Mfahamu the Green Mamba

Sikumbuki ni mwaka gani lakin huyu nyoka nishakutana nae juu ya mti wa mpera,kwa bahati nzuri nlikua na panga sa ile nmemwona akiwa karibu yangu lile shina alokuwepi nikaligonga na panga akaanguka chin akapotelea kweny majani
 
Tuliwahi kukutana na Black mamba jioni tukiwa tunatoka kuwinda digidigi porini, nilikuwa na Uncle wangu ana Riffle yenye Binocular tulimzawadia risasi moja ya kichwa biashara ikaisha, nyoka na Binadamu wapi na wapi?
 
Nilikuwa na mwembe ilinidi nilate maana walikuwa hawaishi kwenye huo mwembe juzi kati nikamkuta kwenye mgomba wakati nakata ndizi
 
Green mamba hata siyo hatari kama mtoa mada ambayo anataka kutuamininisha na thread yake , nimecheza nao sana , Ukifika machame nkuu muulizie Riri utaambiwa tabia yake ya kuwafuga hawa viumbe since Akiwa std 2 Mpaka sasa hivi kaachana nao kashakuwa mkubwaaa
 

Green mamba ni wengi sana katika misitu ya Handeni-Tanga, enzi hizo natembea maporini haswa wakati wa mvua ukipumzika tu utashangaa ukiangalia juu ya matawi ya miti lazim umuone, nadhani wangekuwa wakali kwa kipindi nilichofanya hizo kazi ningalikuwa nishakufa
 
Hawa ndio wale nilikuwa nakutana nao sana kwenye mipera enzi zile za utoto...
Kwenye mikorosho noma Sana hasa ukipanda juu kutungua bibo utakutana na huyo kiumbe mzito,
Miaka ya 80 nilikutana naye tabata dampo kwenye mikorosho ya watu ebwanae wacha nijirushe toka juu ya mti na kutoka nduki Kali,
Maumivu nilienda kuyasikilizia home!!!
Ila ni kweli hawa nyoka hawana madhara Hadi wachokozwe
 
Huyo nyoka ni mjanja sana aisee..... ukimuona halafu ukageuza macho kidogo tu humuoni tena....
Sahihi a'fu wanauwezo mkubwa kukwepa mawe pindi wanaposhambuliwa.
Wazee wetu Zama hizo walikuwa wakituambia kwamba hivi vijamaa vinapenda kugonga kichwani hivyo vilikuwa na uwezo wa kupaa hewani na vikikugonga huponi.
 


Sio hawa mkuu tunaowaona ukitaka kuwatofautisha angalia midomo yao kama nikivyosema hapo wao wana midomo yenye rangi nyeupe na kijani kilichokolea sana
 
Huyu mdudu nimpore sana,tanga kuna kabila moja huluhusiwi kumuua huyu,na hata akiingia ndani wanadai ni baraka,ninyoka anae kaa kwenye miti hasa ile yenye kijani kibichi kama yeye.
 
Black mamba""""koboko""" acha bwana Yule kiumbe mimi naona huyo nimpole sana.
 
Hawa nyoka ni wapole sana,kule mbeya kwenye majani ya migomba nimekutana nao sana,lakini kwa ukubwa wa saizi hiyo sijawahi kuwaona.
Wale saizi yao ya kati.
 
mimi niliwahi kumjeruhi,akantoroka baada ya mda nko maeneo ya shamba naskia kitu kama kinanifata kugeuka nkamwona ananifwata kwa speed,nkakimbia bado yuko na mimi nkawahi rungu nkammalizia,alikua na jeraha nkagundua aliniwekea kisasi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…