SI KWELI Mfamle Mswati III atangaza kuwanunulia nyumba na kulipia gharama za harusi wanaume wanaooa wanawake watano kwenye nchi yake

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na barua inayiosambaa Mtandaoni ikionesha kuandikwa na Mfalme Mswati III ametoa tangazo linalodai kuwa kutokana na uhaba wa Wanaume kwenye nchi yake, amewaomba wananchi wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara kuomba uraia kwenye nchi yake, na kila mwanaume atayeoa walau wanakwake 5 atamlipia gharama za harusi zao pamoja na kuwanunulia nyumba.

FAKE uswatini letter.jpg


Ukweli wa taarifa hii upoje?
 
Tunachokijua
Machi 8, 2024, barua yenye saini ya Mfalme Mswati III ilianza kusambaa kwenye mitandao ya Kijamii. Sehemu ya Maneno yaliyoandikwa kwenye barua hii yanasema;

"Mimi, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland, nawakaribisha raia kutoka Mataifa ya Kusini mwa Afrika kuomba uraia katika ardhi yangu, na hii ndiyo ahadi yangu, oa angalau wake watano, serikali yangu itagharamia sherehe za harusi na kununua nyumba kwa ajili yenu."

Aidha, ombi hili la Mfalme Mswati III lilikuja baada ya kuwepo wa uhaba wa wanaume nchini Swaziland (Eswatini), na kwamba Fomu za maombi kwa zoezi hili zinapatikana katika ofisi za umma za Mataifa yote ya Kusini mwa Afrika isipokuwa Malawi.

Ujumbe huu uliteta shauku kubwa miongoni mwa watu na baadhi walitaka kufahamu ukweli wake ndipo JamiiCheck ikaamua kufuatilia undani wake.

Matokeo ya ufuatiliaji wa JamiiCheck
Kwa kutumia utafutaji wa maneno 'King of Swaziland', JamiiCheck ilipata watu kadhaa waliochapisha taarifa hii kwenye mtandao wa kijamii wa X. Baadhi ya taarifa hizo zimehifadhiwa hapa, hapa na hapa.

Aidha, utafutaji mwingine wa JamiiCheck umebaini Mei 14, 2019, Jarida la Eswatini Observer liliwahi kukanisha madai mengine yanayofanana na haya. Wakati huo, Mfalme Mswati III alinukuliwa akisema ilikuwa ni lazima kila mwanaume aoe wanawake wengi, na ambaye hakufanya hivyo angefungwa Jela.

Siku moja baadaye, Mei 15, 2019, taasisi ya uhakiki wa taarifa inayoitwa AFP Fact Check ilikanusha pia madai hayo kwa kunukuu sehemu ya maneno yaliyotolewa na Serikali ya Eswatini yakisema taarifa hiyo ilikuwa ni dhihaka kubwa kwa Mfalme wao, pia ni tendo linalotia aibu tasnia ya uandishi wa habari.

Barua ya Sasa ni halisi?
JamiiCheck imefanya uhakiki wa barua hii ili kugundua usahihi wake. Baadhi ya mambo tuliyogundua ni uwepo wa mashaka juu ya utofauti wa saini ya Mfalme Mswati. Kwa mujibu wa nyaraka rasmi ya Serikali ya Eswatini, saini ya Mfalme Mswati haifanani na hii iliyowekwa kwenye barua ya sasa.

Pia, taarifa hii haijtangazwa kwenye chanzo chochote cha kuaminika, ikiwemo kuchapishwa kwenye tovuti kuu ya Serikali pamoja na Akaunti rasmi za Serikali hiyo kwenye Mitandao ya kijamii.

Pia, utaratibu wa kuomba uraia wa Ewatini uliotajwa kwenye barua hii unakiuka mwongozo kamili wa kuomba uraia kama ulivyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi hiyo ambapo mwombaji hupaswa kujanza maombi Online.

Baada ya ufuatiliaji huu, JamiiCheck ilipata pia taarifa rasmi ya Serikali ya Eswatini iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, saa 1:58 Jioni ya Machi 10, 2024 ikikanusha barua hiyo. Tazama hapa.

Kwa kurejea mapungufu ambayo JamiiCheck iliyabaini kutoka kwenye barua hii, pamoja na taarifa rasmi ya Serikali ya Eswatini, tumejirisha pasipo shaka huwa taarifa hii haina ukweli.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom