Mfagiaji (mbeba maboksi) amng'oa Waziri

Mfagiaji (mbeba maboksi) amng'oa Waziri

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
MFAGIAJI AMNG'OA WAZIRI UK:

130710125815_mark_harper_304x171_bbc.jpg

+Waziri wa Uhamiaji, Mark Harper ajiuzulu usiku huu baada ya kugundulika mfagiaji wake hakuwa na vibali halali vya kuishi Uingereza.

Mytake: Tahadhari kwa Watanzania wabeba maboksi - wasio kuwa na vibali halali...!

===
Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.

Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.

Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.

Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.

bbc.
 
Amemng'oa au Waziri amejiuzulu kulinda hadhi yake na ya chama??
 
huyo ndiye kiongozi,. ameonyesha kujali maadili.
jiulize ingekuwa Tz kwetu angejiuzulu?
 
Akijiuzulu mzungu tunampa hongera sana! Akijiuzulu Lowassa, ni fisadi jambazi hafai na kwanza alifukuzwa!

Hehehhehe! My countrymen bana!
 
Kosa la Lowasa ni kujiuzulu ili kuilinda serikali yake ya CCM ilibidi mmoja afe kibudu
 
MFAGIAJI AMNG'OA WAZIRI UK:

130710125815_mark_harper_304x171_bbc.jpg

+Waziri wa Uhamiaji, Mark Harper ajiuzulu usiku huu baada ya kugundulika mfagiaji wake hakuwa na vibali halali vya kuishi Uingereza.

Mytake: Tahadhari kwa Watanzania wabeba maboksi - wasio kuwa na vibali halali...!

===
Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.

Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.

Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.

Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.

bbc.
kwa nchi yetu ni ngumu, mbona wamejaa kila kona na kulindwa na mamlaka za juu? tena wengine wanaitwa wawekezaji
 
huku kwetu mpaka ikulu in a Linda wahamiaji haramu ili kutetea uharamia wa matoto yao
 
Hapo ndipo alipobugi alipopewa uwaziri na kuanza na hii kali ya mwaka kuweka mabango ya kuwatimua wahamiaji nchini,
Kwani wachambuzi wengi wa siasa na waandishi waliponda sana.
Huyu ndie alietegemewa kuwa waziri mkuu in future
 
Back
Top Bottom