Mfanyabiashara wa madini Arusha kortini

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
752
1,810
Mfanya biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Mushi (30) maarufu kwa jina la sullu, amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa glassi usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na wadhamini wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya .
94e6fd630c79b3a385e75d2b6dd5fa1f.jpg
24f65477de160f0e21efe7d58340ee3e.jpg
 
Duuh, ndoano tena... Alimkuta akigegedwa nini?

Mbina hasira ya kumuumiza mwenzake namna hiyo. Dawa ya mwanamke wala siyo kumpiga na kumuumiza, kwani ulizaliwa naye.

Apite kushoto na mimi kulia,, wanawake wapo wengi tu, ya nini kutoana manundu. Mama si hatujazaliwa wote, tumekutana tu ukubwani,, shika hamsini zako niache na maisha yangu:cool:
 
Utafiti usio rasmi unaonyesha watu wa ukanda wa kaskazini kuanzia West Kilimanjaro, Arusha yote tambarare ya serengeti na mkoa wa Mara,
Wanahitilafu katika ku Control Temper hii inasababishwa na nyama za maeneo hayo na maji.
Kuna madini ambayo humfanya mtu kushindwa kujizuia.
severe_dental_fluorosis.jpg

Uharibifu huu huenda mpaka kwenye ubongo.
 
OMG! Hivi mtu anaekupenda anaweza fanya hivi jamani! Hapo hakuna ndoa tena huyo dada bado ni mdogo sana asonge mbele na maisha yake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Utafiti usio rasmi unaonyesha watu wa ukanda wa kaskazini kuanzia West Kilimanjaro, Arusha yote tambarare ya serengeti na mkoa wa Mara,
Wanahitilafu katika ku Control Temper hii inasababishwa na nyama za maeneo hayo na maji.
Kuna madini ambayo humfanya mtu kushindwa kujizuia.
severe_dental_fluorosis.jpg

Uharibifu huu huenda mpaka kwenye ubongo.
Mmmmh! Labda upande wa mara ila kwingine i doubt
 
Pole yake . baada ya kupona anaenda kuomba kesi ifutwe wakaongee nyumbani. Siku mbili mapenzi moto moto. Mdomo koma
 
dogo pesa zinampa jeuri ...... kumuumiza hivyo ndiyo nini sasa? utakuta kisa mchepuko
 
Yaani tukio lilitokea March 2016 alafu mashitaka January 2017 ?
kwenye hili tukio kuna nini chini ya 'kapeti'
 
Mfanya biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Mushi (30) maarufu kwa jina la sullu, amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa glassi usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na wadhamini wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya .
94e6fd630c79b3a385e75d2b6dd5fa1f.jpg
24f65477de160f0e21efe7d58340ee3e.jpg
Nilisikia mahali familia nzuri ni ile Baba kamzidi mke umri, urefu na kipato; sasa hawa marika wanaoana si lazima watakuwa wanashikana huko ndani? Mke hawezi mwamkia mumeo shikamoo maana wanalingana kiumri na isitoshe yeye ni mrefuko kuliko mumewe
 
Back
Top Bottom