singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
MFADHILI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Musoma Mjini, Dk. Eliud Tongola, amejiengua chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na ACT –Wazalendo, chama hicho kimekiri Dk. Tongola kujiunga nacho. Kwa takriban miaka minne alikuwa akilipia pango la ofisi za Chadema jimboni humo.
Dk. Tongola alisema kilichomtoa Chadema ni kuona viongozi wakiwa na wagombea wao mfukoni.
Alisema mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu ndani ya Chadema jimboni humo haukuwekwa wazi badala yake viongozi wa jimbo na wilaya walikuwa wakifanya kila jitihada kuhakikisha mbunge aliyemaliza muda wake hapati upinzani.
"Julai 3 ilitangazwa kuwa siku ya kuchukua fomu, tulikwenda lakini cha kushangaza tulipofika ofisini tuliambiwa fomu hazipo, tulizitafuta kwenye mitandao na kujaza baadaye tuliambiwa uchukuaji fomu umeahirishwa hadi Julai 17 nasi tulikubali," alisema.
Alisema walipata taarifa kuwa Vincent Nyerere, alichukua fomu Julai 10 na kuirudisha siku hiyo hiyo pasipo wagombea wengine kushirikishwa kuhusu mabadiliko hayo.
Dk. Tongola alisema alifuatilia ofisi ya jimbo na hakukuwa na majibu ya kueleweka badala yake waliambiwa uchaguzi utafanyika Julai 22 na uliahirishwa hadi Julai 24 na baadaye Julai 29.
"Walisema mpaka wabunge watoke bungeni, tukasubiri lakini siku mbili kabla ya uchaguzi waliniletea mashitaka wakidai nimeshiriki kuvunja ofisi na kuiba nyaraka za chama na kuzipeleka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema jambo la kusikitisha ni kuona malalamiko aliyopeleka ngazi za juu za chama hicho hayakushughulikiwa kwa wakati na siku ya uchaguzi jina lake halikuwemo.
Ofisa Habari wa Chama cha ACT -Wazalendo, Abdallah Khamis, amethibitisha kumpokea Dk. Tongola aliyejiunga wiki mbili zilizopita na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba.
Chanzo: Raia Tanzania