RAHA KAMILI
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 203
- 84

Kampuni ya Umoja switch imewazawadia washindi wake zawadi walizoshinda kwenye droo ya Shinda na Umoja Switch iliyochezeshwa January 16 mwaka huuKatika droo hiyo ya kwanza ilitoa washindi katika vipengele vinne ambavyo ni, Mshindi wa fedha taslimu Milioni moja, washindi wa fedha taslim mara mbili ya muamala aliyofanya kwenye ATMs za UmojaSwitch, washindi watano wa Simu za mkononi (Smart phones) na washindi zaidi ya 20 wa T-shirt za UmojaSwitch
Akiwakabidhi zawadi hizo za afisa masoko wa Umoja Switch Umoja Beatrice Emmanuel amesema anawashukuru wateja wa Umoja Switch kwa kuendelea kutumia kadi za Umoja Switch na amewataka wale ambao hawajabadili kadi zao wafike kwenye Benki zao ili kubadilisha kadi zao na waingie kwenye droo ya Pili ya Promosheni hii ya Shinda na Umoja Switch
Akizungumza na waandishi wa habari bi Paulina Cosmas Kigolo ambae ni mjasiriamali na mmiliki wa Boda boda amesema hakutegema kama angekuwa mshindi wa fedha hizo kwani kwa mara kadhaa amekua akitumia kadi kadi yake ya umoja Switch kufanya miamala na hakuwa akijua kama kuna zawadi zinatolewa kwa watumiaji wa kadi za Umoja Switch hivyo kwake lilikuani jambo la kushangaza
“Kiukweli mara ya kwanza napigiwa Simu sikuamini kabisa kwa sababu sikuwa nikijua kama kuna promosheni inachezeshwa, kwa hiyo siku napigiwa kwakweli sikuamini kabisa, mi nawashauri wateja wazidi kutumia kadi za UmojaSwitch ili nao washinde kama mimi” alisema bi KigoloKwa upande wa mshindi wa pili wa fedha taslimu mara mbili bi, Catherin Mbogela amewashukuru sana Umoja Switch kwa kuanzisha promosheni kwa sababu inaonyesha kuwajali wateja wake
Umoja Switch leo imechezesha droo yake mwisho ambayo washindi wake watatangazwa hivi karibuni.