kama kuna Mtanzania anasema tumerudi nyuma compared na 1961 basi huyo si mzalendo au anasukumwa zaidi na utashi wa kisiasa. Utandawazi (ambao ni mfumo mpya wa ukoloni) ndo ulizozisukuma nchi nyingi maskini zikubali kubinafsisha mashirika yao kwa wenye pesa, na hasa baada ya kushindwa ujamaa. Believe me or not, nchi maskini kokote kule duniani zinaendeshwa kwa matakwa ya mataifa makuu kama Marekani, Uingereza etc.
compare it in this way....
ulikuwa unatumia muda gani kuwasiliana na ndg zako kule shamba wakati wa uhuru na sasa ni vipi(it termz za teknohama)?
ulikuwa unatumia muda gani kwenda kijijini kwenu kule kasulu na kwingineko wakati wa uhuru ukilinganisha na sasa?
kulikuwa na watanzania wangapi wenye elimu ya kuanzia atleast secondary hadi uprofesa 1961 compared na sasa?
fursa za ajira kipindi kile na sasa (of course after uwekezaji hasusani sekta ya mawasiliano) ziko sawa?
hivi makazi na malazi mijini na vijijini yalikuwa bora wakati ule kuliko sasa?
uhuru wa habari ulikuwa bora wakati ule kuliko sasa?hivi wakati ule ungethubutu kumtukana rais gazetini na ukaendelea kucheka mtaani?
idadi ya watanzaia wanaoshika nafasi mbalimbali kwenye organs za kimataifa zimepungua/zimeongezeka?
na mengine mengi.
mafanikio ya nchi hayapimwi kwa serikali kuwa na idadi kubwa ya mashirika ya uma yasiyo na tija yeyote kwa mustabali wa nchi
wala hayapimwi kwa porojo majukwaani bali kwa kufanya kazi kwa bidii. Jiulize wewe kama mtanzania mzalendo umefanya nini cha kujivunia kwa nchi yako. na ni ukweli usiopingika kwa yeyote mwenye utambuzi na upeo wa ziada kuwa serikali za nchi masikini kama yetu (ukubali ukatae) huendeshwa kwa matakwa ya magharibi, na bahati mbaya sana huwa tunawatelekeza wale wanaopambana na ufedhuli wao just kwa kudanganywa kidogo tu kama tulivyofanya kwa akina gadafi,mugabe na wengineo ambao tuliambiwa hadithi za kipuuzi tukaziamini. na ndio maana tumebaki watumwa wa fikra kwa wanasiasa mafukara wa hoja wa nchi masikini ambao wapo kwa ajili ya matumbo yao tu hata kama ni kwa kusacrifice wengine....NI KWELI....TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE...ninachoweza ku add kama mtanzania mzalendo ni kuwa (huu ni ukweli) tulitakiwa tuwe mbali zaidi ya hapa kama uadilifu ungesimama miongoni mwa viongozi wetu. ni wakati wa kutafakari kama Taifa...