Mfahamu kinyonga

Kwa kuwa jamaa kaandika kuna aina 100 za vinyonga epuka kumuita Muongo.
 
Asante sana
Ila nafikiri hiyo ya #4 ni hadithi ya kizamani sana (myths) ambayo haina ukweli kisayansi wala kichawi
Kinyonga wapo aina nyingi duniani wapo wanaozaa na wapo wanaotaga mayai wakiwa wamechimba chini kama anavyofanya Mamba
Kinyonga anzaa watoto wengi lakini kama kuna mzee aliona kinyonga mjamzito ambae kwa bahati mbaya alizidiwa uzito na tumbo mpaka kuanguka na kupasusa na watoto kutoka hai hilo nalo neno
Lakini naomba ushahidi zaidi ya huo au kapicha basi akiwa kapasuka

Mengine mengi nimekubaliana nayo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Reactions: amu
Hii ya 16 sidhani kama ni kweli,ni imani tu potofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinyonga wako wanaozaa na wanaotaga mayai.Hao wanaozaa wanazaa kawaida tu aidha juu ya mti au chini kwenye majani au vichaka vidogo,ilo lakuzaa kwakujitupa ili tumbo lipasuke nadhani ni stori za vijiweni tu.
Wanaotaga mayai baada ya watoto kutoka hawadumu zaidi ya miezi 5 wanakufa.
 
Mimi nina uhakika kinyonga anataga mayai. Hiyo ya kuzaa ni hadithi.
 
Mkuu umejitahidi kuuleza lakini kuna makosa mengi ya kitaalamu... Zingine ni hadithi za vile jamii zinavyoamini kuhusu kinyonga(legend/myth) yaani hazina uthibitisho kisayansi...
Vinyonga hawana sumu... Wengi ni wapole(hufura midomoni na kutoa sauti pale wanapohisi hatari, baadhi yao wana meno ncha kuzunguka mdomo hivyo huweza kung'ata) sio hatari sana labda upate maambukizi ya ziada(secondary infection) kwenye kidonda
Hakuna kinyonga anazaa kwa kujiangusha ili apasuke tumbo na kutoa watoto... Kinyonga hutaga mayai na kuenguliwa baada ya siku kadhaa...baadhi ya spishi za vinyonga wanazaa watoto hai...yaani mayai hubaki na huenguliwa mwilini na watoto kuzaliwa
Kinyonga anabadili rangi kutokana na hali (mood) yaani inaweza kuwa hasira pindi madume wawili wanapokutana na kugombania jike, pia hata kumvutia jike,Halijoto (temperature) kama kuna baridi kali vinyonga wengi huwa weusi kuhifadhi joto, kama ni joto kali hubalika kuwa weupe na hili la kujilinda wasionekane kirahisi (camouflage) umelieleza.
NB. Kitaalamu Kinyonga ni aina ya mjusi

Sent from my RMX1971 using JamiiForums mobile app
 
Hahaha! Hili la 16 huuitaji shangazi aisee... Kama unavijua hivi viumbe na unakaujasiri unakamata tu

Sent from my RMX1971 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…