Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,798
Nmemfahamu huyu mama anaejiita Mfalme Zumaridi miaka 2 iliyopita. Nilivyoiona ibada na tabiri zake tu nikajua huyu ni mpigaji kama ilivyo kwa wapiga wengine. Lakini kabla hatuja mkosoa au kushangaa kwanini serikali imemfungia hebu tujiulize je kwenye makanisa yetu kuko salama?
Achana na akina Mwamposa tuyachunguze haya haya makanisa yanayojiita makubwa na yasioamini sanaa mahubiri ya miujiza ya mitume na manabii. Makanisa ambayo si ya kiroho kwani yale ya Kilokole yanaitwa ni ya Kiroho japo sijui kwanini. Haya ni makanisa ya Katoliki, Moravian, Anglican, Wasabato na KKT. Hawa wanajiona wako sahihi sana.
Mimi kwa mtazamo wangu tena nikiwa mkristo niliewahi kusali kwenye haya madhehebu kuna kutu na ukakasi ambao hausemwi ktk ishu ya upigaji kwa kutumia jina la Yesu.Ukweli ni kwamba makanisa haya yanaendelea kupiga pesa watu kwa kisingizio cha kutoa kuhuma, Kivipi nitaeleza
1. Haya makanisa yanatumia jina la Yesu kufanya biashara kubwa kupitia mashule, vyuo, maduka ya madawa na mahospitali, mashamba n.k Leo hii shule, na hospitali zinazomilikiwa na Wakatoliki, KKK Wasabato n.k ndio zinazoongoza kuwa na gharama kubwa. Wanaosoma kwenye shule za Mission ni wale wenye kipato kikubwa tu na si vinginevyo. Miminilitegemea shule na hospital za dini na madhehebu ziwahudumie watoto, wazee na wajane ambao ni fukara na maskini.
Ule upendo mkuu tulioachiwa na Yesu uko wapi? Njooni wote wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha. ( Mathayo 11:28) . Kwenye kikao chake na viongozi wa dini Mh. Rais Magufuli aliwachana live viongozi wa kanisa Katoliki na kushangaa kwann hospitali zao zina gharama kubwa sn licha ya kuwa na ubia na serikali.
Mnakumbuka elimu ya juu ilivyotaka kuharibiwa na vyuo vikuu vya Dini kabla ya serkali kuingilia kati?Ilikua pesa mbele kuangalia cheti na ufauru wa mtu. Biashara nyingi za makanisa hazipo kwa ajili ya huduma za jamii bali ni biashara km biashara zingine. Mara ngapi tumeona na kusikia kanisa likigombeana Ardhi na wananchi mpaka kupelekana mahakamani.
Kuna makanisa yanafanya biashara ya mabenki kwa kutumia sadaka je hivyo maandiko ya Biblia yameagiza?. Tunaomshangaa Zumaridi tulitakiwa kushangaa yanayoendelea kwenye makanisa yetu. Ujanja wanaoutumia ni kuwa karibu na serikali ndio maana hata mapungufu yao hayakemewi Msiwaone kusifia kila kitu cha serikali lengo ni kuwa salama.Upigaji ni ule ule sema mbinu ndo tofauti. Ukifatilia kiundani zaidi ni makanisa machache sn ambayo kweli yapo kwa ajili ya kusudi la Mungu.
Kama Zumaridi angekua karibu na chama ipo siku mngemuona apiga maombi uwanja ndege akipokea Bombadia.