Mfanyabiashara adaiwa kutishia kuua wandishi wa habari

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,109
Posted Date::10/26/2007
Mfanyabiashara adaiwa kutishia kuua wandishi wa habari
*Kisa kuripoti kesi yake ya wizi mahakamani
*Asema ataua na kuwachomea nyumba zao

*Mmoja wa wandishi hao avamiwa na majambazi

Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mwananchi


MFANYABIASHARA maarufu mkoani Arusha, Samson Laizer anatafutwa na polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuwatishia kuwaua kwa maneno waandishi wa habari.

Habari zilizopatikana jana na kuthibitisha Kaimu Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha,Winceslauce Magoha zinaeleza kuwa mfanyabiashara huyo,anasakwa kufuatia kufunguliwa jalada la kesi ya jinai namba AR/RB/12252/2007 katika kituo kikuu cha polisi Arusha Oktoba 22 mwaka huu.

Mfanyabiashara huyo ambaye rafiki wa karibu na kiongozi mmoja mkubwa serikalini, alitishia kuwaua mwandishi wa gazeti hili Mkoa wa Arusha, Mussa Juma na Jamila Omar wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Oktoba 15 mwaka huu.

Juma akielezea tukio hilo alisema, Mfanyabiashara huyo alitoa vitisho hivyo saa 7:00 mchana baada ya yeye kurejea ofisini kutoka mahakamani ya Hakimu mkazi wa mkoa ambako alikuwa na Mwandishi wenzake Jamila wakiliripoti kesi inayomkabili mfanyabiashara huyo ya kuvunja na kuiba ambayo iliyofunguliwa na Abdul Gayum.

Alisema akiwa ofisini alipigiwa na Laizer kupitia simu yake ya mkononi akimtaka aache kuiandika hiyo stori,lakini alipomweleza kwamba hawezi kumfundisha kufanya kazi ndipo alipotakata simu.

Juma alisema baadaye akiwa na mwandishi wenzake Jamila katika Baa ya Washington saa 11:00 jioni, Laizer aliwatishia kuwaua na kuwachomea nyumba zao kama wataendelea kuifuatilia hiyo kwa ajili ya kuichapisha au kuitangaza katika televisheni.

Nyinyi endeleeni tu kuifuatilia hiyo kesi , mkiandika ikitoka nisipowaua nitawachomea nyumba zenu moto, alisema Juma akikariri maneno ya Laizer.

Alisema mbali ya kuwatishia kuwaua aliwaambia kuwa kesi yake inakwenda vizuri anashangaa waandishi wanaingilia kuiripoti.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu kazi Judith Kamala na inatarajiwa kutolewa uamuzi Novemba 13 mwaka huu kama mfanyabiashara huyo anakesi ya kujibu au la.


Baada ya kutoa tuhuma hizo na vitisho, Juma alisema aliandika habari hiyo na kuituma chumba cha habari cha gazeti la Mwananchi na ikachapishwa Oktoba 17 mwaka huu.

Alisema baada ya habari hiyo kutoka, siku hiyo saa 6.00 usiku majambazi zaidi ya 10 walivamia nyumba yake wakiwa na silaha mbalimbali.

?Hata hivyo, walishindwa kuingia ndani ya nyumba baada ya kufanikiwa kupanda ukuta wa uzio wa kutokana na mlinzi wake kupiga filimbi na polisi wa doria kuwahi kufika bada ya kupigiwa simu.

Alisema Oktoba 18 mwaka huu , Mfanyabiashara huyo alizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa magazeti ya This Day na Kulikoni, Mack Valantine Kwame, na kusisitiza kuwa ataendelea kupambana na waandishi hadi watakapoacha kumfuatilia.

Katika mazungumzo hayo ambayo yamerekodiwa, Mfanyabiashara huyo alidai kuwa waandishi Juma na Jamila kwa muda mrefu wamekuwa wakimfuatafuata na lazima atawashughulikia.

Hata hivyo, hadi jana mchana, askari mpelelezi wa kesi hiyo, Sajenti Kaitira alisema walikuwa wakiendelea kumsaka mfanyabiashara huyo mkoani hapa bila mafanikio.

Alisema alipoongea naye jana kwa njia ya simu Laizer alisema yupo jijini Dar es Salaam na angekuja Arusha? Novemba 11 mwaka huu.

Nimemwambia aje hapa Arusha polisi hiyo Novemba 11 lakini kama yupo mjini mkimuona naomba mtupe taarifa tumkamate,alisema Kaitara.

Katika siku za hivi karibuni baadhi ya wafanyabiashara na viongozi wa serikali wamekuwa wakitishia waandishi wa habari ili kuacha kuandika habari zinazowakabili.
 
jambo ni uzi wa zamani ila upo mtindo wa waandishi kutumika kumchafua mfanyabiashara au kampuni husika na lengo lao na kupewa hela au unakuta wanapewa hela na mahasimu wa mfanyabiashara au kampuni husika
 
Back
Top Bottom