Mfahamu Mpinga Kristo

Mungu akimsamehe Shetani mtajisikia vibaya sana, wale walikaa wote Heaven, Na Mungu kwanza hamchukii shetani, soma Biblia yote!


Hivi akitubu je?

Ila wanadamu duu wanamchukia km nini!
 

Unaleta maelezo marefu sana, lakini tatizo ni kwamba mengi si maneno ya Biblia bali ni tafsiri za watu. Nipe aya moja tu inayosema wazi kwamba Mpinga Kristo atatawala dunia kwa miaka saba, miaka mitatu na nusu ya kwanza ataleta amani, kisha ataanzisha serikali moja ya dunia, dini moja, mfumo wa fedha usio na pesa taslimu, microchip, kompyuta na New World Order. Hakuna aya hata moja inayosema hayo.


Biblia yako inaonya kutoongeza maneno ya unabii:


"Mimi namshuhudia kila aisikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu akiyaongeza juu yake, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki." (Ufunuo 22:18)


Wewe umeongeza mambo ambayo Yohana hakuyasema.


Pia unasema mpanda farasi mweupe wa Ufunuo 6 ni Mpinga Kristo. Lakini Biblia haimtaji hapo kuwa ni Mpinga Kristo. Huo ni mtazamo wa baadhi ya wanatheolojia tu. Wengine wa Kikristo wanaamini farasi mweupe anamwakilisha Kristo au ushindi wa Injili. Kama Wakristo wenyewe hawajakubaliana, unawezaje kusema tafsiri yako ndiyo ukweli wa Biblia?


Yesu alisema:


"Jihadharini mtu asiwadanganye." (Mathayo 24:4)


Hakuwahi kusema "Mpinga Kristo ataanzisha microchip" wala "ataleta mfumo wa cashless."


Kuhusu alama ya mnyama (666), Biblia inasema:


"Hapa ndipo penye hekima; yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya mnyama..." (Ufunuo 13:18)


Haijasema ni microchip, wala RFID, wala teknolojia ya kisasa. Hayo ni mawazo ya waandishi wa leo, si maandiko.


Kisha unasema Wayahudi watamkubali kuwa Masihi. Aya gani inasema hivyo? Hakuna.


Unasema atakuwa Myahudi kutoka Ashuru. Aya gani inasema hivyo wazi? Hakuna. Ni hitimisho la wanadamu, si tamko la Biblia.


Biblia inasema:


"Msipite yale yaliyoandikwa." (1 Wakorintho 4:6)


Lakini umejenga mafundisho marefu juu ya mambo ambayo hayajaandikwa.


Kama kweli unasimamia Biblia, basi simamia maandiko, si vitabu vya wanatheolojia.

Neno la Mungu halihitaji kuongeza New World Order, microchip, kompyuta, serikali ya dunia, wala tafsiri za kisasa ili lisimame.

Ukiongeza yasiyoandikwa, unakuwa unaifafanua Biblia kwa mawazo ya watu badala ya kuifuata Biblia yenyewe.
 
Kijana umechanganya Biblia na uchambuzi wa siasa za kimataifa. Hayo unayosema kuhusu Trump, UN, Britain, EU, Russia, Turkey, Arab League, Vatican, Palestina na "UN Blueprint" hayapo hata aya moja katika Biblia.


Nionyeshe andiko moja linalosema:


Trump atahusika na Mpinga Kristo.
UN itakuwa serikali ya Mpinga Kristo.
Russia na Turkey zitaongoza jeshi la Mpinga Kristo.
Vatican itashirikiana na Mpinga Kristo.
Hekalu la tatu litajengwa pembeni ya Al-Aqsa kwa makubaliano ya UN.

Hakuna hata mstari mmoja unaosema hayo.


Yesu alisema:


"Angalieni, mtu asiwadanganye." (Mathayo 24:4)


Wewe umejaza nafasi ambazo Biblia haikuzijaza.


Biblia pia inasema:


"Msipite yale yaliyoandikwa." (1 Wakorintho 4:6)


Lakini wewe umepita mbali sana kuliko yaliyoandikwa.


Kisha unasema "Mpinga Kristo akija mambo yatakuwa mazuri sana, tule maisha."


Biblia yako inasemaje?


"Ole wao wakaao juu ya nchi..." (Ufunuo 12:12)


"Kwa kuwa kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu." (Mathayo 24:21)


Kama Biblia inasema kutakuwa na dhiki isiyowahi kutokea, wewe unasemaje "tutakula maisha"? Unampinga Yesu kwa maneno yako mwenyewe.


Pia Mtume Paulo anasema:


"Kuja kwake yule mwovu ni kwa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uongo." (2 Wathesalonike 2:9)


Huyo si mtu wa kutamani aje ili "uchumi uimarike"; ni mwovu anayekuja kuwapoteza watu.


Biblia inasema waumini wamngojee Kristo, si Mpinga Kristo.


"Bwana Yesu, njoo." (Ufunuo 22:20)


Sijawahi kuona mtume yeyote akiomba: "Mpinga Kristo njoo ili tule maisha."


Kwa hiyo hoja yako si mafundisho ya Biblia, bali ni nadharia za kisiasa ulizoziunganisha na unabii. Biblia inatufundisha kumngojea Kristo, si kushabikia kuja kwa Mpinga Kristo kwa sababu ya uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…