Naona umeyashupalia makanisa ambayo siyo ya "Kiroho" tu!! Vipi kuhusu hayo ya Kiroho unayosali wewe mtoa mada, hayajishughulishi na huo upigaji? Mfano Kanisa la Efatha, halikuwahi kuingia kwenye mgogoro wa ardhi na watu wa Rukwa? Halikuwahi kumiliki benki?
Vipi kuhusu kanisa la Gwajima, Mama Lwakatare, Kakobe, Mzee wa Upako, nk. Unayajua mapato na matumizi yao? Kuwa fair na uachane na ubaguzi wa kiimani!
Baada ya kuondokana na siasa za Ujamaa na Kujitegemea, tuliruhusu watu binafsi kuwekeza kwenye huduma za kijamii kama ujenzi wa shule, hospitali, nk. Wewe kama unaona huna uwezo wa kumpeleka mwanao St. Francis, basi mpeleke kwenye shule za magufuli za elimu bure, St. Kayumba! badala ya kulialia. Siku zote vitu vizuri vina gharama.
Unapoamua kuongelea uozo wa hizo taasisi/madhehebu ya kidini, usijitoe ufahamu na kubagua. Ongelea kwa ujumla wake, sababu hayo madhehebu yote, mpaka Bakwata! yana madhaifu na mazuri yao pia.