Kijinsia,ubaguzi wa aina yoyote haukubaliki
 
Mambo mengine ni ya ajabu kabisa. Mtu anawaita nyani akiwa kwenu halafu mnalalamika? Hata nyani ukiwachokoza lazima wakushughulikie.
Waliotukanwa wamepoteza fursa ya kutoa fundisho kwa huyo mpumbavu na kwa wengine wenye mawazo kama yake!
Tunatakiwa kuwafundisha watu wetu kumalizana kimya kimya na wapuuzi kama hawa! Siyo lazima kufuata sheria kwa mambo ya kipuuzi, mnadhalilika, pia siyo lazima kutangaza!
 
Back
Top Bottom