Safi sana.?Aina hii ya mteja ikiwezekana usimuuzie kabisa huduma au bidhaa yako.Ukimuonea huruma sana Mwambie Nenda kanunue Pale kwa bei ya chini uje uniuzie mimi.Akija na mzigo wake mwambie peleka kwako ukatumie wote.
Duh nakuunga mkono kabisa! Hawa wanaopanga bei wanazingua sana.Katika ulimwengu wa biashara,kuna aina mbili za wateja
Kuna wateja ambao ni LOYAL na wateja ambao ni ROYAL mteja ambaye hayuko katika kundi moja katia ya hili basi sio mteja.
Mteja ROYAL ni mteja yoyote yule ambaye ananunua kwako kwa mara ya kwanza au mara kwa mara-Ndio maana kuna msemo mteja ni mfalme.Mteja wa pili ni yule ambaye ananunua kwako mara kwa mara yaani ni loyal kwako.
Sasa hawa wateja wawili ndio wa muhimu sana kwenye biashara yako na ukiwapoteza hao basi utawapoteza wateja wengi zaidi.
Hata hivo kuna wateja wengine ambao bado sijawapa jina ila wanakua na tabia ya kuja dukani kwako na kukuelekeza namna ya kufanya biashara yako kwa maslahi yao.Mfano(Mteja anakwambia mbona kwa fulani tunauziwa bei hii?)Kama anauziwa bei hio si aende akanunue huko?Aina hii ya mteja ikiwezekana usimuuzie kabisa huduma au bidhaa yako.Ukimuonea huruma sana Mwambie Nenda kanunue Pale kwa bei ya chini uje uniuzie mimi.Akija na mzigo wake mwambie peleka kwako ukatumie wote.
Kwa nini nasema huyu ni mteja wa kupotezwa na kupotezewa?Ni kwa sababu yeye anataka kukufundisha wewe jinsi ya kufanya biashara yako bila kujali maslahi yako.Unapofanya biashara,una malengo na unaelewa ni nini unataka kupata,Mtu anapokupangia BEI anakosa adabu.Kupangiwa bei ni tofauti na kuomba discount-Mteja anaeomba discount sio sawa na anayekupangia bei.
Kila heri
Aiseeee wanaboa sanaDuh nakuunga mkono kabisa! Hawa wanaopanga bei wanazingua sana.
Mkuu,Biashara inahitaji uvumilivu,ukiwa na hasira unaweza kupoteza wateja wengi; mteja anayekupangia bei jaribu kumuelewesha kwanini bei ya bidhaa au huduma yako ni tofauti na sehemu nyingine, unaweza kutumia pointi za ubora n.k. Cha muhimu jitahidi kumu-win mteja yeyote anayekuja kwako
Ni kweli wanaudhi,ila wanamna hiyo unaweza kumjibu, inategememea na anapochukulia mzigo,yawezekana huko alipochukulia hatozwi kodi n.k ndio maana bei yake iko chiniMkuu,
Kuna wateja wa kueleweshwa na wakija unawaelewesha ila kuna wapanga BEI.Huwa wanaanza na "MBONA" fulani anatuuzia bei flani?Akianza hivo ndugu yangu huyu ni chuma ulete.Mteja wa kueleweshwa atakuuliza kwa nini?huku analipa hatakutajia bei ya mshindani wako mpaka aone kuna ulazima.
Mkuu umewahi kutana na mteja wa aina hii?Huwa wanakuwa na tabia ya kutaka kukufanya wewe ama ujisikie vibaya,ujione mwizi,uone aibu.Huwa sio hao unaoelezea wewe wa kuambiwa kuwa kuna sehemu sijui hawalioi kodi.Ni kweli wanaudhi,ila wanamna hiyo unaweza kumjibu, inategememea na anapochukulia mzigo,yawezekana huko alipochukulia hatozwi kodi n.k ndio maana bei yake iko chini
Mimi isemi uwe na kisirani,Nasema hivi kwamba kuna aina ya wateja ambaohawaheshimu biashara ya mtu.Wanfikiri maslahi yao tu.Na mbaya zaidi wanakufanya wewe huijui biashara yako.Hao sio wateja wa kutumia nguvu kumshawishiMkuu biashara kwako itakuwa ngumu ukiwa namna hiyo, mteja hata aje kwa gia gani lazima ujue namna bora ya kum win.
Akijifanya mjuaji na wewe ukashupaza shingo baishara haita songa mbele. Hakikisha unamu win tu.
Usiweke kisirani na mteja.
Nilikuelewa vizuri tu, ujue kuna wateja ambao wana taarifa ambazo sio sahihi juu ya bidhaa fulani, so, akija na 'kukupangia bei' wewe ndo muda wako wa kumuelimisha na kumpa taarifa sahihi huenda akaja kuwa mteja wako wa kudumu hadi ukashangaa.Mimi isemi uwe na kisirani,Nasema hivi kwamba kuna aina ya wateja ambaohawaheshimu biashara ya mtu.Wanfikiri maslahi yao tu.Na mbaya zaidi wanakufanya wewe huijui biashara yako.Hao sio wateja wa kutumia nguvu kumshawishi
Mkuu; Biashara ina Utaratibu wake (Maadili ya kuzingatia) mfano akija mtu ktk eneo la Biashara yako, jiridhishe kwanza je ni Mteja kweli au amekuja hapo kwako kuwa ni kijiweni? Pili chukua tahadhari isijekuwa ni Mwizi au mtu anaetafuta Udhaifu wako ktk biashara yako.Aina hii ya Wateja/Watu - utakuta anachukua muda mrefu sana kupata Bidhaa/Huduma na hata kama ameshahudumiwa bado ataendelea kuwepo hapo na vijihadithi viiingi(Umbea) yaani anaweka kiwingu hapo ktk Biashara yako.Wabongo bwana!! Mtu anajifanya hana shida ya wateja wakati ndio wanaomuweka mjini.
Mpaka najiuliza wenzetu wanafanya biashara za aina gani mbona kama hawabembelezi wateja kabisa?Wabongo bwana!! Mtu anajifanya hana shida ya wateja wakati ndio wanaomuweka mjini.
Wenzetu wana loyal na royal wateja, hawahitaji wengine.Mpaka najiuliza wenzetu wanafanya biashara za aina gani mbona kama hawabembelezi wateja kabisa?
Mteja kukupangia bei tu au kusema mbona kwa fulani wanauza hivi ndio yamtoke hayo yote! Labda kama mteja amekwapua bidhaa na kukimbia nayo hivi hivi mteja kwangu ni mfalme daima. Nipo kwa hili game kwa miaka takribani 10 sasa kumjibu mteja jambo ambalo halijakaa sawa hapana kwa kweli.
Pamoja na kuwa mteja mfalme asivuke mipaka. Kuna wateja kama alivyosema mtoa mada wanataka hadi wakupangie jinsi gani uendeshe biashara yako, unaweza kumpa sababu zote hizo kwanini unauza bei hii au unauza brand hii na sio ile yeye akang'ang'ania msimamo wake kuwa fulani anauza hivi wewe bei zako kubwa (yaani mpigaji) ndio majibu kama hayo yanakuja, kuwa kifupi siwezi kubeat bei ya huyo kiroho safi kachukue kwa huyo na mara nyingi wateja hao huwa wanaishia kununua kwako kwasababu unakuta hata huko anakosema wanauza bei ndogo si kweli anakutikisa tu au wanauza vitu vya kiwango cha chini na anajua.Mpaka najiuliza wenzetu wanafanya biashara za aina gani mbona kama hawabembelezi wateja kabisa?
Mteja kukupangia bei tu au kusema mbona kwa fulani wanauza hivi ndio yamtoke hayo yote! Labda kama mteja amekwapua bidhaa na kukimbia nayo hivi hivi mteja kwangu ni mfalme daima. Nipo kwa hili game kwa miaka takribani 10 sasa kumjibu mteja jambo ambalo halijakaa sawa hapana kwa kweli.
Kuna wateja pasua kichwa, hata humu jf nenda jukwaa la matangazo utaona mifano yao na majibu yao.Wenzetu wana loyal na royal wateja, hawahitaji wengine.