MFAHAMU NYUMBU

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,685
MFAHAMU NYUMBU

Anafahamika kwa sifa kubwa ya ujinga, pengine kutoeleweka kwa urahisi matendo yao ndio maana hupewa sifa hiyo mbaya ambayo kimsingi hawastahili kuibeba, ni mnyama ambaye huwa na kilo kati ya 140 mpaka 280, utofauti wa kilo hutokana na umri, afya pamoja na jinsia ambapo madume huwa wazito zaidi, chakula chao kikuu ni majani, hupendelea zaidi nyasi fupi, umri wa kuishi hufika mpaka miaka 20 japokuwa huweza kuzidi zaidi ya hapo, wanapendelea kukaa katika makundi na marafiki wao wa jilani ni pamoja na pundamilia na swala, uwezo wa kukimbia ni km 85 kwa saa.

Wanyama hawa hupatikana Afrika tuu, na si nchi zote wapo Angola, Botswana, Kenya, Mozambique, Namibia, South Africa, Swaziland, Zambia, Zimbabwe huku hapa nyumbani Tanzania wakiipa umaarufu nchi yetu kutokana na balaa lao ambalo hulifanya huko Serengeti linaloingia katika maajabu ya Dunia na kupewa jina la kizungu : The Great Wildebeest Migration, ambapo husafiri km zaidi ya 800 (sawa na umbali wa kutoka Dar es salaam mpaka Mbeya) usijefikiri wanapanda kitu hapana ni kwa kukimbia tuu, ambapo huwa milion moja na nusu mpaka milion mbili, wakitoka Tanzania kwenda nchi jilani na baada ya hapo hugeuza tena, katika safari yao hiyo nyumbu zaidi ya laki mbili na nusu hufa kwa sababu ya ajali, kuuwawa na wanyama wala nyama, njaa pamoja na magonjwa.

Wanyama wanaowawinda sana viumbe hawa ni pamoja na Simba (Mfalme), Fisi (bwana afya), Mbwa Mwitu (wazee wa heka heka) pamoja na chui, duma (mapaka), katika jamii yao nyumbu huwa wanasaidiana katika tatizo lolote lakini si kutoana kwenye midomo ya vifo, ukinaswa huko hilo ni lako, kidogo majike huonesha ubabe pale watoto wao wanapokamatwa na hii ni kutokana na ile siri ya uchungu wa mwana, hili ni moja kati ya jambo ambalo huwafanya binadamu kusema kwamba nyumbu ni wajinga kwakuwa wao wanakuwa wengi lakini wanamkimbia labda simba mmoja, tuseme sawa basi mfano huo tuugeuze kwa binadamu hivi pasina ya kushika silaha binadamu wakiwa wengi akitokea simba mmoja mtasimama ? Mara paaap kariakoo limedondoshwa simba dume nafikiri kwa binadamu inaweza kuwa zaidi ya nyumbu maana binadamu wengine watakufa kwa kukanyangwa na binadamu wenzie ?

SIFA ZAO.

1. Hubeba mimba kwa kwa umri sawa na binadamu miezi tisa, ingawa wengine huzaa hata kwa miezi nane.
2. Jike anapozaa si lazima atulie anaweza kuendelea na shughuli nyingine huku tendo hilo likiendelea
3. Muda mfupi tuu baada ya kuzaliwa mtoto wa nyumbu huanza kutembea, na hii humsaidia mtoto kwakuwa maisha yao ni ya kuhama hama.
4. Nyumbu ni miongoni mwa wanyama ambao ukimpiga picha rangi yake hutofautiana kidogo na rangi zao, wana rangi nzuri sana ya kuvutia tofauti na tuwaonavyo katika picha hizi.
5. Hulala kwa zamu, kwa mfano wakiwa kumi watano watalala huku watano wakiwalinda wenzao na wanyama wakali, na muda ukienda itakuwa zamu yao kulala na wenzao kupiga ulinzi.
6. Sauti watoazo huelewana kwa urahisi kwamba kuna hatari au vinginevyo.
7. Katika jamii zao ukikaa mbele ndio umeukwaa uongozi hawapigi kura kama mbwa mwitu.
8. Wanapoamua jambo lao pasina kujari vikwazo vilivyo mbele huwa ni lazima watimize agano lao, ndio maana huweza kuvuka mto hali ya kuwa ndani ya maji washawaona mamba na hapa ndio binadamu mnawasema wajinga, lakini wao hujua wanafanya nini kuliko kundi lote life njaa ni bora wachache waliwe na mamba lakini watakao salimika wakapate chakula ng'ambo ya pili.

9. Jamaa hawa ni wazalendo sana baina yao,huweza jirusha katika bonde kubwa ambalo ana hakika hawezi pona, lakini kwa kufanya hivyo bonde hilo litatengeneza njia kutokana na kumomonyoka kwa udongo na wanaofuata watapita hapo kwa urahisi kabisa ingawa wenzao watawaacha hapo marehemu au vilema, unapoona mchezo huo lazima uwahukumu wajinga.

10. Michezo yao wawapo wawili wawili ni pamoja na kudanganya mmoja kafa na anayebaki atahakikisha anamuamsha mwenzie.

11. Pembe zao ni silaha kali sana kwani zimechongoka mno, ikikupigia ni kama kisu kimepenya.

Kwa sasa nitahishia hapa ila unaweza kuwaelewa zaidi, kwakuwa karibuni nitawachambua kwa undani zaidi katika gazeti la Mtanzania, Je kwa uchache huu bado imani yako haijateteleka kwamba nyumbu ni vilaza ?
 
Asante nimesoma yote.
 
Sa kwanini wema sepetu wakamuita nyumbu?
 
....Huyu atakuwa ndugu wa karibu wa Nyati, angalau kwa mfanano??
 
Kumbe nyumbu wana uzalendo hivi kama watz tungekuwa na uzalendo si tungekuwa ulaya ya pili
 
Kumbe nyumbu wana uzalendo hivi kama watz tungekuwa na uzalendo si tungekuwa ulaya ya pili
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚subiri wadanganyika wakusikie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…