Mfalme Mzee Yusuph amethibitisha kurudi kwenye taarabu

Hatimaye mfalme wa taarabu Alhaji Mzee Yusuph ametangaza rasmi ujio wake kwa mara nyingine kwenye muziki wa taarabu.

View attachment 1389678

Kwa kifupi tangu mfalme akae nje ya muziki wa taarabu , muziki wa taarabu ulikosa radha kabisa maana waimbaji waliobaki wanapiga piga kelele tu cha maana wanachokiimba hakuna.

Tumemiss kusikia ngoma kali za kipindi kile kama vile Wasiwasi Wako ndio maradhi yako,My Valentine, mpenzi chocolate, VIP, Wagombano ndio wapatanao , Two in One nk.

View attachment 1389681

Mzee Yusuph alifanikiwa kuibua vipaji kadhaa cya wasanii wanaofanya vizuri kwenye muziki wa taarabu kama vile Abuubakar Sudi (Prince Amigo) ,Mohammed Ally (mtoto pori), Isha Ramadhani (Isha Mashauzi), Fatma Mahmoud (Fatma Nyoro), Rahma Machupa (Messi) ,Mwasiti Kitoronto nk.

Kwa sasa wasanii walioibuliwa na mzee Yusuph wanafanya vizuri kwenye bendi zao mpya wanazofanya kazi, mfano Fatma Nyoro ni msanii tegemezi wa Yah TMK , Rahma Machupa na Mohammed Ally na Mwasiti Kitoronto ni wasanii tegemezi wa Nakshi Nakshi Modern taarabu chini ya father Mauji na Chidy boy.

View attachment 1389683


Mashabiki tunamsubiri kwa hamu mfalme aturudishe kundini mashabiki zake tulioacha kusikiliza taarabu tangu yeye ajiweke kando na muziki huo.

Na kwa hakika jamaa atapigahela sana .
Hawakukosea wahenga waliposema usitoe ahadi yoyote ukiwa na furaha.

Jamaa katoka hijja. Furaha ya kumrudia muumba kautangazia ulimwengu kwamba anaacha muziki, sasa hivi anarudi tena kwenye muziki Huo huo alio tangaza kuupa kisogo...

It is like he takes God for a joke or something
 
Ni NJAA TU ,,ndy INAYOMSUMBUWA,hakuna KINGINE..wakati ule anatangaza KUSTAAFU TAARABU alikuwa na Biashara KIBAO..NADHANI SASA HANA TENA.,,story YAKE inanikumbusha JAMAA MMOJA NILIKUWA NIKIMFAHAMU AMBAYE SASA NI MAREHEMU.,,alichukuwa KITABU CHA QURAN akaapa kwa MUNGU kutorudia BIASHARA FULANI AMBAYO alikuwa AKIIFANYA HAPO AWALI....jamaa baada ya KUPIGWA NA NJAA KWA MUDA,,,akaanza KUTAFUTA MASHEKH WAMFUNDISHE JINSI YA KUTENGUA KIAPO CHAKO...mwisho jamaa AKARUDI KWNY BIASHARA ZILE ALIZO JIAPIZA....hakuchukuwa ROUND HATUNAE TENA...hivyo BASI ANACHOPITIA MZEE YUSUPH NI MAJARIBU YA YALE ALIYOYASIMAMIA MWANZO... ,,,Nakumbuka video YAKE ALIYOITOA HUKU AKITOKWA MACHOZI akisema kwamba ALIPOKUWA KWENYE TAARABU ALIKUWA ANAPOTEA na ANAPOTEZA WATU.na NYIMBO ZAKE ZISIPIGWE. TENA REDIONI NA KWENYE TV NA HATA VYOMBO VYA MUZIKI ALIUZA...,,,,sasa iweje Leo ARUDI?au sasa TAARABU IMEHALALISHWA MBELE YA MUNGU? ajitathmini Mara mbili..NJAA BABA YAO...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunajua ni shida za dunia, haswaa kwa mtu aliyezoea kushika mipesa pesa,
Sema nae Mzee si angeimba Qaswida basiii wengi wangemsapoti kuliko kurudi kwenye Taaraabu atajiharibia siha yake.
 
Nilishangaa sana, bila majibu, huyu mtu wa watu kutoka ktk huu muziki wa Taarabu. alidanganywa na wapiga hela wa Dini. kupitia Dini kuwa anacho fanya ni dhambi. kumbe Dini yenyewe ilianzishwa Vatican ili kuvuruga Maisha ya watu. Prince Katega kamfungua Macho!

sasa anarudi kwa kasi! leo anapiga Bahari beach Motel kule Kunduchi
Wapiga hela kwenye uislam hakuna labda huko Vatican huku imani tu... na hata hizo kaswida unazozisikia watu wanaimbia kwa mapenzi tu ya mwenyezi mungu na mtume lkn hamna kipato chochote kitakachokufa labda utegemee ndo iwe kazi.... tofauti na uko walter chilambo game imemshinda kaamua kukimbilia huko kwa midundo ile ile na style zile zile kasoro maneno kabadilisha kidogo tu anapiga hela...
N.b... maisha anayoishi imamu wa msikiti wa mtoro ni tofauti kabisa na life analoishi kasisi wa kanisa la s.t joseph.. kifupi huku imani tu swala maisha ni juu yako sio hakuna upigaji huku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom